top of page

TUTAMBUE KUTOKA KWETU WENYEWE

LENGO:

Lengo letu ni kurejesha jamii khasa vijana, katika mkondo sahihi wa maadili tukizingatia uhuru wa imani ya dini kwa wafaidi wetu, huku tukiwazawadia faani tafauti ili wasiwe tegemezi bali wawe ni tegemeo la jamii kwa siku za usoni.

 

DIRA:

Dira tulionayo ni kuhakikisha vijana wote wamepata fursa ya kuandaliwa kimaadili  na kitaaluma kiasi cha kuwafanya wayapende majukumu yao kwa jamii yao ya walimwengu kwa jumla. Tuniwa sisi ndio sababu... na moja ya yaasisi bora nchini miongoni mwa taasisi zinazo ihudumia jamii katika nyanza ya ustawi.

KAULI MBIU:

Kauli mbiu maisha ni hadith ... kuwa hadith nzuri kwa watakao simuliwa habari zako maana kuzaliwa ni mara moja na kufariki dunia ni mara moja pia.

 

 

UTAGULIZI

      Shukran zote ni zake ALLAH MUUMBA wa mbingu na dunia  na vilivyomo. Rahma na amani ziwaendee mitume wote,na salaama juu ya mtume MUHAMMAD na watu wa nyumbani kwake na masahaba wake na watu wote watakao amua kuwafuata na kuwaiga katika mambo ya kheri na wema.

HISTORIA YETU

Mnamo miaka ya 1985 karne iliopita tulishawishika kuwa na fikra ya kuanzisha chombo kwa ajili ya kuwaendeleza vijana ili wazifikia ndoto zao. Fikra hii ilitujia tukiwa ni kundi la vijana 4 tulio kuwa tunashirikishwa katika harakati mbali mbali kwa ajili ya ustawi wa vijana, lakin kwa bahati walio kuwa wakitushirikisha walikuwa hawana malengo halisi kwa siku za usoni jambo lililo wapelekea kutuwacha bila tija yoyote.

Baada ya kuvunjika moyo, wenzangu waliamua kuachana na harakati, mimi nikaendelea na kuhamasika kuijenga NDOTO ya kuasisi taasisi maalumu kwa ajili ya kuwasaidia vijana kuzifikia ndoto zao za maisha.

Kwa miaka hio nilikuwa sina elimu, kiasi taswira ya taasisi ilikuwa haikukaa vilivyo kichwani mwangu.

Mnamo miaka ya 1988 nilibahatika kukutana na kasisi mchungaji fulani aliyeamua kuyahama "maisha ya utawa" na kurudi katika jamii ya waumini wa kawaida , kwa kipindi hicho nilipo kutana naye alikuwa ameoa, kwa bahati miaka ya nyuma kabla ya hapo mkewe aliwahi kufaidika na juhudi za hakarati zangu. Mke huyo ndiye aliye nikutanisha na kasisi mchungaji husika, nikabahatika kupongezwa na kasisi huyo na kupata bahati ya kuendelezwa kifikra na kupewa nasaha zitakazo nisaidia kuifikia ndoto ya maisha yangu.

Mnamo miaka ya 2013 nikiwa mwanafunzi wa shahada ya diploma ya maandalizi(post graduate) ya shahada ya pili katika kitivo cha MANAGEMENT chuo kikuu cha International University Of Africa jijini Khartoum nchini Sudan  nilibahatika kuitwa na mkuu wa chuo hicho baada yake kupata habari za harakati za kujitolea kwangu katika kuwaendeleza kimasomo baadahi ya wanafunzi wapya na baadhi ya wengine miongoni mwa wakongwe wanaohitaji kusaidiwa. Fursa hiyo niliitumia kumuonesha PLAN ya harakati zangu, nikabahatika kusamehewa  ada ya chuo ikiwa ndio malipo ya shahada ya pili ( REJEA katika ofisi ya mkuu wa chuo hicho International Univesity of Africa: ( عمومي رقم الملف 6 & رقم الملف 186 في شهر مارس 2014.

UONGOZI NA UTAWALA

مؤسسة الرحمن  ni taasisi tawi la mambo ya kidini inayo milikiwa na taasisi ya GLOBAL SERVICES HIGH TARGETS yenye usajili wa jina serikalini brela nambari 4650666. Hivyo مؤسسة الرحمن inao uongozi wake chini ya katibu anaye ripoti kila mwaka kwa mmiliki wake ambaye ni GLOBAL SERVICES HIGH TARGETS .

SABABU ZA KUANZISHA HARAKATI

Kama tunavyo elewa kuwa kila jambo lina sababu zake , hali kadhalika harakati hizi zinavyo visababishi visivyo pungua vitatu.  Lau niliyo yabainisha hapo juu yatakuwa yameeleweka , basi utabaini kuwa sababu kuu zilizo pelekea kuwa na fikra ya kuanzisha taasisi. Moja ya sababu  hizo ni hali linio ielezea hapo juu kuwa nimewahi kuwa mhanga wa kutelekezwa na watu fulani nilio waashiria hapo juu  kuwa waliwahi kutushirikisha katika harakati halafu wakatuachia njiani. Hali kadhalika zipo sababu nyenginezo zilijitokeza katika mazingira nilio kuwa nikiishi kila miaka ilivyo kuwa ikisonga mbele na kunifanya kujenga taswira upya ya uhalisia wa ndoto yangu ya maisha.

LENGO LA KUANZISHA HARAKATI

Kutokana na changamoto kadhaa zinazo wapata vijana ambao wao ndio tegemeo la jamii kwa siku za usoni tumedhamiria kudurusu sababu za kila changamoto tulizo kumbana nazo maishani ili  kuzipatia ufumbuzi kwa kadri tutavyo wezeshwa na ALLAH.

Baada ya uamuzi na kukita katika kuihudumia jamii, tumelenga yafuatayo:

  1. Kuwajenga vijana dhamira ya uzalendo na kufanya sana juhudi za kujitolea katika kuyaleta maendeleo katika jamii wanako ishi wao. Hii ni baada ya kuwaona wahitimu wengi wa vyuo vikuu kugeuka kuwa ni tegemezi na mzigo kwa jamii badala ya wao kuwa ndio tegemewa na watatuzi wa matatizo ya jamii kwa kutumia elimu yao, bali wengi wao hushawishiwa na fikra za kuhama nchi punde tu wanapo hitimu elimu vyuoni kisa wanataka kuepuka tatizo la kuwa tegemezi, lilio wapata walio tangulia kuhitimu,

  2. Kuwazawadia wanajamii, elimu ya ujasiriamali ili wapate kuzitumia nyezo wanazo zimiliki na uwezo wao wa kitaaluma kwa ajili ya kujiletea maendeleo katika kaya zao wenyewe. Hii ni baada ya kubaini kwamba raia wengi wameishi katika umaskini wa kupindukia kutokana na ukosefu wa maarifa sahihi ya kuzijua nyezo halisi za kutumia katika kujiendeleza kimapato.

  3. Kuendeleza na kusomesha elimu ya dini na faani za kisasa za kusomeshea kwa wafaidi (waalimu wa madrasa na vituo vya elimu ya dini) wa program za taasisi yetu tukiwa na dira tatu kuhusu taaluma ya elimu ya dini:

    • Kuoanisha shughuli za ujasiriamali na uaminifu (amana) kwa wanajamii maana mjasiriamali akipoteza amana ,hali hiyo huwa ni sababu tosha yeye kuwa ni mlaghai katika huduma zake kwa wanajamii,

    • Kulenga mabadiliko katika uendeshaji wa vyuo vya kusomesha quraan kwa njia za kitaalamu, tukiwa mbioni kupata suluhu kwa tatizo la ulawiti wa wavijana katika vituo vya kufundishia quaan, maana imetokea kutuhumiwa waalimu kadhaa kujihusisha ya unyama huo kwa njia moja ama nyengine , bali imebainika kuwa baadhi yao ndio watendaji wa kubwa wa vitendo hivyo,

    • Kupata aina nyengine mpya ya walinganiaji wa dini kinyume na ilivyo hivi sasa miaka hii ya 1998 na kwenda mbele, maana majengo ya  ibada badala ya kutumiwa kwa lengo la kuelekeza waumini na kuhubiri amani yamekuwa yatumiwa majengo hayo kuhubiri chuki baina ya watu. Jambo linalo weza kuwa ni sababu ya uvunjifu wa amani,

  4. Kutoa maelekezo kwa wanafunzi wa kitanzania na wengineo waliopo ndani na nje ya nchi ili wapate kuziepuka changamoto zilizoko katika vyuo vikuu, changamoto ambozo zinaweza kuwapelekea kujiingiza matatizoni dhidi ya jamii zao waliko zaliwa. Hii ni baada ya kushuhudia kwa macho baadhi ya matukio kama hayo, pia kusikia kuwa  baadhi ya vijana hutumiwa vibaya na makundi tofauti ya watu, au watu binafsi kwa lengo la kujiimarisha wao kimalengo,

  5. Kuwaendeleza walio poteza fursa zao za masomo ... kwa kuwakusanya na kuwaandaa upya ili warejee tena mitihani yao ya taifa ao kuwafundisha kazi za mikono (ufundi stadi) na shughuli za kiujasiriamali kwa lengo la kuwaepusha na maisha tegemezi kwa wakati huo huo watakuwa na uwezo wa kuleta maendeleo katika kaya zao na maeneo wanako ishi wao.

  6.  Jambo lolote lengine litakalo kuwa na uhusiano  wa mbali au wa karibu na suala zima la ustawi wa jamii, kuweka imara misingi ya harakati za kujitolea kuwaendeleza wanajamii, katika mambo yanayo zuka katika maisha ya kawaida, mfano wa unajisi na ulawiti wa watoto katika maeneo tofauti nchini na nchi jirani.

NEMBO YETU

Nembo tunayo itumia ni hiyo iliopo  juu mwanzoni mwa tovuti hii, pia tunatarajia kuanzisha nembo ndogo ndogo zitazo kuwa chini ya nembo hiyo mama,zikiwa hizo nembo ndogo ni ishara za miradi (taasisi ndogo ndogo) tofauti zilizopo chini ya taasisi yetu, miradi itakayo anzishwa na kuamuliwa kuwa ni endelevu kwa ajili ya kukabiliana na changamoto mpya zinazo jitokeza katika jamii. Miradi hiyo ndio itakayo tafutiwa nembo zake maalumu kama tulivyo elezea hapo juu katika kipengele hiki cha nembo.

MAKAO MA KUU YETU

Kutokana na changamoto za kila leo zinazo zikabili taasisi nyingi duniani, hali kadhalika tumekuwa tunakabiliwa na changamoto za kifedha kwa ajili ya kukimu na kukabiliana na matatizo ya shughuli za kiuendeshaji katika taasisi yetu. Hadi hivi leo hatumiliki jengo lolote wala ardhi kwa ajili ya kuendeshea shughuli zetu zaidi ya kuazimwa eneo mkoani Dar es Salaam, wilaya ya ubungo kata ya Kwembe  mtaa wa Mloganzila (kibamba).. Tayari tumekamilisha taratibu za usajili wa jina la taasisi serikalini (BRELA ID No: 465066 hapo juu) tokea mwaka wa 2020.

VYANZO VYA MAPATO

Sisi ni taasisi ya kujitolea yaani hadi leo hii hakuna yeyote tuliye wahi kumtoza ada ya huduma au mafunzo tunayo yatoa kwa wanajamii, hata hivyo kwa siku za baadae tunatarajia kuwa na miradi ya kuingiza mapato ili kumudu gharama ya uendeshaji wa shughuli zetu. Hii ni baada ya kukabiliana na tatizo la ukosefu wa uhisani na ufadhili kwa program zetu.

Katika kupunguza gharama za kuendesha program zetu kwa wanajamii na kuepuka changamoto za kuifanya taasisi yetu kuwa ya maneno matupu bila ya matendo, huwa tunawaomba wakufunzwa, kila mmoja wao ajigharimie vitendea kazi vyote na nyenzo nyenginezo atakazo  zihitaji na kuzitumia kwa ajili ya mafunzo husika, yaani tunacho kifanya sisi katika huduma zetu kwa wanajamii ni kutoa elimu  bila ya malipo wala gharama yoyote kutoka kwa mfaidi kuja kwetu, kwa sharti mfaidi ahimili majukumu mengine yalio baki ili zoezi la mafunzo likamilike (gharama za kula, kulala, usafiri na vitendea kazi vyote ... ni juu yake mfaidi wa huduma zetu sisi tunacho kiandaa ni wakufunzi na sehemu ya kufanyia mafunzo).

Pamoja na lengo la kuja kuanzisha miradi ya kuingiza mapato, basi itabaki kuwa 80 % ya shughuli na huduma zetu kwa wanajamii ni za kitaaluma kwa lengo la kuwazadia wanajamii ala ya kuendeshea shughuli za kimaendeleo katika maeneo wanakoishi, na mafunzo hayo yatakuwa yatolewa bila ya malipo, hali kadhalika 20%  zilizo baki katiaka huduma zetu kwa wanajamii, itakuwa ni vitega uchumi vyetu kwa ajili ya kuziendeleza program  zetu, hivyo hivyo huduma hizo zitatolewa kwa gharama nafuu, unafuu utakao fikia kiwango cha 80 % ya huduma kama hizo ukilinganisha hali nzima ya soko la huduma hukika.

“ GLOBAL SERVICES HIGH TARGETS ” NI NINI ?

     Sisi ni taasisi ya mafunzo ya kiujasiriamali na kuwaendeleza waalimu wa mashuleni katika kukuza vipaji vyao kazini, kuziendeleza madrassah  pia tunahudumu katika tafiti za kijamii kwa ustawi wa jamii ya kiislamu na jamii nyenginezo katika maeleo wanako ishi waislamu ( leadership & entrepreneurship within volunteering services ), ikiwemo elimu ya dini kwa vijana na watoto. Huduma ya elimu ya dini inasimamiwa na kitengo kiitwacho " مؤسسة الرحمن ". Tumekuwa tunahudumu hapa nchini Tanzania visiwani Zanzibar tokea mwaka 2015.  Tumeanza fikra ya taasisi tokea mwaka 1989 karne ilio pita bahati mnamo mwaka 2010 tukaibuka moja ya jumuiya zilizo wahudumia jamii ya wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 80 duniani, chuoni  International University Of Africa nchini Sudan nakupata fursa ya kutekeleza jukumu la kuitanganza Tanzania kwa wageni.   Tukitambulika kwa jina la "Global Services High Court"  au  " مؤسسة الرحمن "lakin hivi sasa tunatambulika rasmi kwa jina la  "Global Services High Targets"  au  " مؤسسة الرحمن baada ya usajili rasmi wa jina la taasisi yetu mwaka huu 2020.

     Ama kwa hapa nchini tokea mwaka 1998 tulikuwa tunahudumu katika makundi ya vijana wa madrasa  katika maeneo tofauti kisiwani Unguja. Mnamo mwaka 2015 tuliamua kuanzisha huduma za moja kwa moja  kwa watu wa kawaida, kwanza kwa lengo la kuwazawadia silaha za kuendeshea maisha kiuchumi, na tukabahatika kutekeleza yafuatayo:

  1. Elimu ya dini mashuleni kwa kujitolea, tokea mwaka 2018 dodoma mjini na mwaka 2019 mkoani Dar es Salaam katika wilaya ya Ubungo kata ya kibamba katika shule zaidi ya 5, bali suala la usomeshaji wa dini mashuleni tumedhamiria liwe endelevu kadri atakavyo tuwezesha ALLAH .

  2. Semina za kielimu zisizo pungua 13 kwa walimu wa dini kwa lengo la kuwazawadia wahusika ala na nyenzo walizokosewa katika shughuli zao za kusomesha,

  3. Courses kadhaa za ujasiriamali kwa wajane na wanafunzi walio kosa nafasi ya kuendelea baada ya mitihani yao ya kidato cha nne,

  4. Teknohama kwa wajasiriamali na waalimu wa dini;

 halafu kabla ya hapo, mwishoni mwa mwaka 2017 tuliamua kutanua nyanja za uhudumu wetu kwa jamii kwa kuwalenga wasomi chipikuzi visiwani. Katika program  hiyo ya wasomi chipukizi:

  • tumesha zunguuka tukitoa mada tofauti kwa wanafunzi wote kwa pamoja (Assembly), katika shule za sekondari za serikali nchini Tanzania visiwani Zanzibar kwa 80 % katika zoni(area) za mjini mkoa ya Mjini magharibi kwa kushirikiana na jumuiya za wanafunzi na waalimu wakuu mashuleni.                                        https://www.youtube.com/watch?v=kx8LL1ltzkY&list=PLjgeP-MpIkz8VcUf6RMUbC8roK0eY22_A

  • kusomesha tuition ya MASOMO YOTE YA SAYANSI bila ya malipo kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya kibele kuanzia mwaka huu 2018 ikiwa ni jaribio la kutafuta sababu zinazo pelekea hadi wakati huo 2017 matokeo ya masomo ya sayansi kuwa ni sifuri tokea kuanzishwa kwa skuli hiyo. Haitoshi ... bali tumekuwa tukiwatembelea waathiriwa wa madawa ya kulevya katika vituo vyao

      https://www.youtube.com/watch?v=j8tv9PC0V9c&list=PLjgeP-MpIkz8xjCTAafz9VpTQEd9_wT0c

  • Vyuo vikuu :

    1. tumebahatika kushirikiana na jumuiya ya wanafunzi wa chuo kikuu cha taifa la Zanzibar SUZA Tunguu Campus, hadi hivi sasa tumebahatika kutekeleza vikao vitatu mada tofauti:

      • Ubaguzi na athari zake mbaya katika jamii ya wasomi,

      • Umuhimu wa “muingiliano” na namna sahihi ya kuamiliana baina ya watu wenye dini na mirengo tofauti katika vituo vya elimu (universities),

      • Elimu – maana yake, makusudio yake, na athari zake katika jamii ya wanaadamu.

    2. Zanzibar university, semina kwa wanafunzi “ LEADERSHIP & ENTREPENEURSHIP “

  1. Mchango na msaada wa malazi (Umulkhairi Hostel - Unguja, Zanzibar) kwa wanafunzi wa  Universities wasio puangu 20 ( wakiwa wao ndio walengwa nambari moja wa program zetu maana wao ndio tegemeo letu na jamii kwa ajili yaharakati za mabadiliko katika jamii yoyote duniani ), kwa sharti wawe tarari kuihudumia jamii kupitia program zetu na kufuata kanuni na miongozo ya nchi kuazia serikali zao za mitaa hadi ngazi ya serikali kuu nchini. Vyenginevyo hatumchukui kabisa jambo lililo tupelekea kuwalaza watu watatu pekea yao waliotimiza masharti na walio weza kutuletea barua kutoka kwa masheha wa shehia (serikali ya mtaa) wanako ishi wao, wengine tulilazimika kuto kuwachukua kutokana na wao kutokuwa na barua kutoka kwa masheha (serikali ya mtaa) wao pamoja na kwamba walikuwa tayari kwa masharti mengine yaliyo baki.

  2. Muswada kwa ZBC (Zanzibar Broadcast Coorporation) ikiwa ni huduma tunayo jitolea bila sis kudai malipo, kupewa kipindi maalumu endelevu kwa lengo la sisi kutoa mchango wetu katika kiijenga jamii na kuwahamasisha raia kuwa na dhamira ya uzalendo na kuijenga nchi yao kupitia maendeleo watakayo yaibua katika maeneo wanakoishi wao,

  3. Muswada wa kuwabadilisha wahalifu walioko jela kwa kipindi hicho (wanafunzi wa chuo cha mafunzo) Zanzibar, kuwaandaa upya kwa lengo la kuwafanya wawe ni raia wema na bora na wajenzi wa uchumi nchini ikiwa hio ni mchango kwetu kwa taifa letu, rejea barua katika moja ya ofisi zetu ( barua tumeambatanisha).

  4. Mafunzo kwa waalimu wa shule ya jeshi  Nyuki secondary school (August 2018) iliyoko mwanakwerekwe, mkoa wa mjini magharib, Unguja Zanzibar

  5. Mnamo mwaka 2018 tuliendesha mafunzo ya faani za UALIMU wa shule  kwa waalimu wa madrasatul istiqaamah kijichi mchangani tukiwa na lengo la kukuza vipaji na kufanya utendaji wao kuwa wa kiwango kinacho lingana na viwango vya shule kama ya Lumumba kisiwani Unguja, Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Fidel Castro kisiwani pemba,Umbwe mkoani moshi ... Nk. kuujua undani wa shughuli zetu tendelea channel yetu kwa kubofya hapo chini tafadhali .

https://www.youtube.com/channel/UCGclt7usg0RkEmrAhUUW6Pg

MAFUNZO TUNAYO YATOA KWA WANAJAMII

MAMA MZAZI AKIHATARISHA MAISHA YA MWANAWE KATIKA JARIBIO LA KUTAFUTA UNAFUU WA MAISHA

     Hakika suala la ustawi wa jamii limekuwa ni gumzo duniani kwote ( video hapo juu ni ushahidi tosha ) na ndilo sababu ya kipekee inayo wapelekea watu maelfu kwa maelfu kuzihama nchi zao na kukimblilia ughaibuni, kiasi wengi wao kuwa tayari kuhatarisha maisha yao.

Kwa haraka haraka nimeashiria kwamba suala la kuogopa madhara ya umaskini ndilo linalo wapelekea watu wengi kujikuta wanazama kama sisimizi katika bahari ya mediterania au kwa uchache kujihusisha na njia haramu za kutaka kujiengezea kipato.

Lakin tathmini tofauti za ashiria kwamba 95 % ya wahamiaji wanao elekea nchi za wazungu hujikuta katika maisha duni kuliko maisha yao ya hato awali kabla ya kuzihama nchi zao  kutokana na changamoto zinazo wakabili tunde tu wanapo nyanyua mguu kwa ajili ya hatua ya kwanza ya safari yao ya uhamiaji (kwa wanao bahatika kufika safari hiyo) hadi siku ya wao kuamua kurudi nchi zao za asili.

Bali baadhi yao hurejeshwa kutoka ughaibuni wakiwa ni wagonjwa au wakiwa hawafai tena katika shughuli za kujenga uchumi wa KAYA zao, si kuambii ngazi ya taifa. Hali hii pia ni changamoto kubwa kwa nchi za asili za wahamiajia hao. Kama leo kuna umasikini wa kupindukia katika nchi zinazo endelea, basi chanzo chake kikubwa ni ukosefu wa maarifa, hata kwa vijana wengi walio hitimu elimu za vyuo vikuu katika nchi nyingi za kusini mwa dunia.

Kumbe sasa kuna haja kubwa ya kukita katika huduma za kitaaluma kwa ajili ya kueneza maarifa sahihi ya maana ya UMASKINI na vyanzo vyake au maana sahihi ya MAENDELEO na vyanzo vyake, maana hata huko wanako kimbilia wahamiaji, pia umaskini upo.  Yaani ukosefu wa maandeleo unaweza kuibuka na kushamiri iwapo wakaazi wa huko watapuuza kutafuta kuelewa vyanzo na sababu za umaskini au maendeleo.

Hivyo katika kulitatuwa tatizo la wimbi la wahamiaji haramu kwa dhana potofu za madai ya kuyafatia maendeleo, huwa tunatoa mafunzo katika Nyanja za UJASIRIAMALI NA LEADERSHIP ili kuwapata watu watakao kuwa tayari kueneza utamaduni wa UZALENDO baina ya raia wenziwao na kuhimizana kuwa na dhamira za kujitolea kwa ajili ya maendeleo yao. Mafunzo yenyewe ni katika courses zifuatazo:

  1. Elimu ya madrassah na elimu ya dini mashuleni

  2. Misingi na chimbuko la ujasiriamali,

  3. Masomo ya elimu ya uendeshaji,

  4. Leadership,

  5. Faani za ualimu (kwa walimu wa vyuo vya quraan),

  6. Teknohama,

  7. umeme,

  8. Soma la misingi na mbinu za utafiti,

  9. Masomo ya dini,

  10. Kuandaa mahafali ya wahitimu 

  11. Kuhuwisha miskiti na madrasa ziliyo telekezwa au zinayo karibia kufa,

  12. Seminars kwa ajili ya kukidhi haja maalumu za kijamii…Nk.

Kuelekea ustawi halisi wa jamii yetu tutapitia awamu nne tulizo ziainisha kama ifutavyo:

  • Awamu ya maandalizi ikiwa na lengo la kuiandaa jamii ili iwe tayari kuyapokea mabadiliko,

  • Awamu ya kuwakinaisha “ watu vinara ” na wanao iendesha jamii na viongozi,

  • Awamu ya kupewa majukumu (vikundi, taasisi na watu, mmoja mmoja kwa mjibu wa ushawishi wake katika jamii)

  • Awamu ya masahihisho ya utendaji katika safari yetu ya kuyaelekea mabadiliko halisi ya ustawi wa jamii yetu.

Tafadhali tunaomba maoni yako kuhusu makala hii

bottom of page