top of page

LADIES FIRST - PROGRAMS CORNER FOR PRE AND UNIVERSITIES STUDENTS

Updated: Mar 9, 2022

Hii ni corner maalumu kwa ajili ya vijana chipukizi, vijana tegemeo la jamii ya uislam duniani pote. Hivyo mara kwa mara tutakuwa na jadili masuala ya maendeleo na vikwazo vyake kwa vijana wa kiislam bila kupuuza changamoto wanazo zikabili katika kuyaelekea maendeleo yao au katika utekelezaji kivitendo vya walio yapata katika vituo mbali mbali vya kielimu.




International University of Africa - Khartoum, Sudan (computer networking).


Mapema mwaka 2010 sisi GLOBAL SERVICES HIGH TARGETS tulianua kuvunja ukima na kudhihirisha ndoto yetu kwa wanajamii. Punde tu baada ya kubaini kuwa jukumu haliwezi kukimbiwa tuliamua kutafasiri ndoto kuwa matendo. Hilo hapo juu ni kundi la wanafunzi wa kike chuoni International University of Africa - Khartoum, nchini Sudan. Vijana hao wa kike wanao oanekana hapo katika video hiyo ni wanafunzi kutoka vitivo vinavyo husisha kozi za sayansi ya kombuita tofauti chuoni hapo ( pure science, engineering, computer studies ). Tuliamua kutoa mafunzo hayo ya bila malipo kwa nia ya kunusuru mamia ya dola za kimarekani zinazo gharimiwa mara kwa mara na wanafunzi katika kujiendeleza na kozi za nje ya mtaala na kudiriki vitu vipya vinavyo vinavyo ibuka kitaaluma kutokana na tafiti za kila leo katika masuala ya kombuita.


Mwito wetu kwa masheikh na maustadh ni Kwamba katika harakati zetu za kidini za kila leo, tusisahau mamia ya wanafunzi wakike waislamu walioko mashuleni na vyuoni, kuna haja kubwa ya kukaa nao kwa pamoja tutizame ni jinsi gani tunaweza kupambana na changamoto zinazo wakabili kitaaluma, kiimani, kijamii na kiuchumi .


MWANAMKE MUISLAMU NA CHANGAMOTO ZINAZO MKABILI.


Suala ya kujikwamua ni suala la kufa na kupona kwa viumbe wa aina zote walio hai, maana tabia ya viumbe kuvutiwa mnoo na mambo ya kuwepesisha uweko wao hai. sasa mwanamke akiwa ni mmoja wa viumbe walio hai, hana budi na yeye pia, ila atamani kunasuka katika nyanza zote za maisha.

Suala la kujikomboa na kujinasua kimaisha, huwa la hukumuwa na juhudi za hapa na pale ili kulifikia lengo husika. Moja ya juhudi muhimu za kujinasua ni suala zima la kuitafuta elimu au maarifa.

Sasa katika makala hii tutanurika mwanga juhudi za mwanawake wakiislam katika mbio zake za kuyaendea maendeleo hadi kujinasua.


Kwanza kabisa mwanamke ni yule kiumbe mmoja wa binadamu wawili, aliye pendelewa na muumba wake kwa kukirimiwa kuwa yeye ndiye TAASISI ya kwanza na ya kipekee katika taasisi zote za kitaaluma na kimalezi. Hakuna jabari yeyote wala mpole yeyote duniani ila kazaliwa, kalelewa na kupewa maarifa ya kwanza na mwanamke. Mwanamke akiwa yeye ndiye taasisi ya mwanzo na ya kipekee katika suala la kutoa maarifa basi hapana budi ila naye kujiendeleza kitaaluma ili aendane na mabadiliko ya kitaaluma na kisayansi yanayo ibuka siku hadi siku, bila shaka akiwa yumo katika mipaka ya utashi wa aliye muumba ili apate kuwa salaama hapa duniani na kesho baada ya uhai wa sasa.


Tayari hapo juu tumesha mtambulisha mwanamke kiasi cha kumfahamu upya pengine kinyume na hapo awali. Sasa ni wakati wa kuvitambulisha vitu vingine vinavyo fungamana au vilivyo na uhusiano na makala yetu haya. Muislamu ni kiumbe yeyote aliye umbwa halafu akawa chini ya muongozo wa yule aliye muumba. Yaani akubali kuishi maisha yake bila ya khiyari ya kutafuta miongozo mingineyo inyo kwenda kinyume na muongozo mkuu alio wekewa na muumba wake. Kwa maana hiyo basi malaika na viumbe wengineo wote waishi maisha ya uislamu kwa sababu wao hawana khiyari ya kuchagua kinyume na maisha akiyo wapangia muumba wao. Kwa lugha nyengine ni kwamba kiumbe yeyote anaye weza kujiamulia kuishi tofauti na muongozo alio wekewa na muumba wake, kiumbe huyo atakuwa katoka katika maisha ya uislamu kwa kipindi cha muda wote atakao uishi kinyume na muongozo alio utoa muumba wake.


Maneno tulio yaandika katika ibara hapo juu hayana ashiria jambo ... nalo ni jambo litalo kuwa ni kikwazo kwa baadhi yetu, hata wasomaji wa makala hii. kikwazo ni jambo lolote linalo weza kukuzuia kulianzisha kimatendo lolote ulilo amrishwa na utazi wako. Ama changamoto ni moja ya aina za vikwazo ingawa kunatofauti baina yake. Yaani changamoto ni lolote linalo mzuia mmoja wetu kuliendeleza jambo alilo kuwa kalianza kabisa kimatendo, na kikwazo ni lolote linalo mpelekea mmoja wetu kulianza lolote alilo tamani kuliasisi au kulitekeleza.


Ibara zilizo tangulia hapo juu ilikuwa ni kuitanguliza makala kwa msomaji tukimuandaa apate kuyasoma makala haya kwa utashi na moyo mkunjufu akiwa na taswira halisi ya yale yanayo tarajia kumvutia kuyapata maarifa mapya kuhusu mwanamke katika nyanza iliyo jieleza kwenye kichwa cha habari hapo juu kisemacho " Mwanamke muislamu na changamoto zinazo mkabili ".

Mtizamo wa uislamu kwa mwanamke yeyote bila kujalisha ni muislamu au laa, ni kwamba mwanamke ni kiumbe aliye tukuzwa kutokana na wadhifa wake wa kijamii kama tulivyo elezea huko juu. Kwa mktadha wa utukufu alio pewa mwanamke hali kadhalika amewekewa mipaka ili aendelee kuishi katika utii wa muongo wa aliye muumba. Sasa moja ya vipengele vidogo vidogo vya muongozo mkuu ni hapo ALLAH alipo amua kutuonesha fadhila kubwa za elimu tukiilinganisha na mambo mengineyo:

... هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ ...

... Jee, wanalingana ambao wanao jua na ambao wasio jua ? hakika hanao elewa hili ni wale wenye akili tu ( wala si vyenginevyo )...


Pia mtume amesema:


من سلك طريقًا يطلبُ فيه علمًا ، سلك اللهُ به طريقًا من طرقِ الجنةِ ، وإنَّ الملائكةَ لتضعُ أجنحتَها رضًا لطالبِ العِلمِ ، وإنَّ العالِمَ ليستغفرُ له من في السماواتِ ومن في الأرضِ ، والحيتانُ في جوفِ الماءِ ، وإنَّ فضلَ العالمِ على العابدِ كفضلِ القمرِ ليلةَ البدرِ على سائرِ الكواكبِ ، وإنَّ العلماءَ ورثةُ الأنبياءِ ، وإنَّ الأنبياءَ لم يُورِّثُوا دينارًا ولا درهمًا ، ورَّثُوا العِلمَ فمن أخذَه أخذ بحظٍّ وافرٍ


Yeyote atakaye ichukuwa njia kwa ajili ya kuitafuta elimu, ALLAH atampa njia moja wapo ya njia za kwenda peponi, hakika malaika huweka mbawa zao ( juu ... kwa lengo la kuweka kivuli ikiwa ni ishara ya radhi ) kwa mtafutaji wa elimu, na msomi ya dini huombewa msamaha na wakaazi wa mbinguni na ardhini pia nyangumi ( na viumbe wengeo ) huko baharini. Hakika kama ilivyo kuwa mwezi ungaao usiku unafadhila kubwa kuliko sayari nyenginezo zote hivyo hivyo fadhila za msomi wa dini ( ni kubwa sana) kuliko anaye abudu bila kuwa na elimu. Wasomi wa dini ndio warithi wa mitume ... hakika mitume hawakurithisha dinar wala dirham ( pesa ). Mitume walirithisha elimu, yeyote atakaye shikamana na elimu atakuwa kashikamana na na chanzo cha mema kisicho katisha neema.


Kidogo kidogo tunabainikiwa kiasi cha kumfanya msomaji wa makala hii, kuelewa ukubwa wa fadhila za elimu kuliko mambo mengineo mengi.

Sasa mwanamke katika kuitafuta hiyo fadhila hizo hapana budi kwake ila akatafute elimu tu, ingawa pia vielelezo ( aaya na hadithi ) tulivyo viweka hapo juu vinahusu zaidi elimu ya dini kuliko elimu nyenginezo, ikumbukwe wazi kuwa uislam haukutuzuia kuisoma elimu ya mazingira maana mazingira nayo pia dini. Muhimu tunapo isoma elimu ya mazingira tuwe na nia halisi na safi kuitumikia dini tukiwa katika mipaka ya muongozo wa muumba. Tukifanya hivyo bila shaka tutaingia katika kundi la fadhila za elimu.


Moja ya vipengele vya muongozo wa ALLAH kwa walimwengu ni hijabu, yaani hijabu ni moja ya mambo muhimu yanayo pelekea mfumo wa Uislamu kudhihiri ndani ya jamii. ALLAH alipo watuma mitume wake kwa mwalimwengu wenziwao, walikuwa na lengo la kujakukataza na kuzuia maasi. Moja ya maasi walio kujakuyapiga marufuku ni suala la zinaa. Yaani kuondoa mfumo wa kujamiiyana kiholela jambo linalo pelekea nasaba za watu kupotezwa au kuchanganwa na kupelekea haki za urithi kupotea.

Katika kulizuia suala la uzinifu ALLAH aliwaanuru waumini wajiepushe na zinaa kwa kuto kuikurubia kabisa:


وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَا إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا

wala msikurubie zinaa ( ikawa mumefungua mlango wa zinaa) hakika zinaa ni ovu na njia mbaya (inayo pelekea kuigia jahanamoni).


Ili maamrisho ya ALLAH yatimie na uzinifu utokomezwe, ALLAH wafunza mitume wake mikakati itakayo pelekea uzinifu kutokomezwa. Mikakati husika ni kama ifuatayo:

  • kupiga marufuku mchanganyiko wa wanauma na wanawake.

  • kuamuru wanawake kuvaa hijabu itayo pelekea wao kutokuwa vishawishi vya mihemko kwa wanaume nakuwapelekea wanaume kutafuta njia za kukimu mihemko yao njia ambazo zinaweza kusababisha dhambi ya zinaa.

  • kuwaamuri wanawake kuto kujiremba kwa urembo wa aina yoyote mbele ya wanaume ambao wanaweza kuwaoa ... ila tu wajirembe kwa waume zao wakiwa na lengo la kuwavutia waume zao na kuwashawishi hatima ya kujamiiyana.

kwa upande mwengine pia ALLAH amewaamuru waislamu wote kike kiume na kuwaasa kuhusu suala la dunia na akhera:



وَابْتَغِ فِيمَا آتَاكَ اللَّهُ الدَّارَ الْآخِرَةَ وَلَا تَنْسَ نَصِيبَكَ مِنَ الدُّنْيَا وَأَحْسِنْ كَمَا أَحْسَنَ اللَّهُ إِلَيْكَ وَلَا تَبْغِ الْفَسَادَ فِي الْأَرْضِ إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ


(Ewe muumini) tumia neema aliyo kupa mola wako, uitafute akhera wala usisahau fungu lako duniani. Na ufanye wema (katika kutumia neema hizo) kama alivyo kufanyia wema ALLAH (akakupatia neema hizo na wengine akawapunguzia). Wala usifanye ufisadi ardhini.Hakika ALLAH hapendi wanao fanya ufisadi.


Aaya zinazo husu mlango huu ni nyingi mnoo, tutosheke na hizo tulizo ziweka hapo juu ili tupate kuendelea moja kwa moja na maudhui tulio ikusudia.

Tunapo itafakari aaya ya pili hapo juu, tutaelewa kwa nini haifai wanawake kujizuia kusoma faana mbali mbali za kitaaluma kwa lengo la kujikimu kimaisha hapa duniani. Hata hivyo kulaulazima waislamu kutakbua kuwa sio kila faani ndio inafaa kusomwa, khasa khasa kwa wanawake ukilinganisha na wanaume ambao ni faani chache zisizo faa kusomwa.

Sasa bila kujalisha ni faani gani wanawake waislamu wamesomea, kiukweli kuna changamoto nyingi sana sinazo wakabili baada ya wao kuhitimu faani husika tukizingatia kuwa upana wa maana ya hijabu unaweza kuwapelekea kuwa kati ya moja ya hali mbili:

  • kuwa mbali ya utekelezaji wa maamrisho ya ALLAH kuhusu hijabu kama tulivyo ashiria hapo juu au,

  • kuwa katika maamrisho ya ALLAH na kushikamana na mipaka ya upana wa maana ya hijabu jambo litalowafanya kuwa mbali na kulitafuta fungu lao duniani hapa.

hiyo ni moja ya changamoto tulizoashiria hapo juu kwenye kicha cha habari ya makala haya. Sasa huenda ya kajitokeza masuali kadhaa utakayo jiuliza wewe msomaji wa makala haya au pengine ukajikuta kuwa njia panda kwenye makutano ya njia zaidi ya moja na ukakosa nini la kufanya, maana kuna masuala ya kujinasua na suala la upana wa maana ya hijabu kama tulivyo ashiria hapo juu. Kwa haraka mtu anaweza dhani kuwa dini haiwezi kutekelezeka vilivyo kutokana na mfumo wa vituo vya elimu vinavyo endeshwa.

Hijabu kiuhalisia sio kikwazo kwa mwanamke kuitafuta elimu na njia za kujinasua tukizingatia kuwa njia ni mingi mnoo za kuyafikia maendeleo na kujinasua.

ALLAH asema katika kitabu chake kitukufu:

... وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ ...

... ( ALLAH ) hakujalia dini kuwa karaha ( au lolote lisilo kuridhisheni ) kwenu ...


Mimi binafsi naamini kuwa hijabu sio changamoto sikuambii kikwazo cha mwanamke kujinsua. Bali mhusika yeye mwenyewe ndiye tatizo kwa kudhani kwake kuwa hijabu ndio tatizo. Tatizo sio hijabu bali sisi wenyewe wanajamii ndio tatizo maana tumeifadhilisha dunia kuliko kahera, jambo linalo pelekea hijabu kuwa ni vigumu kwa wanawake waiislamu walio wengi kuivaa. Wanapo ivaa pia bado huwa wavaa kama fashion jambo linalo pelekea badala yao wao kuwa nakika hijabu ya kisheria wajikuta wamo katika kujifunika tu badala ya kustirika wasiwe vivutio vya mihemko kwa wanaume wasio haki yao kimatamanio. Maana lengo la hijabu ni kuweka kizuizi cha upanyo wa kutamanika wala si vyenginevyo. Wanawake wengi wamekuwa wajifunika bila yao wao kuwa katika hijabu maana nguo walizo jifunika huwa hazikidhi masharti na vigezo vya kuwa ni hijabu inayo wezo kuzuia wao kuwa kivutio kwa wanaume.

Utayari wa kuvaa hijabu ni mdogo sana kwa walio wengi. Sababu kuu la hali kuwa hivyo baadhi yake ni kama zifuatazo:

  • hijabu halisi kuto kuwekewa mkazo na wasimamizi wa wanawake,

  • kuenea kwa fatwa za maajabu wanazo zitoa baadhi ya wasimamizi wa masuala ya kiimani,

  • wanajamii kuwa na dhana isiyo sahihi ... kudhani kwao kuwa hizo fatwa za maajabu ndio zinazo wa halalishia kujifunika maguo badala ya kuvaa hijabu, na wasimamizi hao kudhani kuwa dhima sio yao bali ni dhima ya walio watolea hizo fatwa.. Ukweli ni kwamba wote wapo hatiani kabisa na lililo baki ni wao kujipatia moyo na kujipongeza,

  • kuwa mbali na vikao vya kielimu, hata kama wanashiriki baadhi ya vikao wao huvikimbia vikao vya elimu ya itikadi na kuisogelea fiqhi ile hali elimu ya itikadi ndio msingi wa funguo wa peponi. Maana fiqhi bila itikadi sahihi ndio huwapelekea kudhani kuwa hali yao ya kujifunika nguo badala ya kuvaa hijabu, ni hali itakayo wasalimisha mbele ya ALLAH,

  • kujaza sana dunia vifuani kuliko akhera kiasi walio wengi wamo katika kuikusanya dunia wewe na kingi bala wao kuzingatia mipaka ya uchumaji wa mali katika radhi halisi za ALLAH.

  • Uhaba wa malezi halisi kwa misingi ya imani ya dini ya kiislamu imani ambayo inabidi ndio ifanywe kuwa utamaduni wa jamii za waislamu. .




 
 
 

Comments


bottom of page