Global Services High Targets
LEADERSHIP – ENTREPRENEURSHIP – VOLUNTEERING
BRELA ID No: 465066, TIN:
BAKWATA ID: BKT /MDRS/O2O/O1O15
0768649111 – 0675103790 – 0777496444 – 0772496444
Email: gshcourt@gmail , uddgshcourt@gmail
TANZANIA DAR es SALAAM, UBUNGO KWEMBE, MLOGANZILA
UBUNGO, KWEMBE, MLOGANZILA

TARIFA ZA BAADHI YA WATU MAARUFU DUNIANI WALIOINGIA KATIKA UISLAM
مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا
katika waumini kuna watu walio tekeleza yale walio muahidi ALLAH, badhi yao tayari wamesha timiza ahadi zao kwa ALLAH na baadhi yao wamo kusubira wakati uwadiye wakutekeleza ahadi hizo, wala hawaku badili niazao kwa mabadiliko ya hali ya maisha
JORAM VAN KLAVEREN
Joram Jaron van Klaveren (amezaliwa 23 Januari 1979) ni mwanasiasa wa Uholanzi . Akiwa mwanachama wa Chama cha Uhuru alikuwa mbunge kuanzia tarehe 17 Juni 2010 hadi Machi 21, 2014. Baadaye alikuwa huru hadi muda wake wa uongozi ulipomalizika tarehe 23 Machi 2017.
Alijikita zaidi katika masuala ya ubaguzi , uwiano wa ajira na idadi ya watu. , usawa na ukombozi . Kuanzia tarehe 24 Machi 2011 hadi 11 Juni 2014, pia alikuwa mwanachama wa Jimbo la Majimbo la Flevoland .
Alijulikana sana kwa maoni ya kupinga Uislamu. Mnamo Oktoba 2018, alisilimu na kuwa muislam na kuwa Muislamu, akiwa mbioni kuandika kitabu cha chuki dhidi ya uislam na waislamu, katikati ya kuandika kitabu kinachopinga Uislamu.
Baada ya kuwa Muislamu, aliamua kukiweka wakfu upya kitabu chake kwa utafutaji wake wa udini na kusilimu baadae. Kitabu chake kiitwacho " Apostate from Christianity to Islam in times of sécularisation and terror" kilichapishwa kwa Kiholanzi na Kiingereza.
MARYAM POUGETOUX
MARYAM POUGETOUX bint mfaransa wa asili kwa mababu na mababu kutoka familia ya wapigania uhuru nchi ya Ufaransa. Alizaliwa mwaka 1999 hapo Paris katika familia ya wakatoliki wenye imani halisi na matendo ya mafunzo ya dini yao. MARYAM ni bint aliye kulia malezi ya kiimani katika dini ya wazee wake na amekuwa ni bint aliye kuwa hakujulikana sana na watu walio wengi kutokana na makuzi yake ya kidini yaliyo mpelekea kutokujichanganya katika makundi ya vijana wa umri wake.
Mnamo Mei 20, 2020 MARYAM alichaguliwa kuwa Rais wa jumiiya ya wanafunzi wa vyuo vikuu UNEF nchini Ufaransa. Kuchaguliwa kwake kuliibua hisia za viongozi wangi wa siasa nchini huko na kuwa ni gumzo kuwa sana kwa kuwa MARYAM alikuwa tayari amesha silimu miaka kadhaa iliyo pita akiwa ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ambaye hakujizuia kuutambulisha uislam wake kwa watu wanao mzunguuka kuanzia nyumbani kwao na mtaani kwao, bali alikiwa akivaa hijabu akiwa shule ya sekondari hali ya kuwa ni marufuku kikanuni mwanafunzi wa sekondari na shule ya msingi kufaa vazi lolote linalo tambulisha hisia za imani ya dini yoyote.
Ili kuwa ni vigumu mnoo kwa viongozi waalimu wa shule kumkataza uvaaji wa hijabu maani alikuwa akivua hijab yake punde tu anapo karibia eneo la shule na mara tu akitoka eneo hilo tayari avaa hijabu yake kama alivyo jiamulia maishani mwake. Alipo jiunga na elimu ya chuo kikuu alikuwa huru kuvaa hijabu bila ya bughudha akiwa ndani na nje ya chuo.
Bint huyo kwa tabia alizo kuwa nazo miongoni mwa watu wajamii yake ... alikuwa na mazoea sana ya kushiriki bila ya kushurutishwa, katika ma suala ya kifamii kabla na baada ya kubadili dini. Jambo lililo mfanya kupenda na watu wangi miongoni mwa wanao mfahamu. Mapema akiwa na umri wa miaka 19 alichaguliwa na wanafunzi wenziwe kuwa Rais wa jumuiya ya wanafunzi nchini hapo.
Waziri wa Mambo ya Ndani na Ibada nchini humo, Gérard Collomb, alimtuhumu sana kwa madai kuwa MARYAM ni mtu anaye dhihirisha "tofauti yake katika jamii ya Ufaransa", pia waziri huyo amekuwa adhihiri katika vyombo vya habari na kumshambulia sana MARYAM POUGETOUX pia waziri huyo aliwahi toa ishara za wazi kuwa ameshangazwa sana taswiri ya Uislam kusambazwa na kuenewza tiviini (TV). Yaani alilaumu sana kwanini wandishi wa habari wakaamua kumkaribisha tiviini na kufanya naye kipindi.
Mwaka huu wa 2020 katika harakati za kupambana na gonjwa la korona, MARYAM POUGETOUX alilazimika kuhudhuria katika kikao malumu cha bunge nchini ufaransa akiwawakilisha wanafunzi wote wavio vikuu jijini Paris. Kwa mshangao mkuwa sana rais huyo wa wanafunzi MARYAM POUGETOUX aliamua kuingia bungeni akiwa kavaa hijabu kama ilivyo kawaida yake ingawa aelewa wazi kuwa vazi la hijabu limepigwa vita na kutungiwa kanuni kwa kulipuga marufuku rasmi kuvaliwa katika baadhi ya maeneo nchini humu. Kuchaguliwa kwake kulileta taharuki sana baina wa raia nchini Ufaransa mpaka viongozi wa serikali aliingilia kati kutaka kutengua uteuzi huo. Jambo lililo wapelekea wanafunzi kugoma kushiriki vipindi madarasani kwa madai wamepokonywa chaguo lao ambaye ni MARYAM POUGETOUX. MIgomo hiyo iliratibiwa na vijana wa dini mbali mbali na kusababisha maandamano mjini Paris, wakalazimika viongozi wa serikali kumuachia uongozi. Mara kwa mara huwa nachaguliwa yeye hadi mwaka huu wa 2020 yeye ndiye Rais wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini humo.
Katika juhudi za kupambana na ugonjwa wa korona serikali kuu ya Ufaransa uliandaa kongamano linalo kutanisha viongozi wa bunge na viama vyote nchini Ufaransa kwa kushirikiana na jumuiya wa wanafunzi wa vyuo vikuu, jumuiya ambayo MARYAM ndiye Rais wa wanafunzi wote, jambo lilo mlazimu MARYAM kuelekea bungeni kushiriki kongamano hilo. MARYAM POUGETOUX kama kawaida yake aliibuka bungeni akiwa kavaa hijabu yake.
Baadhi ya wabunge waliingilia kati kwa kutishia na kumtaka MARYAM kuvua hijabu yake au kumuamuri kutokuhudhuria kikao husika. " hijabu ni maamuzi yangu binafsi, kuvaa sijalazimishwa na yeyote, walaa sio ishara ya mrengo wowote wa kisiasa ", MARYAM PUGETOUX kajibu kwa kujiamini. Kwa bahati sana mwenye kiti wa kikao husika alielewa fika kuwa mualikwa wao MARYAM atachagua kuondoka na kukiwacha kikao hicho...mwenyekiti ya kikao hicho aliingilia kati kumtetea MARYAM na kusema: "ni sahihi kabisa kuwa nchi yetu ya Ufaransa imeamua kwa miaka mingi sana kuwa ni nchi ya kialmania (isio vumilia ishara za imani ya dini yoyote katika shughuli za dola). Hata hivyo suala la kikao chetu hiki cha gonjwa la korona, hakuna sheria yoyote wala muongozo wowote unaozuia mmoja wetu kuvaa vazi la ishara ya imani ya dini. Hivyo yeyote kati yenu akitaka kususia kikao hupo huru kuondoka na kuwaachia walio tayari kuendelea na kikao."
AMIR JUNAID ALMUHADITH
AMIR JUNAID MUHADITHU aliye kuwa maarufu kwa jina la LOON katika dunia ya mziki na sinema ni mwanamziki maarufu sana aliye hudumu baina ya miaka ya 1998 – 2007 . Kwa ubingwa wa vipaji alivyo kuwa navyo, alijikuta anapendwa sana na washabiki kiasi makambuni mengi walimtaka kufanya naye tenda za mziki. Mnamo mwaka 2008 alielekea Abuu dhabi kwa ajili ya maandalizi ya kudumbuiza … lakin huko huko ndiko alipo pata uongofu akasilimu. Jambo lililo washangaza watu wengi sana maana alisita mara moja siku ya mkesha wa shoo na kuacha maandalizi yote aliyo yafanya kwa ajili ya shoo (show) husika. Wala hakujali khasara ya pesa alizo kuwa amezitumia kwa ajili shoo hiyo.
Punde tu alipo silimu alibadili jina akaitwa Amir Junaid Muhadhu, alirudi kwao kuaga wazee wake na kuafanya hijza akahamia kairo nchini Misri kwa lengo la kuisoma dini kabisa. Huko kairo alishi miaka 3 baada ya kuipata elimu aliasisi kituo cha elimu ya dini kwao nchini marekani na mali zake zote akazitumia katika shughuli za kituo chake hicho cha dini. Kwa bahati Amir Junaid Muhadith Alitengenezewa kesi ya madawa ya kulevya eti tukio hilo kahusika nalo tokea mwaka 2006 yaani miaka mitatu kabla ya kusilimu. Akiwa uwanja wandege jijini Bruxelles nchini Ubeljiji, Amir Junaidi Muhadith alishikwa uwanzani na kupelekwa jela kwa kifungo cha miaka 14. Alikaa kwa miezi kadha jela huko ubeljiji halafu akahamishwa hadi kupelekwa nchini kwako kifungoni.
Huko marekani jela nyingi mno zikimtema akajikuta mara kwa mara ahamishwa jela hadi jela nakupitia jela nyingi mno miongoni mwake Butner, huko Carolina ya kaskazini, Yazoo iliyoko Mississippi, Estill iliyoko Carolina ya kusini hadi jela ya mwisho ya Coleman huko Florida. Baada ya miaka 9 jela imekuja kubainika kuwa hakuwa na hatia yoyote mnamo 29 julai 2020 Amir Junaid Muhadith ametolewa jela baada ya kutetewa na wafungwa wenziwe kwa miaka yote alio kaa jela Weldon Angelos, mmoja wa wafungwa wazamani aliye kuwa kahukumiwa miaka 55 jela, ndiye aliye kuwa aendesha kesi ya Amir Junaid Muhadith akiwa upande wa kumtetea hadi akafanikiwa hivi sasa yupo huru nchini karekani jijini kwao New York . Hata hivyo huko jela hakupachika mikono kabisa bali aliwasilimisha watu wengi katika jela zote alizo pitia laikn alikuta kituo chake cha dini alicho kiasisi kimenyumba mno. ALLAH amlipe kwa nia yake njema … tayari yupo mbioni katika kukufufua kwa mara nyengine tena pamoja na change moto nyingi alizo nazo kwa kwa sasa.
Miezi 3 tu baada ya kutoka kifungoni makala hii tunaiandika akiwa Amir Junaid Almuhadih akiwa kimia ... tunaamini kuwa kwa siku sa usoni ataongea na kutenda.
Hivyo ataye kuwa hai anaweza kushuhudia na kuyasikia mengi kutoka kwa Amir Junaad Almuhadith.
MELANIE GEORGIADES
Mfaransa Diam' s aliye badili jina lake la zamani MELANIE GEORGIDES baada ya kujulikana talanta yake ya mziki aliokuwa nayo! Diam mwanamziki aliyeweza kushinda hadhira kubwa kwa Albamu 3 tu jambo lililo kuwa halikuwahi kutokea kwa msani yeyote nchini ufaransa na ulaya nzima katika historia ya mziki. Mtindo wake ambao ukichanganya hip hop kwa ustadi na sauti yake ya kumtoa nyoka pangoni ... kumsukuma na kumvuta hadi juu kweupa, alipendwa sana miaka ya 2001 huko Ufaransa. Mnamo 2007, rapa huyo alitoa DVD yake, "Au tour de ma bubble". Mélanie Georgiades alizaliwa mnamo Julai 25, 1980 huko Nicosia, moja ya visiwa Vya dola ya Ufaransa. Mama yake ni Mfaransa, baba yake ni Msipro. Mwisho baba yake aliiacha familia yake mapema sana na Mélanie, binti wa kipekee, alilelewa na mama yake kutoka umri wa miaka minne katika vitongoji vya Paris. Akikabiliwa na utamaduni wa rap kitongojini kwao, badala ya kuitwa adui mpotasha jamii alitunukiwa cheo kuwa waziri wa vijana katika Umma wa kifaransa kwa sababu ya mziki, cheo hicho alipewa kutokana na ushawishi wake mkubwa kwa vijana na watu wazima na ubunifi alio kuwa kajaliwa na MUUMBA wake. Punde tu baada ya kupewa ofisi katika wizara ya vijana MELANIE alibadili jina lake na kuchukuwa jina la utani, DIam's lililo beba maana ya neno almasi. Mwaka 1995: Diam's akiwa na umri wa miaka 15, licha ya umri wake mdogo alikuwa tayari ni nguri wa mziki jijini Paris. Mnamo 98, alishirikiana na kikundi cha Mafia Trece. Muda mfupi baadaye, aliibuka kwenye mkusanyiko na Neg'Marrons. Wakati huo huo, Diam's akapata uzoefu thabiti na hatua ya uhodari. Mwaka 1999 tayari alitoa albamu yake ya kwanza "Premier mandate" na rapa-mtayarishaji Blacdk Mozart.
Licha ya kufeli kwa biashara, Diam's hakusita kuendelea na mikutano na meneja wake, Choukri. Akishiriki katika miradi mingi ya nyanza za mziki. Mnamo Mei 2003, Diam's hatimaye alitoa albamu yake ya pili "Brut de femme". Mwaka 2003, mwaka 2004 alibuni matamasha mengi ikiwemo tamasha la "Victoire de la Musique "tamasha la aina yake. Mwisho wa mwaka huo huo, alitoa DVD yake ya kwanza. Februari 2006: Albamu mpya iliyo subiriwa kwa hamu sana na mashabiki wake. Katika mwaka mmoja, sio chini ya 6 zilizopigwa ("La boulette", "Jeune demoiselle", "Big up", "Confession nocturne", "For love", "My France to me") alitangazwa kuwa msanii wa mwaka katika bara la ulaya. Huko Cannes alitwaa cheo cha Msanii wa Kike, Albamu na Wimbo wa Mwaka wa Ufaransa.
Mnamo 2007, Diam alitoa DVD mpya, iliyoitwa "Au tour de ma bubble" na akarudi mwaka uliofuata na rekodi iitwayo "Black Session", ikiwa na nyimbo za duet na Sinik, L'Skadrille, Philo na Koma. Njia nzuri ya kujifunza zaidi juu ya msanii huyu kama hakuna mwingine .. Mnamo Novemba 2009, Diam's alitoa albamu nyengine mpya "SOS". Singo ya kwanza inaitwa "Watoto wa Jangwani". Baada ya hapo Diam's alisilimu na kuvaa hijabu kama anavyo onekana katika video hapo juu. Hapo ndipo yalipo anza madhila ya kukashifiwa na kutukanwa na walio kuwa hawakufurahishwa na kitendo chake cha kusilimu. Bahati walio kuwa washabiki wake na walio mtunza na kumpa vyeo keme keme, wengi wao wali mgeuka na mkupaka sifa mbaya mbaya uzijuazo duniani hapa, mpaka walio wengi walidhani kawa kichaa kuvaa hijabu wakilinganisha na mambo aliyo yafanya hapo awali kabla ya kusilimu.
Mnamo 2012 takiriban baada ya miaka 3 ya matusi na kashfa dhidi yake , sasa ikiwa sote tunaelewa kuwa Melanie alijitwalia umaarufu kupitia uandishi wa mashairi na mziki wa hip hop basi sio ajabu pia kuamua kwake kuvunja ukimia na kuchapiasha kitabu chake "AUTOBIOGRAPHIE " akielezea maisha yake ya kabla na baada ya kusilimu, halafu miaka 3 baadaye yaani 2015 MELANIE GEORGIADES aliibuka na kitabu kipya alicho kiita "MELANIE, FRANCAISE ET MUSULMANE" yaani "Melenie, mfaransa na muislamu ".
Ikumbukwe kuwa melanie alipitia faani ya uandishi wa vitabu na mashairii kabla ya kuibuka mwana hip hop nchini kwao. Hivyo ana weledi wa hali ya juu mnoo katika kuyapanga na kuyapambo maneno, kila toleo la kitabu chake huchapishwa kwa mamilioni ya nakala za vitabu na zote huisha kwa wiki kadhaa baada ya chapicho.
Wakiwa walimwengu wajiuliza: "JEE, MELANIE ATAIBUKA NA KITABU KINGINE BAADA YA VIWILI ALIVYO VIANDIKA BAADA YA KUSILIMU ?"
Mapema juzi kati Julai 19, 2020 Melanie kesha post zinga la maneno huko katika akaunti yake katika mitandao ya kijamii kama anavyo someka: " WATU WENGI WAMEKUWA WANIULIZA IWAPO KUNA MPANGO WA KUTOA KITABU CHA TATU ... KIUHALISIA NDIO, NITATOA KITABU INGAWA MARA HII KITAHUSU MAISHA YANGU YA MAMA WA NYUMBANI NA WANANGU WENGINE. NAKIRI KUWA MUDA UMENIBANA MNOO. SASA IKIWA BADO KITABU HAKIJA DHIHIRI KWENYE NYARAKA TAMBUENI KUWA TAYARI TASWIRA YA KITABU HUSIKA NINAYO KICHWANI. SIKU YAJA KITABU HICHO KITAKUWA MIKONONI KWENU NA VITABU VINGINEVYO IN SHAA ALLAH", aliandika Melanie Georgiades.
Leo hii Melanie georgiades ana mradi wa kusafirisha mahujaji kutoka bara la Ulaya kwenda kuhiji Makkah ingawa ugonjwa wa korona umepelekea Melanie kusitisha shughuli za mahujaji kwa muda hadi siku za usoni.
VINCE FOCARELLI
Abdus Salaam Vince Forecarolli ni raia mzaliwa wa nchini Italia aliye julikana sana na vyombo vya usalaama vya nchi nyingi duniani. Adus Salaam alikuwa akiitwa Vince Forecarolli, hapo awali kabla ya kubadili dini. Vince alikuwa ni jambazi mkubwa sana na muuza madawa ya kulevia duniani. Kutokana na shughuli zake hizo Vince alikuwa ni mtu hatari sana, muuaji wa watu hasa wale alio kuwa awadhani kuwa ni changamoto kwa shughuli zake haramia.
Vince alikuwa ni mmoja wa watu 5 wahalifu wanao tafutwa duniani, kutokana na hali hiyo Vince ali jiandalia kuwa na walinzi ambao walikuwa kama jeshi kamili. Polisi na majeshi italia na ulaya nzima walikuwa wakimsaka sana na yeye pia alikuwa awasaka wa kuu wa polisi na wa kuu wa jeshi. Kati yao baina ya Vince na vikosi vya jeshi, aliye kuwa amuwahi mwenziwe basi alikuwa amuua.
Hivyo polisi, jeshi na watu wengi walio kuwa ni kizuizi cha shughuli za Vince wameuliwa sana kwa mamia katika nchi nyingi za ulaya. Vince mwenyewe amewahi kuzingirwa na vikosi vya jeshi na polisi mara sita katika maeneo tofauti barani Ulaya, wakiwa wanajeshi na imani kuwa wamemuua Vince lakin baada ya kuvukua vifusi vya shambulizi la mabumo yanayo tumiwa katika mashambulizi huwa
Vince haonekani kabisa halafu siku chache wamsikia kutorokea nchi nyengine na kufanya matukio mengine ya ujambazi huko. Katika moja ya mashambulizi aliyo kuwa akifanyiwa na majeshi, mwanawe Vince, jambazi kama yeye aliuliwa vibaya mnoo lakin Vince alinusurika yeye . Vince Forecarolii alibadili dini na kuwa muislam hivi sasa anaishi nchini Australia akimuuguza mama yake mzazi anaye umwa na ugonjwa wa cancer ya daraja la nne. Vince hivi sasa aitwa Abdus Salaam ni raia mwema na mjasiriamali kama anavyo onekana katika video hapo juu.