top of page

UNYANYASAJI

Updated: Jun 29, 2022

Utangulizi

Picha hii tumeipata famii forum

https://twitter.com/jamiiforums/status/1315522202306052096

ree

Tafiti nchini Marekani zinaashiria kwamba asilimia 20 ya wasichana na 8% ya wavulana hufanyiwa unyanyasaji wa kijinsia kabla ya kufikia umri wa miaka 18, na inatia wasiwasi kwamba asilimia hizi hazitokei mbali na na maeneo yanayo tarajiwa kuwa yatakuwa na usalama katika maisha yao, mfano shuleni. , nyumba za marafiki na jamaa, au hata ndani ya kaya wanazo ishi.


Kulingana na Kikundi cha Kitaifa cha Kiwewe cha Mtoto cha nchini Marekani NCTSN, zaidi ya nusu ya visa vyote vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto vinatokana na jamaa au mtu wa karibu na wanafamilia, mfano rafiki wa familia au jirani, na kulingana na Baraza la Ulinzi wa Mtoto kwamba 95% ya kesi za unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto ni kutoka kwa mtu mwenye taarifa halisi za mhanga husika.


Katika makala hii tumeshawishika kukuleteeni mambo yanayo weza kusaidia kuviepuka kwa mbali ikiwa sio kwa karibu, vitendo vya unyanyasaji kwa watoto. Pia tunasikitika sana kukosa taarifa halisi na za kuaminika kuhusu ukubwa wa vitendo vya unyanyasaji barani Afrika kwa jumla, na hasa nchi Tanzania, kadhalika katika ngazi ya mikoa na wilaya, tarifa hakuna zaidi ya ishara zinazo ashiriwa na wanajamii pia katika mitandao ya kijamii mfano wa jamii forum katika tovuti yao ( https://twitter.com/jamiiforums/status/1315522202306052096 ) . Dondoo zetu tutazileta kupitia yafuatayo:

  1. Maana ya unyanyasaji

  2. Njia za unyanyasaji

  3. Aina za unyanyasaji

  4. Wahanga wa unyanyasaji?

  5. Wanyanyasaji ni kina nani?

  6. Takwimu kuhusu vitendo vya unyasaji

  7. Namna ya kuuepuka unyanyasaji



katika video hapo nchini kuanzia mwanzo hadi dakika 1:17 Rais Samia Suluhu Hasan akidokeza kuweko unyanyasaji nchini Tanzania


sasa baada ya kumsikiliza rais Samia ni wakati wa udadavuzi wa dondoo za makala.


MAANA YA UNYANYASAJI ( bado)


NJIA ZA UNYANYASAJI ( bado)


AINA ZA UNYANYASAJI ( bado)


WAHANGA WA UNYANYASAJI NI KINANANI? ( bado)


WANYANYASAJI NI KINANANI? ( bado)


TAKWIMU KUHUSU VUTENDO VYA UNYANYASAJI ( bado)


NAMNA YA KUJIKINGA DHIDI YA UNYANYASAJI WA KIJINSIA


Kwa hivyo, kumfundisha mtoto jinsi ya kujilinda ni muhimu sana, kwani huwezi kumfuatilia na kwenda naye sehemu zote atakokwenda yeye kila wakati. Lakini anaweza kufundishwa kujilinda mwenyewe, haswa kwa vile watoto wanaweza wasijue maana na matokeo ya unyanyasaji wa kijinsia kwao wao, jambo linalo weza kupelekea kurubuniwa na wakarubunika kwa kulaghaiwa na ahadi wanazo pewa na watu wenye nia mbaya, hata kama wanawezahisi na kutambua vizuri kwamba kuna jambo lisilo la kawaida wanatendewa.


Kwa mkhtasari mfundishe mwanao vidokezo 9 ambavyo vitakuwa ndio mwongozo wake wa kumzindua kabla hajafanyiwa lolote la kiunyanyasaji mwanao jambo litalo msaidia kujikinga na unyanyasaji :

1. Mfundishe mwanao kuwa kiwili wili kia sehemu zionekanazo na zisizo onekana. Halafu mjuze kuwa sehemu zisizo onekana sio ruhusa mtu yeyote kuziona wala kuzigusa hata kama ni baba yake mzazim mama yake mzazi, kaka na dada zake na watu wa nyumbani kwao pia na majirani. Bali mwambie kuwa tendo la kuguswa sehemu hizo likifanyika ni lazima atoe taarifa kwa wazee au mmoja wa wazee aliye kuwa siye ndiye aliye tenda kitendo hicho au akaripoti polisi kabisa. Jitahidi kumjuza kiasi awe na uwezo wa kutofautisha baina ya sehemu za " UCHI NA UTUPU ", usikose kabisa kumfunza viungo vya mwili wake kwa majina. Haraka unapozungumza na mtoto wako juu ya mipaka ya mwili wake, Pia ujizuie kugusa sehemu zake za siri. Ni lazima mzazi kuwa yeye ndiye mwalilu wa kwanza kwa mwanawe, yaani mzazi amfundishe mwanawe majina ya sehemu za mwili wake kwa kwa msisitizo badala ya mtoto kufundishwa kwa mara ya kwanza skulini na waalimu au mitaani na watu wengine. Baadhi ya watoto wanayenyanyaswa ni mwoga sana hawapo tayari kuwa waziwazi pindi yanapo tokea manyanyaso dhidi yao kwa kuwa tu wazee wao hawakupatapo kuwafundisha maswala hayo . Ama mnyanyasaji akitambua kwamba mtoto atawaeleza wazazi wake yale aliyo tendewa, ataogopa mnoo kuibuliwa kwa wanajamii. Sasa kabla yajatenda tendo lake la unyanyasaji hutafuta kumsoma mtoto, akigundua kuwa mtoto ana maarifa sahihi kuhusu unyanyasaji ni rahisi huyo mhalifu kujizuia kumtendea mwanao kwa khofu ya kuadhirika na mashitaka ya mtoto.

2. Mipaka ya mwili Mfundishe mtoto wako kwamba hakuna mtu aliye na haki ya kugusa maeneo yake ya yanayo funikwa na mwili wake maana ni maeneo binafsi kwake tu na kwamba hakuna mwengine mwenye haki ya kugusa wala kuyatizama kwa hali yoyote ile isipokuwa kama yeye ni mgonjwa wa sehemu husika tu, si jamaa yake wala mtoto mwenziwe katika marafiki zake na watu asio kuwa na urafiki nao, na kwamba kuonyesha maeneo haya haifanyiki bila uwepo wa mzazi na katika kesi maalum kama uchunguzi wa daktari. Mtoto lazima ajue kuwa hakuna mtu mwenye haki ya kumtaka aonyeshe sehemu hizo za mwili wake, au kuzigusa au kuzipiga picha, au kuona viungo vya mtu mwingine pia, na ikiwa mmoja wao atafanya hivyo, lazima kukataa na ni bora kwake yeye kuondoka mahali hapo mara moja, na kumjulisha wazazi au walezi wake, na ikiwa ni mmoja wa wazazi/walezi au wote wameshiriki unyanyasaji, basi mtoto akaripoti katika vyombo vya dola .

3. Mjuze mwanao kuwa kuna aina mbili za miguso:

  • mguso salaama na,

  • mguso usio salaama yaani wa kutisha.

Mfunze aina zote hizo mbili za miguso kinadharia na umuombe ajiguse sehemu zote za mwili wake unazo mtajia ili atambue maeneo ya miguso salaama na miguso isio salaama katika mwili wake. Halafu umjuze kuwa umemuomba kujigusa mwenyewe kwa kuwa wewe mzazi pia huna ruhusa ya kugusa sehemu zake hizo husika, jambo ambalo humwezesha kujua kivitendo kuwa ni kweli sehemu husika hazifaai kuguswa na yeyote dunia zaidi yake mwenyewe au kwa dharura za magonjwa akiwa na wazazi wake spitalini.

4. Muombe ruhusa mwanao kabla ya kuugusa mwili wake na umjuze kuwa mwili wake ni mali yake pekee, na ana haki ya kuombwa ruhusa kabla ya kuguswa na yeyote awaye katika jamaa na wageni, kama vile watu wazima wana haki ya kuridhia kabla ya kuwaguswa, na jambo hili huongeza ujasiri na ujuzi wake wa mipaka yake binafsi na mipaka ya wengine pamoja naye. Hata inapo bidi kumkumbatia mwanao muombe ruhusa ili kumzoesha kuwa mwili wake ni milki yake ya kipekee apate kutambua kuwa hapaswi kukumbatiwa na yeyote bila ruhusa yake mwenyewe, na haipendezi. kwa mtoto kuzoea kumbusuwa.

5. Mfundishe mwanao kusema "Hapana". Mtoto lazima afundishwe haki yake ya kupinga na kusema "hapana", atajikuta ni hodari wa kukataa lolote asiloridhika nalo hali hii itapelekea aheshimike bila kutishika na lolote hasa atapo hisi kuwa hayupo salaama na miguso au mipapaso migeni kwake wala hatokosa kosa kusema hapana kwa yeyote awaye.

6. Mtengenezee mwanao mtandao salama. Hisia ya usalama ya mtoto haipatikani kiurahisi kama wanavyo zani walio wengi , lakini huandaliwa tokea mwaka wa kwanza wa umri wa mtoto na kuimarishwa kadri anavyo songa mbele kimaisha, na uwepo wa dhamana salama kwake yeye, hilo hufanyika kwa kumjuza kuwepo hatari ya usalaama wake kutoka kwa mtu mwingine japo mmoja wa wazazi jambo litakalo msaidia kufanya maamuzi magumu ya kutoa taarifa iwapo atafanyiwa unyanyasaji kutoka kwa watu wa kayani anakoishi yeye kwa wakati huo. Tunaamini kuwa hali hii itamuongezea utashi mkubwa wa hisia za usalaama wake na kwa watoto wenziwe . Mtoto anapofikisha umri wa miaka mitatu lazima awe na mtandao salama wa watu kadhaa kutoka kwenye familia, ikiwezekana hata kutoka kwa watu wasio kuwa katika familia yake, mfano wa mwalimu au mwanasaikolojia shuleni kwake, wawe ndio kimbilio la kwanza ikiwa tu mtoto atahisi hatari ya usalaama wake au wa watoto wenziwe kwa lolote, bila woga hata kama akitishiwa na mtoto mwingine au kutoka kwa mtu mzima.

7. Itambulike kuwa Zaidi ya asilimia 73 ya watoto waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia hawamjulishi mtu yeyote kile kilichotokea kwa mwaka mmoja au maishani mwao, kulingana na American Huff Post, asilimia 45 ya watoto huhifadhi kile kilichowatokea kwa Zaidi ya miaka mitano, na hii ndiyo sababu ya lazima ya kusisitizwa umuhimu wa kufahamisha watoto uwezekano wa hatari ya unyanyasaji wa kijinsia inayo wazunguuka kutoka kwa watu wanaoishi nao au wanao kutana nao katika maeneo tofauti wawe watu wazima au watoto wenzi wao… na ulazima wa kutoa taarifa kwa watu wazima kuhusu chochote kinachotokea. Halafu umuhakikishie mwanao kwamba yuko salama hatotokewa na lolote la madhara kwa kutoa kwake taarifa husika.Tuwasisitize wanetu kuwa hakuna siri, iwapo watatokewa na vitu vya unyanyasaji.

8. TUwafunze wanetu kuwa sehemu zote za miili yao zisizo onekana ni sehemu zisizo pashwa kuguswa na mtu yeyote hata kama ni baba au mama mzazi isipo kuwa tu kwa dharura za kitibabu na ana haki ya kupinga hili kwa kusema "Sitaki uniguse". Pia, mfundishe tofauti kati ya hali ya usalama na woga kwa kutoa mifano, kwa kumuuliza anahisi nini unapoketi karibu naye kabla hajalala, ambayo ni hisia ya faraja na usalama, na anahisi nini akikupoteza.

9. Tuwafundishe wanetu tabia zisiyokubalika kama kuvua nguo mbele za watu hata kama ni watoto wenziwe, kuingia bafuni chooni watu wawili kwa pamoja kwa sababu yoyote iwayo na ikiwa anakabiliwa na hili, lazima akataa kwa nguvu na kupiga kelele, pamoja na kukataa pia tuwafunze kukataa kumbusiwa sehemu yoyote ya mwili wake au kukaa juu ya. mguu wa mgeni yeyote, au kuwa pekee yake naye na kuuliza vitu ambavyo vinavyo husiana na mwili wake.


Ahsante sana kutoa muda wako kusoma makala hii. Toa maoni yako.

 
 
 

Comentarios


bottom of page