top of page
web slide gsht.jpg

Utangulizi

Asalaam alaikum wa rahmatuLLAH wa barakaatuh.   
kwa siku nyingi mnoo tumeendelea kupambana na suala la changamoto ya uhitaji wa mabadiliko ndani ya jamii  katika ukanda wa Afrika ya mashariki na ya kati. Hitajio hili limetokana na hali duni ya kiuchumi kwa wanajamii kwa jumla na kwa sura ya kipekee, kwa waislamu walio wengi, hali inayo chochea mmomonyoko wa maadili kwa waislamu wa rika zote za umri katika eneo tajwa. 

Hivyo dira yetu ni kutafuta namna ya kupata kizazi kipya cha wasimamizi wa jamii kidini, kupitia kundi la waathirika wa hali tulio ielezea hapo juu. Yaani tunacho lenga kukifanya ni kuwatumia wale wanao onekana kupigwa chenga ndoto zao za maisha.  Hata hivyo hatuna nia ya kutokushirikiana na wasio kuwa waathirika wa hali tulio ielezea hapo juu. Bali tupo tayari kushirikiana na yeyote atakaye guswa na lengo letu.

    
Tovuti hii imepangiliwa kwa mtindo wa makala, kila makala ikiwa na ukusara wake maalumu. Sasa tunakujuza wewe ndugu msomaji kwamba kila picha au video utakayo iona katika tovuti hii, au kurasa zitakazo fuatia basi picha au video husika inawakilisha makala maalumu. Ili kuyapitia makala husika utalazimika KUBOFYA MAANDISHI ELEKEZI YALIOPO PEMBEZONI MWA PICHA AU VIDEO HUSIKA, kama yanavyo onekana hapo: 

​

​

 

Tutakushukuruni sana kuzingatia utangulizi huu katika ufuatiliaji wa tovuti yetu hii.

- SALHA ELIEZA MBILINYI -
bottom of page