top of page
HOME PAGE.png

MASJIDUL MADINATUL MUNAWARAH

Asalaam alaikum wa rahmatuLLAH wa barakaatuh.            
 
MNAMO mwaka 2018 tulipata fursa ya kupewa usimamizi wa Masjidul Madinatul Munawarah iliopo Dar es Salaam Ubungo, Kwembe Mloganzila. Masjidul Madinatul Munawarah ilijengwa  mwaka 2016 na kumalizika mwaka huo huo, halafu ikakabidhiwa wanakijiji.

​

Kwa bahati, maimamu wote walio kuwa wakiletwa hapo hawa kuwa wakaazi maana kati yao hakunaaliye subutu kukaa japo miezi 2, jambo lililo pelekea msikiti kufungwa kwa kipindi cha miaka miwili na mieki kadhaa kutokana na ukosefu wa imaamu.

​

​

Mnamo 2019 mwezi wa kwanza tulikabidhiwa dhamana ya uendeshaji wa msikiti husika hadi leo hii 22 December 2021 siku ya kuandika Makala haya. Miezi 9 Baada ya kukabidhiwa dhamana tuliamua kuwatafuta

Pamoja na changamoto nyingi tuliamua kuwaendeleza wanafunzi wtu hao wane. Hata hivyo wanafunzi wetu hao walitupa moyo sana maana walikubaliana na hali ilivyo na wakawa tayari kuwa wanalima mashamba kwa

SIKU YA KWANZA YA KAMBI, 24 /11/ 2019

wanafunzi kwa lengo la kuuhuisha. Tuliwapata vijana wanne wa kiume kutoka mkoa wa lindi kilwa masoko. Baada ya wiki mbili tu ilitubidi kumrejesha mmoja wao makwao maana tulibaini kuwa sio msomaji halisi, tukabakisha wanafinzi wa tatu.

Kutokana na changamoto za kiuchumi tulilazimika kubaki na idadi hiyo hiyo ya wanafunzi watatu ila baada ya mwaka mmoja alijiunga mwanafunzi mpya wa kike aliye kuwa akisoma mkoani mwanza, na kufanya idadi yao irudi kuwa ni wanafunzi wane. 

Lengo la kujikimu kimaisha huko wakisoma elimu ya dini.

Wakati huu wa kuandika Makala haya wanafunzi wetu wamesha timiza miezi 26 kamili tukiwa nao kimuhanga kama Picha za vivedo zinavyo enesha hapo chini. Licha ya yote hayo ni kwamba Masjidul Madinatul Munawarah imejengwa katika sehemu yenye wakristo wengi jambo lililo changia maimamu walio tutangulia kushawishika kukimbia. Vile vile suala uchache wa waislamu katika eneo husika lina athari hasi kwa

​

maendeleo ya Masjidul Madinatul Munawarah kwa sura binafsi ya masjidi na kwa sura ya Uislam wote katika eneo husika. Moja ya athari hasi hapa masjidul Madinatul Munawarah ni kwamba masjidi yavuja sana kiasi cha kudhorotesha shulughi za kitaaluma hapa masjidi.

Ujasiri tuliamua kujivisha kutokana na kwamba hatuna njia nyengineyo ya kutumia ilikuziepuka changamoto zinazo tukabili. Dini tunaitaka na changamoto zatukabidi, tukaamua kwa dhati kukubali muhanga ili tujiendeleze kidini. Zifuatilieni video mtapata taswira halisi ya muhanga tunayo ipitia kituoni kwetu.

Miaka yetu hii ni miaka ya zama za mwisho, watu hawapo tayari kutumia pesa zao kwa ajili ya mafanikio halisi ya didi. Sasa njia ya kipekee ya kupambana na changamoto za kiuchumi kituoni kwetu na baada ya kuhitimisha wanafunzi wetu, ni kutoa mafunzo ya standi za kazi  ili kumuepusha mwanafunzi wetu kuwa ni tegemezi katika maisha yake ya uhudumu wa kidini.

​

bottom of page