top of page
HOME PAGE.png

HUDUMA BILA MALIPO KWA WANAFUNZI

MUSTAKBALI NA HATMA VIZAZI KATIKA JAMII YETU UMO MIKONONI KWA VIJANA WETU . LEO HII ASILI MIA KUBWA SANA YA VIJANA WAISLAM WAMEBAKI WAKIJINASIBU NA UISLAM HALI YA KUWA WAPO MBALI NA UISLAM HALISI KIUTENDAJI NA KIITIKADI, JAMBO HILI LIMECHANGIWA NA HALI YA WATU WAZIMA KUKAA MBALI NA VIJANA. KUNA HAJA KUBWA YA KUANZISHA JUHUDI KATIKA MAENEO MBALI MBALI KWA AJILI YA KULINDA VIJANA WETU NA MAMBO YANAYO WAWEKA KANDO NA DINI WAKIWA WAO HAWANA HABARI KABISA. HIVYO SISI TAYARI NI SEHEMU YA JUHUDI HIZO INGAWA CHANGAMOTO ZA NDANI NA NJE YA JAMII YETU NI KUBWA SANA KULIKO UWEZO WETU. HATA HIVYO TUTAENDELEA KADRI ATAVYO TUWEZESHA ALLAH. 

VIJANA NDIO JAMII

01

FIQHU NA ITIKADI

Kuwafundisha mambo muhimu katika dini kiasi waishi maisha yao wakuwa waelewa majukumu yao kwa mola wao na jamii kwa jumla, kwa mujibu wa maelekezo ya Uislm 

03

UONGOZI BORA NA SALAAMA

Huwa tunatoa mafunzo ya utawala, uendeshaji na uongozi kwa vijana wetu. Hii ni baada ya kubaini kuwa vijana wetu wamekuwa wa kiharibikiwa katika uongozi wa umoja wa vijana waislam huko mashuleni. 

05

MAFUNZO YA SAIKOLOJIA

Kutokana na umuhimu wa saikolojia kwa viumbe walio hai, tumekuwa tukitoa mafunzo hayo kwa vijana wetu ili watape uelewa wa mambo yanayo jiri katika mazingira wanako ishi wao. Jambo litakalo wasaidia kuepuka "unenguaji wa ngoma sio zao".

02

MAISHA YA BAADA YA MASOMO

Uhalisia wa vijana wengi wakiwa masomoni huwa wapo mbali na kutambua kuwa ndoto zao za maisha zinaweza kuishia hewani na kubaki kuwa zilikuwa ni ndoto za alinacho. Jambo hili huchangiwa sana na uhalisia wa maisha walio yaishi vijana wetu tokea safari yao ya kutafuta elimu.

Hivyo tuliona haja ya kuwajuza wasio yajua kuhusi uhai na maisha.

04

TUITION

Utatuzi wa kitaaluma kwa wanafunzi walio na matatizo katika masomo yao. Tunapanga program kwa mujibu wa viwango vya kitaaluma. Programu hizo ni kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari tu. Mafunzo hayo ni bila malipo. Hata hivyo zipo taratibu za kufuatwa ili kujiunga,

06

KUENDESHA MIJADALA

Tunayo programu ya kuendesha mijadala (debats) ili kukuza viwango vya usimamishaji wa hoja kwa vijana wetu kila inapo wabidi kufanya hivyo maishani mwao.

KUWEPO TUPO ILA TU NI WADOGO DUA ZENU TU  ... ILI TUENDELEE KUWEPO KIHUDUMA. 

MWANDISHI

bottom of page