top of page

TAFADHALI PITIA VIDEO HIZO UTAELEWA SABABU ZA MTAALA WETU KUWA KAMA ULIVYO ELEZEWA HAPO CHINI

VIDEO HIZI TUMEZIOKOTA MITANDAONI ... IKIWA NI MOJA YA VIELELEZO VYA CHANGAMOTO ZA KIDINI KATIKA JAMII

MUKHTASARI WA USOMESHAJI WETU

 

 

Asalaam alaikum wa rahmatuLLAH wa barakatuh.

Tunatarajia kuwa umepitia video zilioko hapo juu, pia huenda umewahi kuitembelea tovuti yetu hii kwa kuingilia lango kuu yaani ukurasa wetu wa mwanzo wa tovuti hii.

 

Kwa kipindi kikubwa sana tumekuwa tukitafuta ginsi gani nasi tuwe ni sehemu ya mabadiliko  na maendeleo ya dini ya Uislam popote tulipo. Sasa ukizingatia kuwa suala hilo ni moja ya malengo yetu, tuliathirika sana tulipo zitizama video hizo hapo juu na tukadhamiria kuanzisha program maalumu kwa lengo la Jaribio la ufumbuzi wa uchache wa maimamu na masheikh maeneo ya vijijini.

Hivyo sasa kuna haja kubwa sana ukaelewa usomeshaji wetu katika vituo vyetu pia kuelewa aina za wanafunzi tulio nao. kwanza kabisa tuna aina 3 za wanafunzi:

  1. maimam tarajiwa, wakusudia kushikilia uimam katika maeneo husika,,

  2. watu wazima, wazazi wanao tuzalia maimam tarajiwa,

  3. vijana wa mashulani... hawa ndio maimam na watu wazima tarajiwa

Mapito ya masomo tunayo somesha yanalengo kuhudumia masuala ya kitaaluma, kujitambua na kimalezi. kiukweli tafiti zaashiria kuwa waislamu wamegawanyika makundi mbili kuu:

Walio soma dini halafu elimu ya maendeleo wakaikosa, jambo linalo pelekea misikiti iliyo mingi kuwa ni tegemezi ya ufadhili badala ya kuanzisha miradi binafsi na kujifadhili,

Wasomi wa elimu ya mazingira wasio kuwa na utayari wa kujiendeleza upande wa elimu ya dini, wakiwa na shauku kubwa wawe ni wasimamizi wa kuu katika misikiti, jambo linalo anzisha migogoro misikitini maana hawasifa ya kuwa viongozi wakuu.

Yaliyo elezewa hapo juu yaashiria wazi chanzo cha mizozo misikitini, mizozo inayo hama kutoka misikitini hadi nje ya misikiti katika jamii. Huko ni kuto kujielewa kwa makundi tajwa hapo juu.

Hivyo huwa tunasomesha wanafunzi wetu tukiwa tunazingatia jambo hilo na kupita mapito yatakayo mfanya mwanafunzi wetu awe ni msomi wa dini aliye na uwezo wakuibua maendeleo katika eneo analo hudumu.

.

Hiyo ndio dira iliyo tusukuma kuchangua masomo yanayo someshwa kwa kipindi cha miaka sita kamili kabla ya ya kufikiria kumupeleka mwanafunzi wetu nje ya nchi. Hata hivyo usomeshaji wetu upo tofauti na utavyo fikiria wewe, maana tuliamua kuenda tofauti na madrassa nyenginezo kutokana na dira ya malengo tulio nayo.

​

Uchungu tulio nao sisi ni VIPI KUWAPATA MAIMAMU mapema iwezekanavyo na kuwapeleka huko vijijini wakahudumu wakiwa wao ndio maimu katika maeneo husika ikiwa ndio mtihani yao wa mwisho utakao tuhakikishia kuwa mwanafunzi wetu anao uwezo wa kusimamia dini na kuibua maendeleo katika eneo analo lihudumia. kinacho fuatia hapo ni kumpeleka nje ya nchi akasome elimu ya juu.

Njia za kuiendea dira ya malengo yetu ni kama ifuatayo:

   

          MAIMAMU TARAJIWA

​

Mwanafunzi wetu katika miaka 6 tunayo kaa naye darasani husomeshwa masomo yafuatayo:

1. Fiqhu         

2. Aqiida     

3. Sirah          

4. tafsiri  ya 30       

5. Nahwu      

6. Sarfu                       

7. mustalahul hadith    

8. Sherhu nudhumil waraqaati      

9. Malengo na ufanisi wake

10. Ahkamut tajuidi   

11. Saikolojia ya watoto  na malezi     

12. turukutadriisul quraan

13. Umeme wa majumbani,

14. Ufundi wa charahani,

15. Tehama. 

 

Miezi 2 ya kwanza wanafunzi wetu husomeshwa kujua kusoma na kuandika herufi za kiarabu kwa umakini pamoja na kumtanabahisha baadhi ya mambo kadhaa ya kasoro za kimaandishi zilizomo katika JUZUU inayo tumiwa katika maeneo mengi nchini Tanzania.

Miezi 3 inayo fuatia wanafunzi wetu hufundi usomaji wa quraan na hadithi wakiwa wapewa maana ya kila neno moja moja kwa lengo la kumuandaa kumakinika na lugha ya kiarabu hapo baadae. Anapo kamilisha mwanafunzi wetu miezi mine kamili huwa tunamuanzisha kuongea mbele za watu msikitini.

Baada ya miezi hiyo mitano huwa tunawafundisha wanafunzi wetu masuala ya kinahau yaliomo katika kila sura wanazo zisoma kiasi cha kumfanya mwanafunzi kuwa na uwezo wa kinahau unaolingana na sura zote alizo zisoma. Pia ni katika kipindi hicho hicho ndio husomeshwa hadithi na aqida kwa mtindo huo huo wa kuyasoma masuala ya kinahau na kisarfu katika vitabu hisika vya hadith na aqiida.

Baada ya mwanafunzi wetu kukamilisha miezi 9 au kumi basi huanza kusomeshwa na suala ya kijasiriamali na uongozi bora katika jamii. Jaribio letu la kwanza tuliwachukuwa wanafunzi wa tano kutoka mkoa wa lindi huko vijijini.

Usomaji wa kila siku kituoni kwatu ni kama ufuatao:

Saa 10 hadi sala ya alfajiri ni kujisomea quraan kila mmoja kivyake,

Baada ya sala ya alfajiri hadi saa 2 tumo barasani na mwalimu,

Saa 2 hadi saa 3 tuna shughuli za usafi wa mazingira ya madrassah,

Saa 3 baada ya kunywa uji hadi saa 5 tumo darasani na mwalimu,

Saa 5 hadii sala ya adhuhuri ni muda wa kazi binafsi au mapumziko,

Saa7 na robo hadi saa 9 na nusu kailuula

Baada ya sala ya laasiri hadi 11:30 tumo darasani na mwalimu,

Saa 11 na nusu hadi saa 12 na robo mapumziko,

Baada ya sala ya magharibi hadi saa 1 na 45 kujisomea quraan,

Saa 1 na 45 hadi saa 2 ni wakati wa sala ya ishaa  na maandalizi yake,

Saa 2 hadi saa 3 ni mapumziko na kula,

Saa 3 hadi saa 5 tumo darasani na mwalimu,

Saa 5 hadi saa 10 alfajiri ni kulala

​

Tafadhali ewe msomaji, huenda tulio yaandika hapo juu yakakuchangaza maana sio katika yalio zoeleka na walio wengi katika tasnia ya taaluma madrasa. Kiukweli ni kwamba tunazo sababu tulizo ziona kuwa za msingi zilizo tushawishi kuchagua miondoko iliopo hapo juu. Baadhi ya sababu zenyewe ni kama zifutazo:

  1.  kuepuka mazoea,

  2. dhamira na utashi wa mabadiliko,

  3. Utatuzi wa ukosefu wa maimamu maeneo ya vijijini,

  4. kuwaendeleza kwa muda mfupi uwezekanao walio kosa fursa ya maaluma ya dini.

  5. ujasiriamali na ufundi stadi kwa lengo la kuboresha hali ya kiuchumi kwa maustadh

         

Hivyo isiwe ni ajabu kwako wewe kuona tuna miondoko ya tofauti na ulivyo zoea wewe kuona. Sisi tunaamini kuwa kila kituo huanzishwa kwa sababu maalumu, ni vema kutambua kuwa na sisi tunazo sababu zisizo fanana au pengine zisizo lingana na sababu zilizo pelekea kuanzishwa vituo vinginevyo. 

 

Pia hatukosi kukushauri wewe msomaji wa makala haya, kuwa kunahaja kubwa na wewe ukazisoma changamoto zilizomo katika jamii upande wa tasnia ya taaluma ya dini ya Uislam, halafu ukachangua njia maalumu ya kukabiliana na changamoto hizo. Ukiwa makini na dhamira ya kuzitatua changamoto husika bila shaka utajikuta na wewe umeondoka tofauti ikiwa sio kinyume na walio kutangulia. Vyenginevyo utakuwa huku lenga kutatua changamoto zilizo kuwa zimekosa utatuzi.

 

Huo ndio mukhtasari wa mtaala tunao utumia kituoni kwetu kwa sasa hivi, mtaala ambao unaweza kubadilishwa baada ya muda fulani kwa kulingana na namna ya muelekeo wa changamoto utavyo kuwa kwa wakati huo.   

 

          WATOTO WA SHULE

​

Upanda wa watoto wa madrasa tuna changamoto kubwa sana maana kila kukicha ndio ratiba za shule zaongezeka na kuwafanya Watoto wasipatikane madrasa. Wazazi walio wengi hawakupitia elimu ya dini na kwa bahati mbaya pia wapo mbali na masuala ya maendeleo yao kiroho na kiimani.

Hivyo hatuwazi kutarajia wazazi hao kuwa kuwa ndio wanaweza kuwa na dhamira ya utatuzi wa changamoto zinazo tukabili katika kuyaendea masuala ya dini na madrasa. Lengo la madrasa ni kurithisha imaani ya dhamira ya kiroho kwa waumini. Sasa kadri tunavyo wakosa Watoto kuhudhuria madrasa ni wazi kuwa kwa siku za usoni tuzidi kupungukiwa na fursa ya kuwapata masheikh na maustadh watakao rithi kazi ya kuismamia dini.

Katika kuliepuka hilo, tumeamua kubadili ratiba rasmi ya kuingia madrasa. Ratiba hiyo ni kwamba watotot washule wote bila ya khiyari kuanzia likizo ya muhula wa kwanza mwaka huu 2023, wote watatoka madrasa baada ya sala ya Ishaa. Maana darasa la baina ya sala ya magharibi na sala ya Ishaa ndilo linalotumiwa katika kutua elimu ya dini kimatendo. Nyakati zisizo kuwa wakati tajwa, hutumika kwa ajili ya kusomesha kisoma cha qur’aan.  Baada ya ramadhani mwaka huu 2023 wanafunzi wa darasa la 3 na la 4 bila khiyari watakuwa wanabaki dakika 75 baada ya sala ya Ishaa kwa lengo la kuwasimamia masomo yao ya Hisabati, Kiingereza na Sayansi kwa wiki nzima isipo kuwa Ijumaa.

Mzazi yeyote ataye kuwa pingamizi kwa ratiba iliyopo hapo juu, atakuwa amedhihirisha wazi kuwa hana lengo mwanawe kuwa mrithi wa kuismamia dini kwa siku za usoni. Hata hivyo hatuto mfunkuza mwanafunzi husika ila tutawatenga wanafunzi wanao endana na mpango wa madrasa watakuwa mbali na wasio endana na mpango kazi wetu. Ama mwanafunzi yeyote mpya hatumchukui mpaka mzazi wake akubali mwanawe kuendana na ratiba hiyo mpya. Vyenginevyo hatumchukui kabisa.

Mapito ya masomo wanayo yasoma Watoto wa shule madrasani kwetu hutoka katika mikondo ya masomo yafuatayo:

1.Tilawatul quraan

2. Fiqhu

3. Aqiida

4. Sirah

5. Maarifa ya jamii na muamala kwa wasio kuwa waislam

6. Hisabati, Kiingereza na Sayansi.

​

Tafadhali pitia video hizo hapo huenda ukaelewa sababu zilizo tusukuma kufanya mabadiliko na kulazimika kuyasimamia mabadiliko husika kimatendo na kiutekelezaji.

​

​

​

​

​

​

​

​

​

​

​

​

​

​

HOME PAGE.png

          WATU WAZIMA

 

Kama tulivyo ashiria huko juu kuwa hatutumii juzuu iliyo zoeleka madrasah pia upande wa watu wazima kike na kiume na Watoto pia huwa tunatumia juzuu yetu wenyewe tulio ianzisha ssis inayohudumia malengo ya kitaaluma tulionayo sisi.

Miondoko ya usomeshwaji upande wa watu wazima haukutofautiana sana na mfumo unaotumika kwa vajina wa shule. Mambo ya ziada kwa watu wazima ni kuwasomesha mbinu za ulinganiaji wa dini maana ni lazima mwanafunzi wetu kufanya zoezi la kuitangaza dini katika kipindi chote atacho soma kwetu, ujasiriamali na ndoa imara ya misingi ya dini.

Mapito ya masomo wanayo yasoma Watu wazima madrasani kwetu hutoka katika mikondo ya masomo yafuatayo:

1.Tilawatul quraan

2. Fiqhu

3. Aqiida

4. Sirah

5. Maarifa ya jamii na muamala kwa wasio kuwa waislam

6. Tehama

7. Malengo na ufanisi wake

8. Ahkamut tajuidi   

9. Saikolojia ya watoto  na malezi     

10. Ufundi wa charahani.

​

Katika jaribio la utekelezaji wa mtaala wetu tulipata fursa ya kutumia :

  1. masjidu fatma ulioko shangani mji mkongwe Unguja zanzibar,

  2. Ladies first hostel Tunguu Zanzibar University

  3. msikiti uitwao Madinatul Munawarah uliopo wilaya ya Ubungo kata ya kwembe mtaa wa mloganzila kitongoji cha kazamoyo zoni 6, Chama road, Mende street No 155. kama unavyo onekana katika clip hapo chini.

  4. madrasatun Nuurul Mutaqiina iliyoko goba mpakani Upendo street. kama unavyo onekana katika clip hapo chini.

BOFYA PICHA 
USOME KANUNI NA MUONGOZO KWA WANAFUNZI
KUSHOTONI HAPO NI MOJA YA JUHUDI ZA UKARABATI WA KITUO
KULIANI HAPO NI SIKU YA KIKAO CHA KWANZA BAINA YETU NA WAMILIKI WA MADRASAH NA WAZAZI WA WANAFUNZI HUKO GOBA MPAKANI. 

Tafadhali tunaomba maoni yako kuhusu makala hii

bottom of page