Global Services High Targets
LEADERSHIP – ENTREPRENEURSHIP – VOLUNTEERING
BRELA ID No: 465066, TIN:
BAKWATA ID: BKT /MDRS/O2O/O1O15
0768649111 – 0675103790 – 0777496444 – 0772496444
Email: gshcourt@gmail , uddgshcourt@gmail
TANZANIA DAR es SALAAM, UBUNGO KWEMBE, MLOGANZILA
UBUNGO, KWEMBE, MLOGANZILA

UISLAM NI NEEMA
الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ
...leo nimekukamilishieni dini yenu na nimetiza neema yangu kwenu pia nimeridhia Uislam kuwa ndio dini kwenu ...
1. Utangulizi
Kama ilivyo jielezea hiyo aaya hapo juu, Uislam ni neema kubwa kuliko neema nyenginezo walizo neemeshwa wanadamu. Kiukweli suala la dini limekuwa mara kwa mara likijadiliwa katika jamii za wasomi duniani kote, kwa taswira baina ya kukiri uwepo wa imani ya MUUMBA na kutokuweko MUUMBA. Hivyo wanaokiri kuweko MUUMBA, huchukuliwa kuwa ni wanadini na wasio kiri kuweko MUUMBA huchukuliwa kuwa hawana dini.
Uislam umekuja na mafunzo kinyume na tulicho kielezea hapo juu, yaani katika mafunzo halisi ya Uislam ni kwamba hakuna mwanaadamu atakaye kuwa bila ya dini, hata neno DINI ni neno la kiarabu lenye maana ya "NJIA". Hivyo yeyote baina ya walimwengu atavyo jiamulia kukiri au kukanusha kuwepo kwa MUUMBA tayari atakuwa amesha jiamulia njia ipi aichukuwe baina ya njia mbili, inayo kiri na inayo kanusha kuwepo MUUMBA.
Hivyo sasa kwa mujibu wa mafundisho ya uislam, kuna dini kuu mbili duniani ambazo ni dini ya wanao kiri kuwepo MUUMBA na dini ya wanao kanusha kuweko MUUMBA.
Bila kujalisha mrengo wa msomaji wa makala haya tunalazimika kuweka andiko kutoka katika kitabu kutukufu cha Uislam, andiko linalo ashiria muono wa dini ya Uislam kuhusa dhana ya dini ya pili.
" وَمَنْ يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَنْ يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ
yeyote atakaye chukua kinyume na Uislam kuwa ndio dini, basi katu hatokubaliwa maamuzi yake hayo bali atakuwa ni miongoni mwa walio ingia khasara huko akhera."
Aaya hiyo hapo juu yaashiria wazi kuwa uislam ni neema kuliko neema nyenginezo. Suala la imani au itikadi ni jambo lisilo epukika kwa mtu yeyote duniani. Hata wanao dai kuto kuamini kuwepo MUUMBA, na wao pia wana itikadi (imani) maana madai yao hayo ndio itakadi na imani walio nayo. Pia watu wanao amini kuweko MUUMBA, na wao pia wamegawanyika makundi:
-
wapo wanao muamini MUUMBA wa haki,
-
wengine wa amini viumbe badala ya imani kwa MUUMBA wa haki
-
wapo wanao amini ngojera na simulizi ... marekani ya kusini kuna imani ya kiumbe aitwaye Melverde .
-
wengine waamini na kusujudia wanyama balada ya MUUMBA.
MOJA YA JAMII YA KIHINDI WAKIWA KATIKA JUHUDI ZA IBADA NA ITIKADI
2. Maana ya Uislam
Uislam una maana nyingi sana ila maana zote huwa hazitoki inje na maana ya "SALAAMA NA AMANI".
-
Siku moja Mtume aliulizwa: uislam ni nini ? Alijibu Mtume kwamba: ni wewe kushahidia kuwa hapana MUABUDIWA wa haki isipo kuwa ALLAH, na kwamba Muhammad (mimi) ni mtume wa ALLAH, na kukasimamisha salah na ukatoa zaka, na ukafunga saumu ya ramadhani na ukahiji nyumba (tukufu aliyo ijenga Ibrahiim na mwanawe Ismail).
-
siku nyengine pia aliulizwa: ewe mjumbe wa ALLAH, nijuze kuhusu Uislam. Akajibu: ni wewe kushahidia kuwa hapana MUABUDIWA wa haki isipo kuwa ALLAH, na kwamba Muhammad (mimi) ni mtume wa ALLAH, na kukasimamisha salah na ukatoa zaka, na ukafunga saumu ya ramadhani na ukahiji nyumba (tukufu aliyo ijenga Ibrahiim na mwanawe Ismail). Halafu akaulizwa papo hapo : nijuze kuhusu imaani (akajibu): imaani ni wewe kumuamini ALLAH na malaika wake na vitabu vyake na Mitume wake na siku ya mwisho na ukaamini qadar (utashi wake ALLAH) kheri na shari . Halafu akaulizwa tena: nijuze kuhusu wema, akajibu Mtume: wema ni wewe kumuabudu ALLAH kana kwamba wamuona, na ukiwa (waitakidu kuwa) humuoni basi hakika yeye akuona. Halafu akaulizwa kwa mara nyengine: nijuze kuhusu saa(ya siku ya mwisho wa dunia). akajibu: sio muulizwaji ndiye anayejua kuliko muulizaji. tena akaulizwa : basi nijuze kuhusu alama zake (ya siku ya mwisho wa dunia). Akajibu: (ni zama ambazo kwamba itadhihiri ) hali ya mzazi kumzaa atakaye mteza nguvu kwa amri (kupotoka maadili), pia wewe kuwaona jamii wenye yenye kaaida ya kutembe peku, mavazi yanayo karibia na kuwa utupu, wakiwa (kwa uchache wao), wachunhaji wanyama, ukawaona wanarefusha majengo (kuibuka na maendeleo makubwa).
Tuliyo yaelezea hapo juu yatoa taswira halisi ya maana ya uislam ... na taswira hiyo hiyo ndio inayo beba nguzo za dini na imani kwa waislam.
3. Ujumbe wa Uislam
Hapa ndipo wanapo feli watu wengi sana pamoja na wao kuzaliwa na wazee wawili waislam au pamoja na kuwa nakuwa wao wamesoma. kiukweli ujumbe wa uislam upo jirani na kuta kufahamika na walio wengi kimatendo na kiitikadi. hali hii ilimlazimu Mtume kusema:
:قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : بَدَأَ الإِسْلامُ غَرِيبًا ، وَسَيَعُودُ كَمَا بَدَأَ غَرِيبًا ، فَطُوبَى لِلْغُرَبَاءِ
kutoka kwa Abii hurayrah: alisema Mtume : ulianza na hali ya kutokujulikana. Hivyo vivyo utarudi (ulikotoka) ukiwa na hali ya kutokujulikana. Tuba ( pepo ndio malipo) kwa watendao (mema kinyume na mazoea).
Hivyo ndivyo alivyo elezea hali ya walimwengu kuhusu ujumbe ulioletwa na Uislamu wao walimwengu.
Sasa tuashirie kiini cha nukta hii. hapo juu tumeona na kuelewa kuwa maana ya Uislam ni salaama na amani, ibada ya MSAHIKI mmoja bila kushirikishwa na yeyote, kuhesabiwa siku ya mwisho, kulinda na kuendeleza maadili na adabu baina ya walimwengu, kujikita katika maendeleo kwa ustawi wa maisha ya walimwengu ... Nk. Kwa uchache tulio kuleteeni hatika idara hii, ndio taswira halisi ya ujumbe wa dini ya Uislam kwa walimwengu.
Hata hivyo walio wengi miongoni mwa wanao jinasibisha na dini ya Uislam ndio wanao ende kinyume na ujumbe wa dini yao kwa walio mwengu, jambo linalo changia sana wasio kuwa waislam kupata mwanya wa kufanya propaganda mbaya dhidi ya Uislam na kusababisha wasio elewa katika wasio kuwa waislam, kutokuingia katika dini ya uislam.
Kuna haja kubwa sana mimi na wewe tutambue kuwa matendo ya waislam hayawakilishi kabisha ujumbe na mafunzo ya dini ya Uislam maana ... baada ya Uislam kuenea watu wameendelea kuwa huru kuchagua baina ya kujipamba na mafundisho ya Uislam au kuyawachilia mbali na kuwa miongoni mwa walio khasirika kesho kiyamani ikiwa wamefariki bila ya tauba.
hivyo sasa Uislam utaendelea kubaki kuwa ni Uislam na kuwa mbali na matendo yasiyo kubalika watakao jipapmba nayo wanao jinasibisha na dini ya Uislam.
4. Misingi ya Uislam
Uhalisia wa misingi ya dini ya Uislam umo katika kuyaingiza makusudio ya nguzo za dini na imaani katika maisha yetu ya kila leo. Sasa hapa tunazungumzia makusudio ya kila nguzo na baadhi ya mafunzo ya Uislam yaliyo kuwa hayakutajwa wazi wazi katika nguzo husika:
-
NGUZO YA KWANZA: KUSHUHUDIA KWAMBA HAPANA MUSTAHIKI WA IBADA ISIPO KUWA ALLA NA MUHAMMAD NI MTUME WAKE:
-
kusudio la kwanza ni kuazimia kuto kumuabudu yeyote awaye kinyume na ALLAH kwa kuwa ALLAH ndiye mustahiki wa ibada zote (ibada ni jambo lolote zuri analo liridhia ALLAH ... hata kula, kujamiiana na mke wa ndoa...Nk vyote ni ibada), kuabudiwa kwake ni kwa sababu yeye ndiye muumba na msimamizi wa walio umbwa na mambo yao yote.
-
kusidio la pili kuazimia kuwa Muhammad ndiye kiongozi wa kuigwa katika kila kitu maishani, asiye endewa kinyume katika mafundisho na maamrisho yake kwa sababu yeye alitumwa na Muumbwa wa haki.
-
-
NGUZO YA PILI: KUSIMAMISHA SALAH: kusudio lake ni kuwa salah ndio kitwaharishi cha roho na nafsi kama ilivyo sabuni kwa vyombo na nguo. Sasa kutokana na makosa anayo yafanya mwanadamu hapana budi kuisimamisha salah(kusali kila salah kwa wakati wake) bali hilo ndio lengo la kuumbwa mwanadamu na ibada ndio nguzo ya kipekee inayo weza kutekelezeka bila dharama yoyote zaidi ya maji, pia ni ibada inayo weza kutekelezeka hata mtu akiwa juu ya chombo cha usafiri sehemu alio kaa yeye.
-
NGUZO YA TATU NI KUTOA ZAKAA: zakaa ni aina mbili:
-
zakaa ya mali hutolewa kila mwaka wa mali milliki kwa mmoja wetu kusudio lake ni kutwaharisha na kusafisha mali za walio na mali
-
pia kutwaharisha ibada ya saum kwa wafungao maana bada ya mwanadamu huingiwa na mambo yanayo weza kuiharibu,
-
kwa wakati huo huo zakaa zote mbili tulizo zielezea hapo juu kusudio lengine katika kutoa zakaa ni kutatua matatizo ya kiuchumi kwa wanajamii na kustawisha jamii.
-
-
NGUZO YA NNE NI KUFUNGA SAUM MWEZI MZIMA WA RAMADHANI: kusudio lake kuu ni kuwafanaya watu wote kulingana mbele ya ALLAH bila kushalisha tofauti zao za kijamii na tabaka zao za kiuchumi. Yaani tariji apate kuelewa uhalisia na maisha ya kipato kidogo kilacho wapalekea baadhi ya wanajamii kuishi katika maisha ya chini ya mlo mmoja kwa siku na kuwafanya waishi maisha yao ya kila siku bila kuelewa nini watakacho kila kwa saa na nyakaati za usoni. Hapo nipo tajiri anaweza kuelewa kuwa yumo ndani ya neema kubwa sana neema ambayo inaweza kumfanya kudumu katika ibada ya ALLAH aliye mzidishia neema ya mali na kuwapunguzia baadhi ya watu ambao pengine ni wenye akili na mahodari kuliko hata tajiri husika.
-
NGUZA YA TANO NI KUHIJI NYUMBU TUKUFU ALIYO IJENGA NABII IBRAHIIM NA MWANAWE ISMAIL: hija ina aina tatu kama zifuatazo:
-
kuhiji makaa na madinah maishini kwa uchahe mara moja
-
kuhiji baitul muqadasu huko palestina, nyumba alio ijenga Nabii Sulaiman bin Daudi
-
kuhiji kwa mara ya pili na zaidhi ya hapo kwa mwenye fursa huko sio lazima kama ilivyo kuwa ya mara ya kwanza.
-
Nguzo hiza za uislam hazimpatii mmoja wetu dhamana ya kuingia peponi bali hizo ni kinga kwake ili aye chini ya himaya kamilifu ya dola ya kiislam na himaya ya waislam wenziwe wanaoishi katika nchi zisizo hukumiwa na sheria ya dini ya Uislam.
Hata hivyo ni lazima nguzo hizo kuingizwa maishani mwa kila muislam ili ithibitike imani yake kiutendaji na utekelezaji.
Sasa tuzungumzie makusudio ya nguzo za imani siti:
-
NGUZO YA KWANZA NI KUWA NA IMAANI KWA MUUMBA MMOJA MSTAHIKI WA IBADA AITWAYE ALLAH KWA LUGH YA KIARABU. Rejea pia makusudio ya nguzo ya kwanza hapo juu.
-
NGUZO YA PILI NI KUWA NA IMANI KUWA MALAIKA wapo hata kama hawaonekani kwa wanaadamu walio wengi pia wao ni viumbe wasio stahiki kuabudiwa maana na wao pia huabudu mstahiki mmoja wa ibada. Yaani hawafai kuabudiwa kabisa.
-
NGUZO YA TATU NI KUAMINI VITABU VYOTE VYA MITUME WALIO MTANGULIA MUHAMMAD: kusudio la kuamini vitabu na kuitakidi kuwa hakuna tofauti hata moja baina ya vitabu hivyo maana vyote vimelenga jumbe kuu tulizo zielezea katika kipangele cha cha ujumbe wa Uislam hapo juu.
-
NGUZO YA NNE NI KUAMINI mitume wote na wamwisho wao ni Muhamaad, bila kubagua hata kama wamekuja zama tofauti maana wote wametumwa na ALLAH ingawa, bila shaka ALLAH amewapa fadhila tofauti kwa sababu anazo zijua yeye ALLAH, sababu zisizo tuhusu kabisa. Wote ni kizazi cha damu moja itokanayo na babu mmoja ambaye ni Nabii Ibrahiim. asiye kuwa katika damu hiyo utume wake ni wauongo.
-
NGUZO YA TANO>>>
-
NGUZO YA SITA>>>
5. Kuingia na kutoka katika Uislam
6. Uislam na dunia
-
siasa
-
maendeleo
7. Uislam na waislam
-
daraja la watu kidini