top of page

MAISHA - MAPATO NA MATUMIZI

Updated: Jan 18, 2023

HAPA TUTAKUWA NA MAKALA ZINAZO HUSU MISINGI YA CHUMO NA MATUMIZI MALI KWA MUJIBU WA DIRA YA UISLAM TU...HATA HIVYO HUENDA BAADHI YA MENGINE YAKAKUTANA NA MIFUMO YA WASIO KUWA WAISLAMU. IKITOKEA HALI HII BASI TAMBUENI KUWA YATAKUWA YA MEFANANA TU WALA SI VYENGINEVYO.




Tatizo la kiuchumi kuweko duniani lipo, wala halibahui rangi ya mtu wala eneo anakoishi yeye, wala tabaka la kijamii alilo nalo mhusika. Hiyo ni hoja isiyo pingika kabisa, hata hivyo uhalisia wa sababu za tatizo la kiuchumi kwetu, ni sisi wenyewe tunao changia kwa asilimia kubwa sana. Njia ni mingi za kuupunguza ukali wa tatizo la kiuchumi katika jamii zetu ... tulicho kosewa ni utashi, kujituma na uthubutu. mambo matatu hayo yamo ndani mwetu wenyewe kilicho baki ni maamuzi tu.


“ KIMA CHA HAIBA NA HISHMA HALISI YA MTU ( JAMII FULANI ) DUNIANI, HUFUNGAMANA NA KIMA CHA UWEZO WAKE ( WAO ) WA KUJITEGEMEA KIMAPATE ... KUNA HAJA YA FUZIFICHA AIBU ZETU ZA KIMAPATO JAMBO LIKAKALO PELEKEA TUJITUME ILI TUSIADHIRIKE AU KUKUBALI KURIDHIKA NA KIDOGO TUNACHO KIMILIKI.”

Ufakiri na utajiri ni mamb; mawili yanayo shughulishwa walimwengu sana kuliko jambo lengine lolote, kiasi cha kuzifanya juhudi zao zote zisiwe nje ya hayo mawili. Yaani ima mmoja wetu humo mbioni kuukimbia ufukara au yumo mbioni kuhakikisha alicho nacho kisipungue ikiwa sio kumtoka kabisa. Tunalo liashiria hapa ni jambo liitwalo " TATIZO LA KIUCHUMI " . Maana nyengine ya tatizo la ni kuchumi ni hali inayo dhihiri kwa mmoja wetu kutokuwa na uwezo wa kukimu hitaji lake kwa wakati husika hata kama uwezo huo ataupata baada ya masaa kadhaa au ni hali ya mmoja wetu kushindwa kulikimu hitaji lake kwa kiwango kilicho tarajiwa.

Mfano unapo kuwa na hitaji la kuipata mikate minane ukaambulia mikate aba na nusu tayari huzingatiwa kuwa ni tatizo la kiuchumi. Uhalisia wa tatizo la kiuchumi ndio kupelekea watu walio wengu kuuza utuwao au kutukiwa katika mambo ambayo kwamba wasinge kuwa tayari kuyafanya lao wasinge jihisi kuwa na utajio la kukimo tatizo ya hitajio lao fulani.

Tatizo la kiuchumi hujengwa katika misingi miwili mikuu:

  • mahitaji ya mwanadamu,

  • njia za mapato ya mwanadamu

Hayo mambo mawili tuliyo yataja hapo juu ndio yanayo jengwa juu yake nadharia la tatizo la kiuchumi.


Mahitaji ya mwanadamu ni jambo lisilo epukika kulikimu ingawa pia sio kila hijati ndio inatulazimu tulikimu. Mamba mengine la kutambua kuhusu mahitaji ya mwanadamu:

  • mahitaji huwa endelevu bila kukata,

  • mahitaji huongezeka idadi kila siku zikienda mble kiumri,

  • mahitaji ni mengi sana kuliko idadi ya vyanzo vya mapato,

  • mahitaji huzalisha mahitaji mengine yaliyo kuwa hayakutegemewa kwa wakati husika,

  • mahitaji yanaweza kusamehewa kwa lengo la kukimu majitaji muhimu kuliko yalio samehewa.

Baada ya kugusia sifa za mahitaji kama tulivyo zielezea hapo juu, tunaamini kuwa msomaji wa makala haya anaweza kuzitumia sifa hizo katika maamuzi yake ya kukukimi mahitaji yake.


Nyezo zinazo tumika katika kujiongezea kipato ili kuyakimu mahitaji ya maishi ni kila kitu na njia tunazo zitegemea kutumia katika shughuli zetu za kimapato.

Mfano:

  • kalamu, njia za upataji wa taarifa, karatasi, afya ya kiwiliwili ... ni katika ya nyenzo ayazo zihitaji mwandishi yeyote wa habari.

  • fedha, dhahabu...ni katika nyenzo anazo zihitaji fundi sonara.

Sasa kuna haja kubwa yakuzijua pia sifa za nyenzo:

  • nyezohuwa zinazo tegemewa kuyakimu hajitaji ni chache tukizingatia idadi ya mahitaji inazo ongezeka kila leo,

  • sio kila nyenzo ndio inayo kubalika katika kuyakimu mahitaji yetu ( uuzaji wa madawa ya kulevya)

  • nyenzo huwa hazipatikani (milikiwi) kirahisi ila mpaka zigharimiwe kwa mali tasili au kuzitolea jasho.


BAADHI YA MAKUNDI YA KIJAMII YANAYO DHIHIRI WAZI KWAO " TATIZO LA KIUCHUMI ".


A. KINAMAMA.

kwa mfumo wa dini ya uislam kila mmoja wetu anayo haki dini ya uislam kila mmoja wetu mwanaume au mwanamke anayo haki ya kumiliki mali, ingwa haki hiyo imo katika mipaka aliyo iweka ALLAH. Mbali na suala la haki iliyo elezewa hapo juu, ni kwamba kinamama wamekuwa ni moja ya kundi la wahanga katika jamii zote duniani maana sababu zao wao kumiliki mali zimekuwa na mizengwe wanayo ichangia kinamama wenyewe kwa upande mmoja, na kwa upande mwengine mizengwe hiyo huchangiwa na mufumo ya kijamii wanako ishi kinamama hao.

Kuna haja kubwa sana juhudi zikafanyika za kuwakomboa kinamama kwa kuwashirikisha kikamilifu katika wao kujitambua wao ni kina nani na nini wajibu wao kwa aliye waumba. Halafu ndio ishirikishwe jamii nzima katika kumuwezesha mwanamama ili awe ni mmoja wa walio miliki mali.


B. WALEMAVU.

Akitoa ujumbe maalumu siku moja Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ulemavu kwa kiasi kikubwa unahusishwa na umasikini, kwani watu wenye ulemavu ni asilimia 20 ya watu masikini wanaoishi kwenye nchi zinazoendelea.

Katika ujumbe wake siku hiyo, Ban alipongeza msimamo na juhudi zinazoonyeshwa na watu wenye ulemavu na alitoa wito kwa serikali zote duniani kujitahidi kuwasaidia zaidi watu wenye ulemavu.

"Tutambue kwamba vita dhidi ya umasikini , maradhi na ubaguzi hatutovishinda kama hakutokuwa na sheria, sera na mipango ya kuwawezesha walemavu ", - Ban ki-moon.


Mwito huo wa katibu mkuu wa zamani wa umajo wa mataifa, ni mwito wakuigwa na kuenziwa maana wanaoishi na ulemavu wa kuzaliwa, sio changuo lao. Wala wasio ishi na ulemavu hawakushauriwa na muumba wao ili wapate kuchagua hali ipi baina ya hali ya ulemavu na hali ya viungo kamili, lipi walipandalo. Ama wanaoishi na ulemavu walio upata baada ya kuzaliwa, kati yao ni wachache sana walio changia hali hiyo kuwapata. Hata hivyo kila kundi kati yao ni sehemu ya jamii wanakoishi. Hivyo hakuna sababu ya wao kubaguliwa wala kuwanyanyapaa. Wanazo haki za msingi kama watu wengine. duniani. Jamii nyingi duniani zimekuwa zawanyima haki zao za msingi:

  • elimu,

  • ndoa,

  • kupata kizazi,

  • fursa za kumiliki mali ... Nk.

kila mmoja baina yetu ni mlemavu mtarajiwa maana waswahili hisema hujafa huja umbika, Tuungane katika kupeana elimu ya kijamii kuhusu suala zima la walemavu na kuwapa haki zao watu wanaoishi na ulemavu maana tunaweza pia kuwatumia katika ustawi wa jamii tunakoishi. wengi wa walemavu wanavyo vipawa tu ila fursa za kuvikuza vipawa hivyo ziliwapita kwa sababu tulizo zichangia wenyewe wanajamii au sababu zilizo nje ya uwezo wetu ikiwa sio katia kuujenga uchumi wa jamii zetu,

C. WAHUDUMU WA SHUGHULI ZA KIDINI.


JEE, USOMI WA DINI NDIO SABABU YA MSINGI YA KUTO KUJISHUGHULISHA NA TENDA ZA UZALISHAJI ?

Zama tulizo nazo ... hishma ya mmoja wetu imefungamanishwa na alicho kimiliki wala sio maarifa maarifa aliyo nayo. ndio sababu kuu inayo wafanya wasomi wa dini kusahaulika ila tu linapo tokea moja ya mambo ya fuatayo:

  • wanandoa kuhasimiana

  • mtoto kumuasi mzazi

  • mazishi na shughuli zinazo fungamana na mashizi


Video iliyoko kuliani hapo ni moja ya video fupi fupi zinazo andaliwa na Mahasini TV. Mahasini TV imekuwa ya andaa video fupi fupi zinazotokana na mawaidha wanazo zitoa masheikh kadhaa kwa lugha ya kiswahili ndani na nje ya Tanzania.

Mzungumzaji, Sheikh Mussa Rusaganya katika video hii kuliani hapa, amejaribu kutoa taswira ya maisha ya maimam, masheikh na maustadh nchini Tanzania. Kiukweli sio kwamba video hiyo hahusu wasomi wa dini nchini Tanzania tu bali ni taswira ya afrika mashariki na viunga vyake ( nchi za kaziwa makuu). Punde tu ukimaliza kuisikiliza video hiyo unaweza kuelewa mustakbali wa dini afrika ya mashariki si kuambii nchi za maziwa makuu.


Sasa suali kuu la kujiuliza: " JEE, USOMI WA DINI NDIO SABABU YA MSINGI YA KUTO KUJISHUGHULISHA NA TENDA ZA UZALISHAJI ? "

Tuki tafakari sana huenda tukapata uhalisia wa ukweli kuhusu sababu zinazo pelekea hali ya wasomi wa dini kuwa kama alivyo tuchorea taswira Sheikh Mussa Rusaganya.


Baada ya kubainisha tatizo la kiuchumi na kutoa baadhi ya mifano kadha ya makundi yanayo dhihiri tatizo la kiuchumi maishani kwao sasa imefika wakati wa kubainisha misingi ya kukimu mahitaji yetu kupitia mafundisho ya uislam ikiwa uislam umetoa pia moja ya mifumo ya kiuchumi duniani. Bali kwa siku za hivi karibuni hata wasio kuwa waislam wameanza kuvutiwa sana na mfumo wa kiislam katika miamala ya kipesa. jambo linalo pelekea bangi kadhaa duniani kuwa na dirisha la miamala ya kipesa ingawa bangi hizo sio milki ya waislam wala hajiendeshi shughuli zake katika nchi za kiislam.

Hata hivyo hapa hatugusii suala la miamala ya kipesa bali uchumi kwa muongozo wa dini ya kiislamu.




D. WAALIMU

Elimu ndio msingi wa kipekee wa maendeleo katika jamii zote duniani. hakuna anaye sahau nadharia hiyo maishani, lakini kwa masikitiko makubwa sana walimu ndio wanao ongoza kwa umaskini popote walipo.

Hakuna mwana mageuzi yeyote duniani ila kapitia sehemu na kusomeshwa haijalishi kasoma katika vituo rasmi vya elimu au kapitia elimu isio rasmi almuradi kuna sehemu kapitia na kuandaliwa na mtu au kundi la watu. huyo/hao wanao andaa watu wengine ndio tunao wakusudia hapa na kuwaita walimi.

Kwa bahati mbaya hata mwalimu mwenyewe anapo hama tasnia ya ualimu na kwenda tasnia nyengineo basi sio ajabu akawasahau walimu wenziwe. Afrika tumewahi kupata marais kadha walio wahi kuwa walimu tena kwa miaka mingi tu, walipo ingia ikulu hawakuboresha Maisha ya mwalimu. Hayati magufuli mwenyewe aliwahi kuwa mwalimu kwa kipindi fulani kabla ya kuwa rais wa Tanzania. Katika muhula wake wa kwanza wote hadi kumali, walimu walibaki na hali yao walio wakuta nayo. Hata hivyo sina uhakika lipi alilo kuwa kalianda kuhusu walimu kabla ya kumaliza fursa za utawala wake.


E. WAKAAZI WA VIJIJINI



MISINGI YA UCHUMI KWA DIRA YA UISLAM.


Utangulizi.

Uislam ni mfumo kamili wa maisha kama ilivyo kuwa mifumo mingineo duniani. Yaani mtu yryote anaye dhani kuwa uislam ni dini tu … ikawa ufahamu wake umekomea hapo basi atakuwa bado haja uelewa uhalisia wa Uislam kabisa. Tunakiri kuwa uislam ni dini yaanai njia maalum ya kumtafuta muumba wetu. Lakin uislam, pamoja na kuwa dini, sio dini kama dini nyenginezo zinazo ishia tu katika masuala ya Imani na kupuuzia masuala mengineyo mfano utawala, afya, missing ya jamii Nk. Hivyo Makala haya yatamurika masuala ya kiuchumu kwa dira ya mafundisho ya Uislam.


Maana ya uchumi.


Uchumi ni masuala yote yanayo husu shughuli za mwanadama katika mbio ya kukimu mahitaji yako na njia anazo zitumia katika jaribio la kuupunguza umaskini na kuboresha kipato chake, kwa ngazi ya dola (nchi) au ngazi ya mtu moja moja… kukimu mahitaji yake na njia za kumiliki mali.

Suala la uschumi kwa kujibu wa dira ya uislam limekuwa halikutambulika uwepo wake na kufahamika na jamii zilizo nyingi duniani. Hali hii ya kuto kufahamika imetokana na moja ya sababu zifuatazo:

  • Wasomi wa masuala ya uchumi wasio kuwa waislamu kujisahaulisha kimakusudi kuweko mfumo wa uchumi usio kuwa mfumo unao tumika katika jamii zako,

  • Wasomi wa masuala ya uchumi wasio kuwa waislamu kutokuwa na maarifa halisi kuhusu uchumi wa kiuslam,

  • Wasomi waislamu wa masuala ya kiuchumi kuwa mbali na misingi halisi ya dini ya Uislam katika jumla la mafundisho yake na ujumbe wake kwa walimwengu jambo linalo wapeleke kutumia mifumo ya kiuchumi inayo kwenda kinyume na maamrisho ya ALLAH hukuzo utatuzi wa kukimu mahitaji ya walimwengu na njia za kumiliki mali,

  • Wasomi waislam, walio soma misingi halisi ya Uislam na kuufahamu ujumbe wake kwa walimwengu, kuto kusimamia majukumu yao vilivyo na kupuuza masuala ya tafiti zinazo husu utatuzi kinadharia na kimatendo, wa ufukara wa raia wa katika nchi zao na njia za kumiliki mali raia hao.

Makala haya yalengu kubainisha uhalisia wa uwepo misingi ya elimu ya uchumi katika mafundinsho ya uislam. Misingi iliyo jengwa kwenye itikadi za mamfiro ya ALLAH kwa walimwengu. Misingi ilio kinyume kabisha na misingi ya mifumo za kiuchumi zisizo kuwa hizo za Uislam.

Hivyo misingi hiyo ya uislam katika masuala ya kiuchumi ndio inayo zingatia kuwa miongozo ya waislam katika juhudi zao za kujikimu kimaisha pia kutumika katika njia zao za kumiliki mali.

Sasa hapana budi mambo kadhaa ya zingatuwe katika ufuatiliaji wa Makala haya:

  • · Uislam haukutosheka na masuala ya Imani na ibada tu kama zilivyo dini nyenginezo, katika ujumbe wake kwa walimwengu. Bali uislm ni mufumo kamili ya maisha ya mwanadamu. Iwe je, ujumbe wake uishie tu katika suala la ibada ya kupuuzia masuala mengineo katika maisha ya walimwengu ! Aaya kadhaa na hadith za mtume zinashuhudia hoja hii:

  • ” وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَانًا لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَى لِلْمُسْلِمِينَ ” النحل 89 ,

Na tumekuteremshia kibabu (quaan) ili kiwe ni ubainifu wa kila jambo, na uongofu, na rahma, na bishara kwa waislam.

  • ” مَّا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِن شَيْءٍ ” الأنعام 38 ,

Wala hatukubakisha lolote (bila kulitolea muongozo) katika kitabu (quraan).


  • ” فَلاَ وَرَبِّكَ لاَ يُؤْمِنُونَ حَتَّىَ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لاَ يَجِدُواْ فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُواْ تَسْلِيمًا ” النساء 65

Kwa mola wako (ewee Muhammad, wafiwasi wako) hawato amini (Imani kamili) mpaka wakufanya kuwa ndiwe unaye wa hukumu (katika kila walifanyalo) wanalo zozana baina yao (kama ikitokea). Halafu wasipate katika nafsi zao kinyongo kwa yale uliyo yahukumu. Wakubali hukumu bila kuhoji lolote.


Aaya za quraani tulizo ziweka hapo juu ni ushahidi tosha kuwa dini ya Uislam ilikuna ujumbe mkuu mmoja wa kujakubadili mifumo ya maisha ya walimwengu katika kila kitu popote wanakoishi wao.

Madamu hapa tumo katika makala ya uchumi, sasa hatuna budi ila tuzilete aaya zinzzo husu miamala ya shughuli za kujiengezea kipato.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ إِذَا تَدَايَنتُم بِدَيْنٍ إِلَى أَجَلٍ مُّسَمًّى فَاكْتُبُوهُ وَلْيَكْتُب بَّيْنَكُمْ كَاتِبٌ بِالْعَدْلِ وَلاَ يَأْبَ كَاتِبٌ أَنْ يَكْتُبَ كَمَا عَلَّمَهُ اللَّهُ فَلْيَكْتُبْ وَلْيُمْلِلِ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ وَلْيَتَّقِ اللَّهَ رَبَّهُ وَلاَ يَبْخَسْ مِنْهُ شَيْئًا فَإِن كَانَ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ سَفِيهًا أَوْ ضَعِيفًا أَوْ لاَ يَسْتَطِيعُ أَن يُمِلَّ هُوَ فَلْيُمْلِلْ وَلِيُّهُ بِالْعَدْلِ وَاسْتَشْهِدُواْ شَهِيدَيْنِ مِن رِّجَالِكُمْ فَإِن لَّمْ يَكُونَا رَجُلَيْنِ فَرَجُلٌ وَامْرَأَتَانِ مِمَّن تَرْضَوْنَ مِنَ الشُّهَدَاء أَن تَضِلَّ إِحْدَاهُمَا فَتُذَكِّرَ إِحْدَاهُمَا الأُخْرَى وَلاَ يَأْبَ الشُّهَدَاء إِذَا مَا دُعُواْ وَلاَ تَسْأَمُوْا أَن تَكْتُبُوهُ صَغِيرًا أَو كَبِيرًا إِلَى أَجَلِهِ ذَلِكُمْ أَقْسَطُ عِندَ اللَّهِ وَأَقْوَمُ لِلشَّهَادَةِ وَأَدْنَى أَلاَّ تَرْتَابُواْ إِلاَّ أَن تَكُونَ تِجَارَةً حَاضِرَةً تُدِيرُونَهَا بَيْنَكُمْ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَلاَّ تَكْتُبُوهَا وَأَشْهِدُواْ إِذَا تَبَايَعْتُمْ وَلاَ يُضَارَّ كَاتِبٌ وَلاَ شَهِيدٌ وَإِن تَفْعَلُواْ فَإِنَّهُ فُسُوقٌ بِكُمْ وَاتَّقُواْ اللَّهَ وَيُعَلِّمُكُمُ اللَّهُ وَاللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ” البقرة 282 .

Enyi mlio amini mnapo daiana baina yetu, deni litakalo chukuwa muda kulipwa basi andikini kwa maandishi. Basi na aandike baina yenu mwandishi muadilifu ( kwa uadilifu). Wala asikatae mwandishi kuandika kama alivyo funzwa (kufanya uadilifi) na ALLAH. Na aandike halafu anaye daiwa ndiye atamke kinacho takiwa kuandikwa na muogope ALLAH wala asidhulumu chochote katika haki ya anaye dai. Iwapo anaye daiwa ni mpungufu (kasoro) wa kufahamu au ana udhaifu wowote ( kuhusu mikataba ) au hawezi kutamka la kuandika, basi atamke yeyote katika watu wake badala yake, kwa uadilifu na muwaweke mashahidi wawili wanaume kati ya jamaa zenu iwapo hakuna wanaume basi washuhudia wanawake wawili na mwanaume mmoja kati ya munao waridhia katika mashahidi. Endapo mwanamke mmoja atasahau basi akaweza kumkumbusha mwanamke mwenziwe. Wala wasikatae mashahidi kutapo ombwa kushuhudia, wala msione uvivu (ajizi) kuandika dogo wala kubwa na kuainisha wakata wa ahadi ya kulipa. Kufanya hivyo ni uadilifu mbele ya ALLAH pia ni njia nzuri na salama ya ushahidi na mtakuwa mbali na majuto isipo kuwa tu ikiwa ni biashara ( nipe ni kupe) munaiendesha baina yenu. Sio tatizo kwenu kutokuandika. Wekeni pia mashahidi mnapo uziana wala msimdhuri mwandishi wala shahidi yeyote. Endapo mkifanya basi huo ni ufisadi kwenu na muogopeni ALLAH na ALLAH atakufuzeni na ALLAH ni mjuzi wa kila kitu.


Kupitia aaya hilizopo hapo juu ni wazi kuwa wasomi waislam wamekuwa wao ndio sababu inayo peleke mfumo wa uislam kiuchumi usitambulike na walimwengu, pamoja na kwamba uislam umeweka bayana misingi hiyo katika mafundiho yake kupitia quraan na sunnah za mtume, mambo wawili haya yanayo weka nidhamu ya maisha ya waislamu kuwa chini ya misingi ya muongozo wa ALLAH katika kila walifanyalo ikiwemo masuala ya kujikimu kimaisha na juhudi zao za kumiliki mali.

Hivyo sabubu kuu za hali hiyo zitakuwa kama zivuatavyo:

  • · Uzezo mdogo wa wasomi waislamu walio somea uchumi kufanya tafiti katika quraani na sunnah kuhusu masuala ya kujikimu na harakati kumiliki mali zilizomo katika mafunzo ya uislam au,

  • · Wameshindwa kusimamia wajibu wao wa kitaaluma katika utawalisha uislam ndani ya nyoyo za waislamu walio kuwa hawakusoma elimu ya uchumi ili wapate kuelewa kuwa dini yao haikuwacha lolote linalo husu maisha ya hapo duniani.


Kwa hali hii kasoro ni zetu sisi waislam tulio soma masuala mbali mbali yanayo husu maisha ya walimwengu, wala sio kuwa quraan ndio yenye kasoro kuwaomba waislamu kuachana na mifumo mingine ya maisha na hali yakuwa haikuleta mfumo mbadala.

Quraan ina kila kitu ndani yake kinacho husu maisha ya mwanadamu. Hivyo tatizo ni la walio somea elimu ya uchumi, kuto kuwa kwao na uwezo wa taaluma ya uislamu ili wawe na uwezo wakufanya tafiti za kiuchumi kwa lengo la kutatua lasuala ya kiuchumi kupitia quraan na sunnah na badala yake wakimbilia mifumo isiyo kuwa wa uislam katika kufanya kwao tafiti hizo. Jambo linalo pelekea wasomi wa elimu ya uchumi waiso kuwa waislamu, kuto kutambua au kukubali kuwa uislamu hauku puuza masuala ya uchumi katika mafundisho yake. Ni kweli kabisa kuwa ni vigumu sana wasomi waislamu kuwa na uwezo wa kuitumia dini katika masuala ya maisha na mazingira maana waislamu tumekuwa mbali sana na uhalisia wa ujumbe wa uislamu kwa walimwengu, maana waislamu walio wengi wamegawanyika kielimu makundi mawili:

  • · Walio soma dini tu na kuwa waatupu pepepe katika masuala ya maisha na mazingira,

  • · Walio soma masuala ya mazingira na kuwa watupu pepepe katika masuala ya dini yao ile hali uislamu umeyabeba yote.

Katika kuifanyia elimu ya uchumi ao masuala mengine ya maisha kupitia mafunzo ya dini kuna shia mbili kuu:

  • Kuifuatilia misingi ya elimu ya uchumi au ya masuala mengine ya maisha, katika quraan na sunnah. Hapo tayari panakuwa na mashiko, maana litapo tokea tatizo lolote la kiuchumi au la maisha ni kuzichukua aaya na hadith husika katika kulitatua tatizo husika,

  • ·Ninapo tokea tatizo la kiuchumi au jengine lolote, ni kutafuta uuiano baina yake na aaya za quraan na sunnah. Inapo tokea kukosa kuuiana basi hapo zitatumiwa juhudi za kitaaluma kidini kwa mujibu wa makusudio ya ujumbe wa Uislamu kwa walimwengu. Juhudi hizo zitakuwa katika yafuatayo ( Qiyaasi, Istihsaan, Maswalih mursalah, Urfu )

Kumbe sasa misingi ya waislamu katika kujikimu kimaisha na harakati zao za kumiliki mali, misingi hiyo huchukuliwa kuhumu za quraan na sunnah pamoja na miongozo ya makusudio ya ujumbe wa dini kwa walimwengu, aaya na hadithi zinazo husu masuala ya kujikimu na kumiliki mali.

Kwa bahati hukumu za uislam zina makundi mawili makuu:

  • Kundi la hukumu thabiti zisizo badilika kwa kubadilika zama wala maeneo wala kubadilika mirengo ya wasomi wa dini. Hukumu hizo zitabaki hadi kiyaama bila kubadilika hata kama walimwengu wata kubaliana kuenda kinyume nazo. Hukumu zenyewe zimo katika aaya za wazi na bayana ya maana (aaya za mirathi…) na sunnah hadithi za wazi na bayana ya maana na Ijmaa. ” وَأَحَلَّ اللَّهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبا ” البقرة 275 “ Na ALLAH amehalalisha kuuza na kununua na ameharamisha riba ”, ” لِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الأنْثَيَيْنِ ” النساء 11 “ Fungu la mwanauke ni sawa na fungu la wanawake wawili (katika mirathi)”, ” وَيْلٌ لِّلْمُطَفِّفِينَ الَّذِينَ إِذَا اكْتَالُواْ عَلَى النَّاسِ يَسْتَوْفُونَ وَإِذَا كَالُوهُمْ أَو وَّزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ ” المطففين 1- 3 adhabu kali kwa wanao punja, ambao wanapo nunua kwa watu huomba kupimiwa sawasawa, na wanapo uzia watu wao huwapuna kisawasawa , ” ألا إن الله حرم عليكم دماءكم وأموالكم ” hakika ALLAH ameharamisha kumwaga damu baina yenu na ameharamisha baadhi yenu kupokonya mali za wengine , Hukumu za kutolea mifano ni nyingi sana tu katika mlango huu … tutosheke na hizo chache. Hizo ni hukumu katika hukumu zisizo balilika hadi kiyamani, yeyote anaye ende kinyume nazo anajidanganya tu maana hatoepuka hatia huko kiyamaani .

  • kundi la hukumu zinazo badilika ni zile aaya au hadith ambazo zinaweza kuwa na maana Zaidi ya moja. Hukumu hubadilika kwa mujibu wa makusudio ya ujumbe wa waislam kwa walimwengu, wala sio kwa mujibu wa utashi wa sheikh Fulani au kikundi Fulani cha masheikh.


Mifumo ya kiuchumi duniani


kadri siku zinavyo zidi kuemba mbele wanadamu wamekuwa wakabiliana na mabadiliko kutokana na changamoto mbali mbali zinazo jitokeza maishani mwao. Hali hii imewapelekea wanadamu kubuni mifuno mbali mbali wakiwa na lengo la kutafuto kuyakimu maisha yao au pi wakiwa mbioni katika juhudi zao za kumiliki.

Kuna mifumo tofauti ya kiuchumi wanayo itumia wanadamu, bila shaka mifumo hiyo imetofautiana kutokana na mambo fulani wanayo jipamba nayo watu husika kwa mujibu wa jamii zao. mambo yenyewe ni kama ya fuatayo:

  • jeograjia za maeneo wanakoishi wao,

  • mifumo ya kijamii inayo endesha jamii zao,

  • imani na itikadi za watu husika ... Nk .

Hivyo ni lazima mmoja wetu kuelewa kuwa juhudi za kumiliki mali huwa zina athari ya mambo matatu tuliyo yaweka hapo juu au zaidi ya hayo na ndio sababu kuu inayo pelekea mifumo ya kiuchumi kiwa tafauti baina ya walimwengu. Isisahaulike kuwa nidhamu ya kiuchumi hulenga:

  • kuwanufaisha watu wa jamii husika pia (kukimi mahitaji yao),

  • kuwaondolea shari za udumu wa maisha (kuwamilikisha nyezo)

Hayo mawili hapo juu ndio kazi kuu ya mfumo wa kiuchumi kwa raia wake. Sasa kama tulivyo elezea hapo juu kuhusu mambo yanayo pelekea mifumo ya kiuchumi kutofautiana( ( jeograjia za maeneo wanakoishi wao, mifumo ya kijamii inayo endesha jamii zao, imani na itikadi za watu husika ... Nk ),

Vivyo hivyo mifumo ya kuuchumi hutofautiana katika kuainisha hitaji la raia na nyenzo zakutumia katika kulikimu hitaji husika.

Inawe kuwa mfumo Fulani unakubali kuwa hitaji Fulani ni moja ya mahitaji yanayo paswa kupata ufumbuzi wa kulikimu na kuainisha nyenzo inayo hitajika kulikimu. Mara nyengine hiyo mifumo tofauti ya kiuchumi inaweza kukubaliana kuwa hitaji Fulani ni moja ya hiitajio linalo stahiki kupatiawa ufumbuzi lakin kwa wakati huo huo mifumo husika ikatofautiana katika njia na nyezo zinazo faa kutumiwa katika kulikimu hitaji walilo kubaliana wote watu wa mifumo hiyo tofauti.

  • Mfano: mifumo yote ya kiuchumi inakubaliana kuwa wanawake ndio kundi la kipekee lililo kuwa mhanga wa umiliki mali, lakin kwa wakati huo huo mifumo hiyo ya kiuchumi imetofautiana katika njia wanazo zitumia wanawake katika juhudi zao za kumiliki mali. Baadhi ya mifumo imekubali wazi wazi kuwa ngono ni moja ya njia za wanawake kutumia ili wakimu mahitaji yao na toa mchngo wa kujenga uchumi wa nchi zao, kwa upande mwengine mifumo ya kiuchumi imeharimisha suala ya wanawake kujiuza ili kukimu mahitaji yao.

Hii ni moja ya sababu kuu inayo pelekea duniani kuwe na mifumo mingi ya kiuchumi kwa kuwa tu mifumo hiyo huanjisha na watu wanaoishi katika maeneo tofauti, watu walio na Imani na itikadi tofauti…

Mara nyengine huja hitajio au tatizo la kiuchumi likachukuwa sura ya mtu binafsi pia huja kipachukuwa sura ya kijamii. Yaani maslahi ya watu mmoja mmoja na masilahi ya jamii zima. Jambo linalo kupelekea sindo fahamu baina ya kukimu mahitaji ya watu binafsi au mahitaji ya jamii kwa jumla. Yaani inapo hudumia jamii kwa jumla watu binafsi huwa pia wana nufaika kinyume na kukimu mahitaji ya watu binafsi maana jamii huwa ndio inayo umia na kupata madhara.

ni wakati wa kuashiria kuwa duniani kuna :

  • mfumo wa kiuchumi ulio toa kipau mbele kwa maslahi ya mtu binafsi na kupuuzilia mbali maslahi ya jamii kwa jumla, hoja yao kuu ni kwamba mifumo husika unapo toa kipau mbele kwa mtu binafsi bila shaka watu wote mmoja mmoja wakatumia fursa hiyo. Jambo litalo pelekea maslahi ya jamii kupatikana japo sio kwa njia ya moja kwa moja. Falsafa yao hiyo imejengwa katika misingi walio iita ULIBERALI ulio badilika na kuwa UBEPARI (liberalism). Eti kama dunia iliumbwa, aliye iumba haiwacha iwe huru na watu wake wawe huru hamna kuingiliana watu katika mambo ya watu wengine. Nchi zao huendeshwa kwa misingi hiyo kila mmoja yupo mbioni kujikusanyia na kujimilikisha mali hata kama kuna wanyonge wataopata madhara. hilo haliwahusu wao maana hawakuwazuia wadaiwao kuwa ni wanyonge, na wao kuenda mbio katika mbio za kumiliki mali. Falsafa hiyo imeleta kukuwa sana kwa milki binafsi na muonekana maendeleo ya sekta binafsi bila kujalisha watu walio wengi kujikimu kimaisha au laa. Jambo linalo pelekea kuweko kwa baadhi ya watu na wengi sana kukosa kiajira na kipato hatima yake kusababisha mmomonyoko wa kiuchume kudhihiri kila inapo dhihiri uhaba wa kukimu mahitaja ya walio wengi katika jamii husika. Haitoshi mfumo huo umepelekea wamiliki wa mali kusababisha kimakusudi soko la bidhaa. kazi yao ni kuficha bidhaa ili uchache huo wa bidhaa sokoni usababishe mlipuko wa bei kutokana na idadi kubwa ya wanaohitaji kuto kupata bidhaa hitajiwa. Suala linalo fikia hatima ya kudhihiri kustawi mzuri wa jamii katika baadhi ya maeneo na kudhorota kwa ustawi wa jamii katika maeneo mengine ya nchi moja. Kuzukwa kwa tabaka za kijamii kuligana na mapato ya wanajamii husika na kuondoa upendo baina yao na tunapo geuza upange mwengine wa sarafu tutakuta kuwa kuna kuzidi chuki baina ya raia wa nchi moja kila mmoja akijenga chuki yake kutokana na hali yake ya kijamii aliyo nayo.

  • mfumo wa kiuchumi ulio toa kipau mbele kwa maslahi ya jamii kwanza na kupuuzalia mbali maslahi ya watu binafsi maana kwa hoja yao ni kwamba watu binafsi ni sehemu ya jamii. Hivyo maslahi ya jamii yanapo patikana mtu mmoja mmoja anakuwa tayari amesha faidi maslahi husika, Falsafa hii ili leta mfumo wa kiuchumi wa UJAMAA. Walipiga marufuku watu binafsi kumiliki nyenzo za uchumi maana walikuwa wanawatukimisha waajiri kama punda kwa kutishia kuwaachisha kazi. Jambo lililo wapelekea waajiriwa wengi kukubali hali hiyo maana wanapo achichwa kazi hawana sehemu nyengine wa kupata ajira kiurahisi maana waliki ni wale wale tu katika kambuni zilizo mingi. Suala la wa ajiriwa kukosa haki zao na madai yao ya msingi lilipelekea wanyonge na wahangu kuungana kwa lengo la kuwavunja kasi waajiri ili kupata nafuu ya ufanya kazi na kuboresha hali ya maisha yao. Zama hizo za kujikomboa waajiriwa alitokea mtu mmoja aitwaye KARL MARX aliye tumia hiyo chuki ya waajiriwa kwa waajiri wao na kupandikiza chuki zaidi. Badala ya kudai uadilifu baina ya muajiri na muajiriwa wake, Karl Marx alibandikiza chuki zaidi na kudai uharamu wa mifumo kama hiyo. jambo lililo pelekea mali za watu binafsi kupokonywa na kugeuzwa kuwa mali za jamii zisizo kuwa na mmiliki rasmi yaani mali hizo ni mali shirika kwa raia wote... na watu wengi kufa sana tu kwa mshituko ya nyoyo wengine waliuliwa kimakusudi kulipa visasi vya waliyo dhaniwa madhila yalio fanywa na wamiliki wa mali kwa wakati huo wa kabla ya Karl Marx.


Marx alitumia fursa hiyo kiitia dini kasoro na kudai kuwa dini ndio njia inayo tumika katika wa wafanya baadhi ya watu kuwa wahanga, maana walio kuwa wanamiliki mali kwa wakati huo wali kuwa ni vigogo wa hubiri wa dini. Kwa wakatik huo ilikuwa ni dini ya kikristo na madhehebu zake ndio vilivyo kuwa vinaitawala ulaya nzima. jambo lililo washawishi walio kubali sera za Karl marx kupiga marufuku moja kwa moja masuala ya kuhudiri dini ya aina yoyote katika nchi zao.

Alicho kilengo Karl Marx ni kukimu mahitaji ya jamii yaani watu walio wengi kinyume na ilivyo kuwa hapo awali. Kila moja alijikuta ni mmiliki mshirika katika mali iliyo pokonywa na kumilikishwa dola. Yaani kila mmoja ni muajiri na kwa wakati huo huo yeye ni muajiriwa. Yaani watu wote sawa bila tofauti ya kijamii. Jambo lilio tarajiwa kuepusha masuala ya kudhurota kwa nguvu za kukimu mahitaji ya wanajamii na kuepuka tatizo la kiuchumi. Mbali na hilo ni kwamba pia walijikuta maeneo yote katika nchi husika, yalingana kiustawa wa jamii na kupotea kwa matabaka ya kijamii. hata hivyo mfumo huyo wa ujamaa ulipelekea kudhorota kwa kuhudi binafsi za mtu moja moja kwa huja kwamba hata kama atajituma katika ubunifu wa kuongeza mapato,mapato hayo ni shirika na watu wengine ambao wapo wapo bila ya juhudi zozote. Sasa ikiwa hali ndio hiyo, kuna faida gani ya kujisumbua kwa kunya kazi kuliko wengine ! Jambo jengine lililo jitokeza ni suala ya uhudumu serikalini kulikuwa na hali ya mtu binafsi kuhisi kutokupata uhuru halisi alio utarajia hapo walipo amua kuutafuta uhuru wao.


Ama mfumo wa mafunzo ya uislam, mfumo wa uchumi wa kiislamu umetofautiana sana na mifumo miwili tulio iashiria hapo juu. Maana uislam haikushughulishwa na mwanajamii kama yeye bali uislamu unashughulishwa na kuhakiki uadilifu baiana ya mtu binafsi na jamii yake, kwa hoja kwamba manfaa ya mtu moja moja na manufaa ya jamii kwa jumla ni mambo wawili yanayo hitajiana bila kutengana. Hivyo katika kulinga manfaa ya mtu mmoja mmoja, kufanya hivyo ni kulinda maslahi ya jamii moja kwa moja.

Tuna kuomba wewe msomaji wa makala haya usije kuingia katika kosa walilo ingia watu wengi kudhani kwao kuwa mfumo wa kiuchumi wa uislam umetokana na kuunganisha sera za mifumo miwili tuliyo itanguliza hapo juu abayo ni ubepari na ujamaa, laa hasha.

Ukweli ni kwamba sera za mfumo wa uchumi wa kiislamu una misingi ya kipekee isiyo chukuliwa katika mifumo miwili tulio itanguliza hapo juu. Sera za uchumi wa kiislamu zimetokana na itikadi ya mafunzo ya dini kwamba mwanadamu kaletwa duniani kwa lengo la kuhakikisha utashi wa ALLAH unafanyika duniani hapo japo utashi huo ufanyike na kundi dogo la watu.


ALLAH asema katika quraan :


” وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الأَرْضِ خَلِيفَةً ” البقرة 30


Pindi ALLAH alipo waambia malaika: mimi nitajalia duniani kuwe na mtawala atakaye shimamisha (utashi wa muumba) , Kutawalishwa bila shaka kutakuwa kwa kusimamia nyenzo vilivyo ili kuya kimu mahitaji wa wakaazi wa ardhini na kuhakikisha wanafaidika ya nyenzo walizo andaliwa na muumba wao ili wapate kujikimu maishani, bila shakawakiwa chini ya muongozo wa namna wa kuzitumia nyenzo hizo wala si vyenginevyo. moja ya aaya za quraan ya sema :


” وَإِلَى ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُواْ اللَّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَهٍ غَيْرُهُ هُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ الأَرْضِ وَاسْتَعْمَرَكُمْ فِيهَا ” هود 61


Na kwa watu wathamud alitumwa ndugu yao Saleh kuwaambia. Enyi watu wangu, kuabuduni ALLAH hamna muabudiwa mwengine kinyume naye. Yeye ndiye aliye kuleteni duniani na kukufanyeni kuvitawala vyote vilivyomo. Hivyo katika kuitawala na kuiendesha dunia mwanadamu hawezi katu kuepuka kutekeleza amri za muumba wake kwa kuyaepuka aliyo katazwa na kutekeleza aliyo amrishwa.

ALLAH aseka katika quraan:


” أَلاَ لَهُ الْخَلْقُ وَالأَمْرُ ” الأعراف 54 ،


Tambueni kuwa vilivyo umba ni vyake ALLAH na hatima yaw ambo yote ni yake ALLAH.


Hapo ndipo panapo mlazimu muislamu yeyote kukusanya mambo ya kiwiliwili pamoja na mambo ya kiroho na Imani katika juhudi zake za kujikimu maishani na kumiliki mali yaani shughuli zake zote za kiuchumi. Jambo linalo ibua hisia za kuweko muumba, mmiliki wa mbungi na ardhi na vilivyomo.

Hivyo sio ajabu tena kuhudhurisha makatazo ya muumba katika shughuli za kiuchumi katika jamii ya waislam kama tulivyo ashiria huko juu kuwa kuna masuala nanayo athiri maamuzi katika mifumo ya kiuchumi ( jeograjia za maeneo wanakoishi wao, mifumo ya kijamii inayo endesha jamii zao, imani na itikadi za watu husika ... Nk ), bali kufanya hivyo ni kuelekea kuasisi jamii inayoishi chini ya utachi wa ALLAH, sio tu kiimani ikawa imetosheleza bali kiuchumi pia.

Pia lengo kuu linalo paswa alifikie muislamu yeyote popot alipo ni kufanya ALLAH kuabudiwa katika nyanza zote za maisha ya walimwengu. ALLAH asema:


: ” وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالإِنسَ إِلا لِيَعْبُدُونِ ” الذاريات 56.

si kuwaumba wanadamu na majini isipo kuwa waniabudu



·

MAKALA HII YAENDELEA TAFADHALI FUATILIA


Comments


bottom of page