Global Services High Targets
LEADERSHIP – ENTREPRENEURSHIP – VOLUNTEERING
BRELA ID No: 465066, TIN:
BAKWATA ID: BKT /MDRS/O2O/O1O15
0768649111 – 0675103790 – 0777496444 – 0772496444
Email: gshcourt@gmail , uddgshcourt@gmail
TANZANIA DAR es SALAAM, UBUNGO KWEMBE, MLOGANZILA
UBUNGO, KWEMBE, MLOGANZILA

HUDUMA ZA KITAALUMA NA MAFUNZO
KATIKA WANAFUNZI 100 WALIO OMBA TUMEWADAKHILI 4 PEKEE YAO MAANA WAO NDIO WALIKIDHI VIGEZO NA MASHARTI YETU, DAR es SALAAM 2019
SIKU YA MTIHANI WA KUSOMA QURAAN KATIKA MAFUNZO YA KOMBUITA NA UJASIRIAMALI KWA KINAMAMA WA NYUMBANI, UNGUJA ZANZIBAR 2017
BOFYA PICHA HIZI ...TULIO WALENGA
UONGOZO WA VITUO KWA WANAFUNZI
utangulizi:
Kama ilivyo amrisha dini yetu, hivyo ndivyo inavyo tarajiwa tuwe katika utendaji wetu wa kila leo.
Moja ya mambo muhimu iliyo yahimiza dini yetu ni suala la nidhamu popote walipo waislamu. Zipo dalili nyingi tu katika quraan na sunnah zinazo zungumzia waziwazi suala la nidhamu baina ya waislam. Baadhi ya dilili zenyewe ni kama zifuatazo:
﴿ إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ وَإِذَا كَانُوا مَعَهُ عَلَى أَمْرٍ جَامِعٍ لَمْ يَذْهَبُوا حَتَّى يَسْتَأْذِنُوهُ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَأْذِنُونَكَ أُوْلَئِكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ فَإِذَا اسْتَأْذَنُوكَ لِبَعْضِ شَأْنِهِمْ فَأْذَن لِّمَن شِئْتَ مِنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمُ اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴾ (النور : 62
Hakika ya waumini walio muamini ALLAH na MTUME wake, wanapo kuwa na Mtume katika jambo la pamoja huwa hawaondoki mpaka wamuombe Mtume ruhusa. ( Ewee MUHAMMAD ) Hakika ya wanao kuomba ruhusa, hao ndio wakamilifu wa kumuamini ALLAH na MTUME wake (kwa wakati husika). Hivyo watapo kuomba ruhusa kwa ajili ya badhi ya mambo yao, basi mruhusu umtakaye kati yao na uwaombee msamaha kwa ALLAH. Hakika ALLAH ni Msamehevu na Mhurumivu. suratun Nuur aya 62
« إذا خرج ثلاثة فى سفر فليؤمروا أحدهم »
Wanapo safiri watu wa tatu basi wamfanye mmoja wao kuwa kiongozi
« المسلمون عند شروطهم إلا شرطا حرم حلالا أو شرطا أحل حراما »
Waislamu hutekeleza waIio kubaliana baina yao isipo kuwa makubaliano yanayo haramisha jambo la halali au makubaliano yanayo halalisha jambo la haramu
Dalili zinazo amrisha kuwepo nidhamu baina ya waislamu popote walipo ni nyingi zaidi ya hizo zilizotajwa lakin tunaweza kutosheka na dalili tatu hizo hapo juu.
Ni wazi kabisa kwamba dalili hizo za faidisha umuhimu wa kuwepo nidhamu baina ya waislamu hata kama idadi yao ni ndogo.
Vivyo hivyo, kituoni kwetu tumeweka nidhamu maalumu atakayo ifuata mfaidi (mwanafunzi) yeyote wa huduma za kituo chetu bila pingamizi lolote, nidhamu husika ni kama ifuatayo:
KANUNI NA MIONGOZO:
-
Hakikisha umesoma na umeelewa halafu umiliki nyaraka zote za miongozo yetu popote ulipo, maana kuto kuujua muongozo au kanuni sio udhuru wa kusalimika na adhabu,
-
Kwa lengo la kuhuisha dini kwa watoto ni marufuku kipindi chote cha likizo au nyakati zisizo kuwa za shule wanafunzi wote wa madrasah watalazimika kuwepo madrasah ila kwa watakao toa taarifa na taarifa hiyo ikakubalika kisheria, hali kadhalika ni lazima wanafunzi wote kushiriki sala za jamaa misikitini.
-
Mwanafunzi yeyote wa kike ni lazima avae nguo za hijabu popote alipo nje ya eneo la madrasah, pia ni lazima kwa wanafunzi wote wa kike na wakiume kuvaa sare za madrasah muda wote nyakati za kusoma na nyakati za ziara mbali mbali zinazo andaliwa na madrasah nje ya madrasah. Marufuku watoto wa kike kucheza michezo na watoto wa kiume ndani na nje ya madrasah.
-
Suruwali ni vazi la lazima kukaguliwa kwa wanafunzi wa kike ndani ya baibui zao, pia wanafunzi wa kiume ndani ya kanzu zao,
-
Marufuku mwanafunzi yeyote kujihusisha na shughuli za kutafuta pesa nyakati za madrasah. Pia ni marufuku wazee wa wanafunzi kuwashughulisha wanafunzi na kazi za nyumbani ila kwa taarifa maalumu atakayo itanguliza mzee kabla ya kumshughulisha kijana wake
-
Ni marufuku ishara yoyote inayo husu siasa ya aina yoyote ya ndani ya nchi au nje ya nchi au chama chochote kinacho daiwa kuwa cha itetea dini mfano wa hizbu tahriri na ikhwanu muslimina…Nk.
-
Pia ni marufuku ushabiki wa vyama vya kisiasa ndani au nje ya kituo chetu kwa kipindi chote atakacho kaa mfaidi(mwanafunzi) kituoni kwetu, hali kadhalika ushabiki wa team za mipira hauruhusiwi kabisa.
-
Kituo kimeanzishwa kwa ajili ya kuwaendeleza vijana kuielekea dini ikiwa ni takrima (motisha,motivation) kwa wanao taka kuitumikia jamii na dini wala si vyenginevyo. Hivyo sasa asije mtu kujiunga na kituo chetu akiwa hana lengo la kuwa mlinganiaji na muhamasishaji wa maadili mema na imani ya dini ya kiislam,
-
Ni lazima kwa kila mwanafunzi kupasi masomo yote anayo soma kituoni kwa pasi ya 60 %, vinginevyo atazuiwa kukaa kituoni mara moja bali ikibainika kwamba hakuja kusoma dini na badala yake alitafuta makaazi tuu hapo atachukuliwa hatua za kimahakama ili arejeshe gharama za huduma kwa kipindi chote alicho hudumiwa,
-
Kila mmoja ana wajibu wa Kujilazimisha kutii kanuni za nchini hapa bila ya shuruti yoyote na miongozo mbali mbali inayo wekwa na uongozi wa nchi na serikali za mitaa isipo kuwa muongozo utakao bainika kuwa utekelezaji wake kidini na kiimani ni mgumu,
-
Uongozi wa kituo cha Global Services High Targets unajivua jukumu la uhalifu wa aina yoyote unaoweza kufanya na mtu tunaye shirikiana naye katika huduma, iwe uhalifu huo kaufanywa ndani au nje ya kituo, bali uongozi wetu utashirikiana na viongozi wa kijamii katika kumurekebisha au kumsalimisha mhalifu hata kama ni mfaidi (mwanafunzi) wa huduma zetu,
-
Muongozo huu unakamilisha makubaliano au mkataba uliyo sainiwa na mzee wa mfaidi (mwanafunzi) wa huduma zetu kituoni,
-
Ni lazima kwa wafaidi (wanafunzi) wa huduma zetu kuwaheshimu wanakijiji na kujiepusha na jambo lolote linalo weza kusababisha ukosefu amani au kuleta adha yoyote iwayo kwa wanakijiji,
-
Mwanafunzi yeyote wa kike haruhusiwi kwenda popote japo dukani … mahitaji yake atayapata kwa kukabidhi pesa kwa viongozi wa kituo kwa ajili ya kumchukulia mahitaji yake dukani , pia wanafunzi wa kiume hawaruhusiwi kuondoka kituoni bila ruhusa na idhni ya viongozi wa kituo,
-
Ni lazima kwa wafaidi (wanafunzi) wa huduma zetu kutoa kipaumbele maslahi ya wanakijiji katika kila watakalo lifanya kwa muda wowote ndani na nje ya eneo la kituo chetu,
-
Haturuhusu kaswida wala mziki wa aina yoyote ndani na nje ya kituo chetu, tunahimiza wafaidi (wanafunzi) kuwa ni vigezo bora hata wakiwa nyumbani kwao au barabarani,
-
Ishara au kitendo chochote kinacho husiana na masuala ya ngono hakitovumiliwa kwa hali yoyote, wanandoa wapo huru kukaa faragha nje ya eneo la kituo bila kuathiri shughuli zetu kituoni vyenginevyo tutawazuia moja kwa moja,
-
Ishara au mazungumzo kuhusu ngono ni marufuku kabisa kituoni kwetu.
IMANI NA ITIKADI:
-
1.Tunaendeshwa na misingi ya dini ya kiislam hivyo kila mmoja ajilazimishe kufuata kiutekelezaji maamrisho ya dini na matendo yoyote yanayo lazimiana na itikadi sahihi ya uislam. Tuna sare maalumu kwa wafaidi (wanafunzi) wetu nayo ni kanzu safi kwa vijana wa kiume na hijabu kamili ikiwemo nikabu kwa vijana wa kike. Lazima kila mwanafunzi aje na musahafu wake, vitabu vyake, jembe na kisu ikiwemo vitendea kazi vyake mwenyewe tokea siku ya kwanza ya kuhudhuria kituoni kwetu kwa ajili ya kupata elimu,
-
Mwanafunzi :
-
Wa kudumu kituoni haruhusiwi kuwa na nguo Zaidi ya nne:
-
Wanawake wasizidishe juu ya mashuka mawili mashungi matatu, baibui 3 gauni 3 na pea 3 za viatu,
-
Wanaume wasizidishe juu ya mashuka mawili kanzu nne na suruwali nne vilemba 3 na pea 2 za viatu,
-
-
Wanafunzi ya muda mfupi haruhusiwi kuwa na nguo Zaidi ya tatu:
-
Wanawake wasizidishe juu ya mashuka mawili mashungi mawili, baibui 2 gauni 3 na pea 2 za viatu,
-
Wanaume wasizidishe juu ya mashuka mawili kanzu tatu na suruwali mbili kilemba 1 na pea 2 za viatu,
-
-
-
Nimarufuku kituoni kwetu kuvaa nguo yoyote inayo onesha au kudhihirisha maumbile ya mvaaji hata kama ni watu wa jinsia moja,
-
Nimarufuku kituoni kwetu kuvaliana nguo au viatu, kugusa vitu tusivyo vimiliki iwe vitu hivyo ni mali ya wanafunzi wenzetu au mali ya wageni au mali ya kituo. Atapo hitaji mmoja wetu anaweza kuomba ruhusa na kusubiria iwapo ataruhusiwa au atanyimwa,
-
Nguo yoyote inayo eleweka kwamba ni ya kuvaa katika fukwe za starehe au chumba cha kulala au inayo bana mwili hairuhusiwi katu kuvaliwa kituoni kwetu wala katika mazingira ya kituoni hapa,
-
Tunahimiza uvaaji wa nguo za heshima kidini na kuepuka nguo za watu wa mitaani au za wanamziki.
-
Ni marufuku matumizi ya simu kituoni kwetu wala haruhusiwi mtu kuibeba simu katika kipindi chote atakacho kuwa kituoni kwetu isipo kuwa mwanafunzi aliye jiunga na mafunzo ya ujasiriamali kwa sharti asiathiri shughuli zetu kituoni
KITUO NA MAENEO YAKE:
-
Viongozi wote wa vitengo/vyumba watapatikana baina ya wanafunzi kwa “kura ya bahati” kama tutavyo ibainisha hapo chini katika kipengele kinacho fuatia hapo, isipo kuwa kiongonzi mkuu wa wanafunzi kituoni atapendekezwa na Global Services High Targets, kiongozi huyo ni lazima asiwe muajiriwa wetu,
-
Baina ya wafaidi (wanafunzi) wa huduma zetu kuna viongozi katika kila kitengo/chumba, ambao wapo chini ya kiongozi wao mkuu aliye ainishwa na kituo. Kiongozi mkuu atapendekezwa na Global Services High Targets na atakuwa yeye ndiye kiongozi wa chumba anacho kaa yeye. wajumbe wawili watapigiwa kura kwa kuandikwa majina ya viongozi walio baki baina ya viongozi wa vyumba, jina la kila mmoja wao litaandikwa kwenye karatasi, halafu zitavutwa karatasi mbili na hao ndio watakao kuwa wajumbe wasaidizi wa kiongozi mkuu wa kituo. Kiongozi mkuu yeye ndiye msimamizi wa ratiba zote za Global Services High Targets kituoni upande wa wanafunzi,
-
Tukiwa katika msafara au ziara ya kituo chetu nje ya hosteli zetu nilazima kwetu kulinda usafi wa mazingira na mandhari husika yaendane na hali ya eneo au sehemu husika. Bali tukiwa katika ziara ni lazima tuwe kuliko tunavyo kuwa hosteli au nyumbani. Nguo tusianike popote na vyovyote. Wanawake ni lazima waanike nguo zao kwa stara sana kiasi tukipata ugeni wa ghafla wasikute nguo zimeanikwa popote na vyovyote. Nguo huanikwa kwenye kamba nje tukizingatia nguo za ndani kuwekewa juu yake nguo za kawaida. Pia nimarufuku kuvua nguo vyumbani ila tukiwa na stara kamili,
-
Tunaishi kituoni kama ni ndugu washirika wanao saidiana baina yao. Hivyo itapo tokea kutoka kwa pamoja baadhi ya wafaidi wa huduma zetu ( yaani wanafunzi) nilazima kwao kurudi kwa pamoja kama walivyo toka, kufanya hivyo itaturahisishia kuelewa lolote litakalo mtokea mmoja wao jambo litakalo tufungua namna ya kuliendea tatizo husika... sio ombi ni amri kwa wote,
-
Tutakuwa na mchango wa kiwango cha dola 1 za kimarekani kila jumatatu au jumamosi tunapo rudi kutoka majumbani ikiwa ni mchango wa matumizi ya dharura kwa ajili na huduma za afya inapo tokea dharura. Pesa hizo atazikusanya kiongozi wa kila chumba na kumkabidhi kiongozi mkuu wa kituo ambaye ni mmoja wa wafaidi (wanafunzi) wala sio muajiriwa wa Global Services High Targets. Pesa za mchango wa kila mwanzo wa week wanapo rudi watu kutoka nyumbani sio za umeme wala ukarabati bali ni kwa ajili ya dharura ya kiafya ambayo inaweza kujitokeza kwa mmoja wetu kituoni hapa. Pesa hizo atakaa nazo kiongozi mkuu hadi likizo ya semester , ikitokea dhrura ya kiafya haikujitokeza basi kila mmoja atarejeshewa haki yake kama alivyo toa. Ama inapo tokea dharura ya kiafya na pesa hizo zikatumika lazima wa arifiwe wachangiaji wapate kuelewa kiasi gani cha pesa zilizo tumika, pesa hizo zitazingatiwa kuwa ni msaada wa wachangiaji kwa mwenziwao aliye patwa na dharura hiyo ya kiafya. Dharura ya kiafya ni pale tutapo lazimika kukodi gari kwa haraka kwa ajili ya kumuwasilisha mmoja wetu katika moja ya vituo vya afya, pia ni lazima mhusika awe katika eneo la kituoni au katika moja ya shughuli zetu nje ya kituo vyenginevyo hiyo haitazingatiwa kuwa dharura inayo tuhusu bali wazee wa mhusika ndio watakao himili gharama husika. Magonjwa ya kawaida au yasio kuwa ya ghafla hayo hayazingatiwi kuwa ni dhrura ya kiafya,
-
Michango yoyote ya pesa kituoni watasimamia, watahifadhi na wataendesha wanafunzi wenyewe wakiwa waondio wamiliki wa pesa husika, kituo cha Global Services High Targets kitafuatilia tu jinsi gani watavyo tumia pesa hizo kwa maslahi ya kila mmoja wao.kipengele hiki ni kwa ajili ya wanafunzi wa muda tu,
-
Mchango wa umeme utatolewa kila mwanzo wa mwezi,wenyewe wafaidi (wanafunzi wa ujasiriamali) ndio watakao amua kiasi gani cha pesa achangie mmoja wao. Mchango wa umeme atausimamia kiongozi wao mkuu. Hairuhusiwi kutumia umeme kwa shughuli za kupikia au kuchemsha maji wala kupiga pasi ila kwa makubaliano baina ya wanafunzi kwa muwafaka wa Global Services High Targets, vyenginevyo hatua kali zitachukuliwa kwa atakaye kwenda kinyume na hivyo (kipengele hiki kina wahusu wanafunzi wa ujasiriamali tu ),
-
Mchango wa ukarabati utatolewa na wanafunzi wote kila itavyo hitajika (kipengele hiki kina wahusu wanafunzi wa ujasiriamali tu ) kutokuhudhuria kwa mwanafunzi sio sababu ya kutohusika na mchango lengwa,
-
Usafi wa pamoja ndani na nje ya kituo katika sehemu zisizo maalumu kwa mtu, utakuwa ni lazima kwa kila mwanafunzi bila pingamizi yoyote na utafanyika kila baada ya week mbili au kwa dharura inapo bidi kufanya hivyo. Ama usafi wa chumbani utawalazimu tu wanao kaa katika chumba husika, usafi wa kumbi za mihadhara na madarasa hapa kituoni utafanywa kila siku kwa taratibu watazo jipangia wanafunzi na kuripoti taratibu hizo kwa uongozi wa Global Services High Targets
-
Yeyote atakaye haribu chochote basi uharibifu huo utakuwa katika dhima yake kikamilifu na ni lazima kwake kufidia alicho kiharibu,
-
Kila mmoja ajihadhari na auchunge mzigo na mali zake, hivyo yeyote atakaye ibiwa atakuwa mwenyewe amechangia kutokea tukio hilo, kituo hakitohusika kwa lolote.
-
Kituo kimeandaliwa kwa ajili ya watu walio tayari kusoma, kujifunza ulinganiaji na uhamasishaji wa maadili mema na imani ya dini ya kiislam na wakawa tayari kujitolea kwa ajili ya kazi hiyo. Hivyo ni muhimu kuzingatia sana maandalizi ya kila kipindi cha kusoma kwa saa moja kamili kabla ya kuanza kipindi au semina au shughuli nyenginezo kuanza. Ni lazima kila mmoja awe amesha hudhuria eneo la tukio (ratiba) kwa nusu saa kabla ya ratiba kuanza, uchelewaji wowote na kutokuhudhuria ipaswavyo itakuwa ni sababu ya kuchukuliwa hatua hata za kimahakama ikibidi kufanya hivyo,
-
Taa ziwashwe saa 10 ya alfajiri na kuzimwa baada ya jua kuchomoza tu, na mwisho wa kuwasha taa za vyumbani ni saa tano kamili usiku.
-
Baada ya saa tano hakuna mazungumzo vyumbani ila kwa makubaliano ya wanachumba bila bughudha kwa vyumba vingine. Mwisho wa kukaa na kuzungumza nje au ndani ya kituo ni saa tano kamili wakati wa taa kuzimwa. Yeyote ataye kuwa na ratiba ya kusomo kwa wakati wa kuzima taa basi ni lazima kwake kuelekea sehemu inayo husika wala sio katika vyumba vya kulala,
-
Likizo yoyote isiyo kuwa ya semester na siku kuu za idi haizingatiwi kuwa ni likizo. Hivyo kuweko kwetu kituoni ni lazima. Likizo ya idi itakuwa siku nne kuanzia jioni ya kuamkia siku kuu hadi asubi ya siku ya tano tokea sherehe za siku kuu. Hivyo sasa kuhudhuria kituoni mwisho ni saa kumi na mbili jioni ya siku hiyo ya tano tokea sherehe za siku kuu ya mwanzo. Jumamosi ni siku ya kulala nyumbani kwa wanao taka, na kurudi jumapili mwisho saa kumi na mbili, magharibi watasali kituoni. Wala hakuna ruhusa ya kwenda nyumbani kwa siku zisizo jumamosi na likizo ya mwisho wa semester ila kwa ruhusa ya Global Services High Targets (kipengele hiki kina wahusu wanafunzi wa ujasiriamali ).
-
Wanafunzi wa dini wataruhusiwa ziara za jamaa zao kila baada ya miezi sita kwa taratibu zitakazo pangwa na uongozi wa kituo,
-
Hairuhusiwi kuwaingiza kituoni watu wasio kaa kituoni, siku ya ziara ya kuwapokea wasio kaa kituoni ni moja tu nayo ni kila alkhamis baina ya adhuhuri hadi saa kumi na moja jioni, pia wageni wa wanafunzi hawato ruhusiwa kuingia vyumbani, watakaa mapokezini na kukutana na jamaa zao hapo hapo au nje katika eneo la kituo,
-
Hakuna ziara kwa wanaume katika kituo cha wanafunzi wa kike wala ziara kwa wanawake katika kituo cha wanafunzi wa kiume ila mzazi wamwanafunzi tu au jamaa yake mzazi lakin kwa ruhusa kutoka kwa mzee wa mwanafunzi kimaandishi au kwa maelekezo ya simu kupitia namba rasmi ya mzee iliyo sajiliwa kituoni kwetu Global Services High Targets,
-
Maadili ya dini ndio suala la kipaumbele kwa dira yetu, hivyo tujilazimishe kuyaepuka maadili yasio ya dini, na lugha mbaya kwa wenzetu. Yeyote atakaye fanyiwa maudhi au uadui na mwanafunzi mwezniwe au mwalimu tunamuomba aripoti kwa viongozi wa Global Services High Targets walio karibu naye kwa wakati huo, wala sio kujichukulia hatua mwenyewe na hatamu ya sheria mikononi mwake, atakaye fanya hivyo atakuwa ni sawa na mhalifu na atafukuzwa mara moja,
-
Lazima wafaidi wetu washiriki kikamilifu shughuli zote zinazo andaliwa kituoni iwe ni za ndani au nje ya kituo bila pingamizi,
-
Lugha zinazo kubaliwa kuongelewa kituoni kwetu na katika misafara yetu ya kidaawa ni mbili tu kiswahili na kiarabu tu ila tukiwa na mgeni asiye fahamu moja ya lugha hizo mbili
ANGALIZO & USIPUUZE:
-
Kifungu chochote kinacho ashiria onyo katika muongozo huu basi sio onyo bali ni adhabu tu ya kufukuzwa bila mjadala wowote pindi tu uongozi unapo ridhika na mashitaka kwamba sio tuhuma tena kwa mhusika bali ni kosa lililo thibiti,
-
Viatu vyote viingizwe vyumbani wala sio mlangoni wala sio katika colidors,
-
Muongozo huu ni haki yako hivyo jitahidi uufahamu vilivyo na uwe nao popote ulipo.