top of page

 

UTAMADUNI NA MAADILI

 

   Utangulizi.

     Kwanza kabisa kabla hatujazungumzia maudhui ya maadili, hapana budi kutambua kuwa maadili na Utamaduni ni mambo mawili yanayo enda sambamba kiasi tulazimika kuwa atapo zungumzia mmoja wetu suala la utamaduni ni vigumu mno kutokugusia suala la maadili, au pia mmoja wetu atapo zungumzia suala la maadili ni vigumu kuwa hatozungumzia suala la utamaduni. Hata hivyo tulazimike kujuzwa kuwa maadili ndio kitovu na uti wa mgongo unao pelekea kuwa hai tamaduni duniani.

A.  UTAMADUNI

  1. Maana ya utamaduni.

 

     Utamaduni ni jumla ya mambo wanayo jitambulisha nayo watu wa jamii fulani au watu wa eneo fulani katika moja ya maeneo duniani. Jamii hiyo ina weza kuwa ni kabila fulani au kundi fulani la makabila kadhaa yanayo ishi katika eneo moja, watu hao hulinda na kudumisha mila na utamaduni wakiwa na lengo la kubainisha kuwepo kwao hai na kutoa taswira ya haiba yao inayo weza kuwatofautisha na watu wengineo walio hamia katika eneo lao la asili au wao(wanautamaduni wanapo hamia) katika maeneo yasiyo kuwa asili yao.

  2. Mambo yanayo dhihirisha utamaduni.

     Pamoja na kukiri kwetu kuwa kuna kitu kiitwacho utamaduni, hapana budi kukiri kuwa suala la utamaduni hudhihiri katika mambo yafuatayo:

  • vyakula,

  • lugha,

  • mavazi,

  • mila,

  • namna ya kuishi ... Nk.

baadhi ya mifano kwa baadhi ya tamaduni duniani:

  • katika bara la Asia jamii ya kichina na makundi yote ya jamii hiyo, wamekuwa na utamaduni wa kula wadudu wa aina zote pia kwa miaka mingi mno wamekuwa wa chemsha mkojo wa binaadani kwa pamoja na mayai ya wanyama wenye mbawa halafu wana kunywa mkojo huo na kula pia mayai husika huku wakirithishana utamaduni huo na kuitakidi kuwa kufanya hivyo kumekuwa kukiwasaidia kiafya na kuwafanya kuisha kwa umri mrefu sana kuliko jamii nyenginezo duniani,

  • nchini tanzania na kenya kuna kabila la masai walio jichukulia umaarufu mkubwa duniani kwa sababu ya kujitofautisha sana na jamii nyenginezo kwa kuto kuachana na lugha na mavazi yao popote walipo. Jambo lililo pelekea hata baadhi ya juhudi za kuunda vijiji vya ujamaa nchini Tanzania, kugonga mwamba katika maaeneo ya kabila hilo. Bali sio rahisi kihivyo kukkuta mmasai akifuatana na mtu wa kabila lengine njiani wakiwa marafiki wa kawaida,

  • nchini india kuna jamii zinazo jinasibisha na utamaduni wa ngono jambo linalo wapelekea wanawake wa jamii hizo kushiriki ngono katika umri mdogo sana hata chini ya miaka 6 na ikawa ni kawaida sana jamii zao kupewa habari za ushiriki wa mtoto fulani wa miaka 7 kushiriki ngono na wanaume zaidi ya mmoja kwa pamoja, si kuambii kwa siku tofauti...ndio kabisa, bali huwa wanafanya sherehe za kila mwaka kuanzimsha siku ya ngono kwao wanajamii husika!

  • jamii za watu wa majangwani wamekuwa na utamaduni wa uvaaji wa majoho (kanzu) tokea enzi na enzi jambo lililo pelekea mitume wote kuibuka na vazi hilo maana wote ni katika kizazi cha jangwani uarabuni na kanaana wote wakiwa ni wana n\ wajukuu wa babu mmoja Ibrahiim.

  3. Sifa za utamaduni.

Pamoja na kuwa tumeelezea hapo juu kuhusi suala la utamaduni, msomaji wa makala haya atakuwa amebainikiwa vyema kuwa suala la utamaduni ni jambo linalo karibia kuwa ni tukufu kwa wanao lisimamia yaani wapo tayari kulilinda kwa hali na mali bali wanaweza kuwa tayari kuziangamiza nafsi zao na kupoteza uhai wao wakiwa katika juhudu za kulinda na kuendeleza utamaduni wao au tamadumi zao. kwa kweli ikiwa ndivyo atavyo elewa msomaji wa makala hii basi atakuwa kapatia kabisa ingawa pia kuna ulazima wa kutambua kuwa utamaduni hauna sifa ya kudumu na kubaki milele pamoja na juhudu kubwa zinazo tumiwa katika kulinda na kudumisha tamaduni.

tukifuatilia vilivyo ni rahisi kuelewa kuwa utamaduni huwa unabadilika kwa mtu mmoja mmoja katika jamii fulani au jamii nzima kubadilika kabisa na kuwacha utamaduni wao.

Moja ya sababu kuu ikiwa sio sababu ya kipekee ya kutumwa mitume dunia ni kuja kubadili tamaduni walizo jiwekea watu katika maaeneo wanako ishi wao. 

Kama tutakuwa tumekielewa tulicho kielezea hapo juu, basi tujue kuwa kuna tamaduni mbaya na zisizo kubalika ingawa wanao zienzi na kuziendeleza wameonekana kuwa wao wazikubali. Jambo la msingi hapa tunataka kulitanabahisha sana, iwapo mmoja wetu hatoukubali utamaduni wa jamii fulani ni bora kwake kutafuta njia sahihi ya kuuzuia au kuubadili badala ya kuukejeli utamaduni husika khasa mkemeaji akiwa katika jamii inayo husika na utamaduni huo. Kukejeli na kudharau mila na uataduni za watu wengine ni ishara ya ukosefu wa uvumilivu jambo linalo weza kutupelekea katika suala la uvunjifu wa amani na salaama baina ya jamii mbili. bali suala la kukejeli au kudharau mambo ya watu wengine, limekemewa na vitabu vya MUUMBA wa mbingu na dunia:

وَلَا تَسُبُّوا الَّذِينَ يَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ فَيَسُبُّوا اللَّهَ عَدْوًا بِغَيْرِ عِلْمٍ 

wala msiwatukane wanao abudu asiye kuwa ALLAH, mkapelekea na wao kumtukana ALLAH kiuadui (kwa kudhani wanalipa kisasi) bila wao kujua ... ''

 zipo pia nchi kadhaa duniani zimeharimisha suala hilo na kuliweka katika kundi la makosa ya jinai kwa kuwa lafungamana na amani na usalaama wa jamii zinazo ishi pamoja au jamii zinazo ishi jirani .

Mwandishi,
Salha Mbilinyi Elieza

  • Facebook
  • Twitter
  • YouTube
  • Tumblr Social Icon
  • Instagram
HOME PAGE.png
MOJA YA TAMADUNI HUKO UCHINA
Anchor 1
MOJA YA TAMADUNI MPAKANI MWA SUDANI, ETHIOPIA NA ERITHREA

Baada ya kugusia suala la lengo la mitume kutumwa, imekuwa bayana kutambua kuwa utamaduni unasifa ya kubadilika. Huko katika maeneo waliko tumwa mitume kulikuwa na tamaduni zisizo kubalika ndio sababu kuwa mitume walitumwa huko.

Mfano Nabii yunus alitumwa niinawah (ninawe) katika vijiji vya sodomo na gomora vijiji ambavyo watu wake walijiwekea utamadunia wa kujamiiana watu wa jinsia moja kinyume na maubule wanaume kwa wanaume na wanawake kwa wanawake kushiriki ngono pamoja. Kwa bahati nzuri ni kwamba mchango wa kuletwa mitume duniani ni kumtoa mwanadamu katika tamaduni mbaya kuelekea tamaduni nzuri.

Baada ya kubaini kuwa moja ya sifa za utamaduni ni kubadilika basi hapana budi ila tu gusie baadhi ya mambo ya nayo changia kubadilika kwa tamaduni.

  4.  Mambo yanayo changia kubadilika kwa tamaduni

hapa tutaashiria mambo husika bila kujalisha ni mrengo gani watamaduni utakao badilishwa au kubadilika. Mambo yenyewe ni kama ya fuatayo:

  • dini,

  • muingiliano wa jamii na jamii,

  • utandawazi,

  • mitaala ya shule,

  • mitandao ya kijamii,

  • vyombo vya habari...NK.

Kidogo kidogo tunaweza kuwa tumefaidika na dondoo zilizopo hapo juu. Sasa tunaweza kugeuza sarafu upande wa pili tukaziwacha vinavyo changia kubadilika kwa utamaduni na kuvitizama vinavyo huwisha na kuendeleza tamaduni duniani.

B.  MAADILI

  1. Maana ya maadili.

    Maadili ni neno linalo ashiria jumla ya mafundisho yanayotolewa katika jamii mbalimbali, ikiwa ni malezi, ili kuelekeza vijana wa jamii husika wakuwa na kulelewa kwa namna ambayo inawajenga kuihuwisha jamii yao nzima. Yaani maadili yanaambatana na makuzi au malezi ya wanajamii fulani katika kuwaandaa warithi wao wanao tarajiwa kuihuisha jamii husika baada ya watu wazima wa jamii hiyo kuishiwa nguvu kama sio kufariki dunia kabisa, maadili hayo hudhihiri katika utendaji wa maisha ya kila leo. Maadili hayo hayo ndio yanayo washawishi watu wajamii husika kuhimiza uendelezaji wa yanayo fanywa na watu wa jamii hiyo au kukemewa vitendo vyao. Hivyo maadili ni jumla ya mambo yanayo kubalika na jamii moja bila kujalisha kuwa madili hayo yanaweza yasikubalike na jamii nyengineyo.

 

     Kupitia tulicho kiandika hapo juu tunaweza kubainikiwa kuwa kuna uwezekano mkubwa maadili ya jamii moja kutofautiana na maadili ya jamii nyengine sababu utamaduni ndio unao hukumu ni maadili yepi yanayo pasha kukubalika katika jamii husika. Hivyo suala na tamaduni kutofautiana duniani ni jambo linalo elewaka na kila mtu. Kubwa zaidi ni kwamba hata sababu zinazo pelekea maadili ya jamii fulani kutokuingiliana na jamii nyengineo, sababu hizo zinaeza kuwa ni sababu za kimaadili. Maana suala la kukubalika jambo fulani kuwa ni moja na mambo ya maadili ya jamii fulani linaambatana na vitu vingi mnoo.

Mfano: imana ya jamii husika, silka na desturi , mazingira inako ishi jamii husika...Nk.

     Kumbe sasa ni jambo la kawaida sana tu maadili ya jamii moja kuwa tofauti na maadili ya jamii nyengine. Hata hivyo kuto kukanusha kuwepo tofauti ya maadili baina ya jamii za wanadamu sio hoja ya kuto kukubali kuwa kuna maadili mabaya na maadili mazuri na maadili bora kuliko yote.

Uhitibisho wa tulicho kielezea hapo juu umo katika video ( tunawashukuru sana BBC, channel ten, Aam TV na ntv bila wao tusinge zipata) tulizo ziweka hapo chini.

Baada ya kujishuhudia tamaduni tofauti katika video ziliopo hapo juu ni vigumu sana kwa mtu mwenye akili salaama, kukanusha kuwa hakuna maadili mbaya na tamaduni bora.

 

  2. Maana nyengine ya maadili

     Katika kukuwa na kutanuka fahamu ya maana ya baadhi ya maneno duniani, kumeathiri pia neno  “ MAADILI ” na kulipa maana pana zaidi kuliko hapo awali.Yaani neno maadili huwa latumiwa katika kuainisha jumla ya taratibu na miongozo au desturi na kanuni zilizo wekwa kwa lengo la uendeshaji wa jambo maalumu bila kuliegemeza neno hilo la maadili, katika suala la tamaduni za jamii mbali mbali za wanadamu duniani.

Hivi sasa kila kazi ina maadili yake nayayo tofautiana na maadili ya kazi nyengineo ingawa kazi hizo zinaweza kuwa chini ya msimamizi mmoja.

          Mfano mahakama za kila nchi zima maadili zake kiasi cha kuwalazimu mahakimu kuto kuruhusiwa kuwa na muingiliano wa kila mtu katika jamii husika, kinyume na maadili ya ualimu mashuleni. Maadili ya kikazi katika sekta ya ualimu ni kuwa mwalimu lazima ajipambe na sifa za muingiliano na wanajamii wote bila kujalisha daraja lao la kijani wala muda unao pelekea wao kujichangani na watu wote katika jamii husika.

 

Sasa, waajiriwa wote katika nchi huwa chini ya muajiri mmoja ambaye ni serikali kuu ya nchi husika yaani hakimu na mwalimu wote wameajiriwa na muajiri mmoja ambaye ni serikali, lakini muajiri huyo huyo ndiye aliye toa muongozo unao pelekea maadili ya kikazi ya hakimu yasilingane na maadili ya kikazi ya mwalimu skulini.

  3. Mmomonyoko wa maadili na kukuwa kwa maadili.

     Hapo juu tumeelezea vya kutosha kuhusu maana ya maadili na kubainisha matumizi tofauti ya neno “ MAADILI “ katika nyanza tofauti katika jamii.

Hivyo baada ya kuelezea tulivyo elezea hapo juu hatuna budi kugusia suala la mmomonyoka wa maadili na kunyume chake pia, yaani kukuwa kwa maadili.

 

     Miaka ya hapo awali kabla ya kuweko mfumo wa serikali kuu duniani katika maeneo tofauti, kulikuweko na mfumo wa serikali ndogo ndogo za kijamii zinye mamlaka ya kijiji au falme za kale kama ufalme wa Mkwawa uheheni. Zama hizo za kale hapakuwa na haja ya kuwekwa maandishi yanayo ratibu maadili ya jamii hizo kwa wakati huo maana wati wakijiji kimaja walikuwa waelewana na kufahamia wao kwa wao kutokana na wao kuwa wanajamii moja na mara nyingi zama hizo hakukuwa na muingiliano wa jamii moja na jamii nyengine kwa kuwa watu wakiishi katika maeneo waliko zaliwa wao.

     Zama hizi za mifumo ya serikali kuu zimetawaliwa na suala la muingiliano wa watu kutoka katika jamii tofauti na maeneo tofauta, watu wanao kutana na kuasisi jiji na na mijiji kwa ajili ya kujiendleza kimaisha. Sasa suala la muingiliano limepelekea tamaduni na maadili tofauti kukutana katika jiji moja au mijini jambo linalo lazimu watu hao wajaribu kuachia baadi ya mambo ya tamaduni zao za asili kwa lengo la kuingiliano na uuwiano wa kuishi pamoja wao walio toka katika maeneo na jamii tofauti, uuwiano unao lazimishwa na maisha ya kutafuta kuvumiliana ili salama na amani ipatikane baina yao makaazini kwao katika jiji lao jipya walilo liasisi.

Ikiwa tumeeleweka katika tulio yabainisha hapo juu tutakuwa tumetambua chanzo cha kuanzishwa mifumo ya serikali kuu duniani na kuhama maisha ya mifumo ya vijiji vya awali kuelekea katika mfumo wa kuasisi jiji na miji duniani. Uasisi wa miji ndio ulio pelekea kuanzishwa kwa mifumo ya serikali kuu, serikali zinazo lazimika kuweka bayana misingi ya kupatikana kwa uvumilivu baina ya watu wa jiji moja walio toka katika asili ya jamii tofauti. Uvumilivu huo baina yao huanzishwa kwa leongo ya kupatikama na kutumisha salama na amani baina yao jijini kwao. Sasa kutokana na kuwa jiji au miji huanzishwa na watu kutoka katika jamii tofauti yaani watu wasio tambuana wala kuingiliana kitamaduni. Hapo sasa kuna ulazima serikali ya jiji hilo jipya kuweka kimaandishi mambo yanayo tarajiwa kufanywa na watu wa jiji hilo jipya, pia kuweka kimaandishi mambo yasiyo ruhusiwa kufanywa na wakaazi wa jiji hilo jipya. Hiyo ndio taswira ya kuasisiwa katiba na kanuni za nchi mbali mbali duniani, wala sio ajabu pia katiba na kanuni za nchi hizo kuweke vipengele rasmi vitakavyo itwa kuwa ndio muongozo wa maadili kwa raia wote wa nchi hizo. Bila bila shaka katika kuitengeneza hiyo miongozo  huzingatiwa tamaduni na maadili ya jamii tofauti za jiji au miji au nchi husika, yaani huingizwa katika katiba maadili yanayo kubalika, kutoka katika katika kila jamii zinazo husika. Hivyo sio ajabu baadhi ya jamii zikajikuta kuwa katika katika hakukuingizwa lolote kutoka katika tamaduni za jamii zao au sio ajabu kuwa katika katiba imejaa mambo yanayo endana na utamaduni na maadili ya jamii fulani. Sababu kuu inayo pelekea hali kuwa hivyo mara nyingi ni kuwa maadili fulani yalikubalika kuwa ni bora kuliko maadili mengine ingawa katiba hiyo hiyo inaweza kuziruhusu jamii fulani kuendelea na tamaduni zao madamu tamaduni hizo hazikuvunja wazi wazi katiba mama kwa taifa husika.

Sasa nakuomba utambue nini kinacho kusudiwa kila utapo sikia latamkwa neno " Mmomonyoko wa maadili ". Mmomonyoko wa maadili ni hali nzima ya kukiukwa jambo au baadhi ya mambo yaliyo ratibiwa kuwa ndio maadili na jamii fulani kama tulivyo elezea kwa undani hapo juu.

 Mfamo wa miongozo (kanuni) iliyo ratibiwa kuwa maadili kwa raia kwa nchini Tanzania    

C.  HUKUMU YA MMOMONYOKO WA MAADILI

Makala haya yaendelea

Tafadhali tunaomba maoni yako kuhusu makala hii

bottom of page