top of page

NYENZO NA MAENDELEO

Updated: Jan 9, 2023


Jee, waelewa kuwa dhana ya ukosefu wa maendeleo katika jamii ya kiislam ina mizizi thabiti na ina ukweli kwa asilimia kubwa sana? Pia tambua kwamba jamii yoyote isiyo kuwa na maendeleo sio jamii tulivu katika uthubutu wa uthibiti wa mila na tamaduni zao, bali watacho kifanya watu wa jamii hiyo ni kuiga zuri n abaya la jamii nyenginezo wanazo kwa sababu tu ya kile ninacho vutia katika mambo ya maendeleo.

Waislam popote walipo ilikuwa wawe ni vigezo kwa jamii nyenginezo ukizingatia sifa alizo wapamba nazo ALLAH. Hali kadhalika Mtume ameashiria sana tu suala la uwepo wa maendeleo katika jamii, hapo alipo bainisha nyenzo mama na za msingi katika kuyaendea maendeleo.

اغْتَنِمْ خَمْسًا قبلَ خَمْسٍ:

  1. شَبابَكَ قبلَ هِرَمِكَ،

  2. وصِحَّتَكَ قبلَ سَقَمِكَ،

  3. وغِناكَ قبلَ فَقْرِكَ،

  4. وفَرَاغَكَ قبلَ شُغْلِكَ،

  5. وحَياتَكَ قبلَ مَوْتِكَ

Faidikeni na mambo matano kabla ya mambo matano:

  • Ujana wako kabla ya uzee wako

  • afya yako kabla ya kuumwa kwako

  • mali zako kabla ya ufakiri wako

  • fursa ya muda wako kabla ya kushughulishwa

  • uhai wako kabla ya kifo chako



Faida ya hadithi iliyopo hapo juu ni kutujuza kuwa tutapo zitumia kwa usahihi nyezo tajwa tutakuwa tumeidiriki faida ya dunia na kesho akhira, nakinyume chake ni khasara ya dunia na akhera. Leo ukifuatilia kwa umakini katika jamii ya kiislam Tanzania na baadhi ya maeneo duniani utabainikiwa kuwa jamii yetu imo katika hali ya ukosefu wa maendeleo katika nyanza nyingi za Maisha, hali yakuwa nyenzo na zana za chachu ya maendeleo zimejaa sana katika maeleo tunakoshi.

Tuchukuwe mfano wa nyanza ya kidini, zimekuwa zatumika mamia ya pesa kwa lengo la kuimasha jamii katika upande wa kiimani. Hili ni jambo zuri sana kwa watendaji na watendewa, il akwa bahati mbaya sana miradi hiyo inapo kamilika na kuwakabdhi watumiaji, baada ya miezi kadha tija yake huwa kinyume na matarajio ya walio toa mali na muda wao katika kuwaletea waumini huduma jirani na maendeo ya kaya zao iki wapate wepesi wa kuyaendea masuala ya Imani. Kinacho fuatia ni ukosefu wa matumizi sahihi na uhaba wa ukarabati wa miradi husika ili matumizi yawe ni endelevu toka kizazi na kuhamia kwa kizazi kijacho. Kuna misikiti mingi na nywakfu (wakfu) vingi sana Tanzania vitumiki kwa usahihi kabisa. Kuna haja kubwa sana ya watu kuwa na mtizamo upya kuhusu uasisi wa miradi ya kiimani. Badala ya kuasisi vituo vipya ni baro gharama hizo kuhuwisha vituo kongwe kwanza.

Sisi tumeanzisha juhudi za kutumia nguvu zetu katika kuhakikisha kuwa tunahuwisha miradi na vituo vilivyo legalega ikiwa sio kutelekezwa kabisa. Juhudi zetu hizo tumezianzisha mwaka 2018 katika mkoa wa Dar es Salaam:


1. MASJIDUL MADINATUL MUNAWARAH - KAZAMOYO



Kituo cha kwanza kufaidika na juhudi zetu ni masjidul madinatul Munawara iliyopo wilayani Ubungo, Kibamba Kwembe, mtaa wa mloganzila hadi leo 2023. Msikiti huu uliasisiwa katika eneo la uchache wa waumini jambo lililo washawishi maimam kadha walio tangulia, kuuacha msikiti utelekee hadi tulipo fika sisi. Kituo hiki kimeasisiwa mnamo mwaka 2016. Msikiti huu una historia ndefu sasa tokea kujengwa kwake hadi wakati huu tunavyo andika makala hii mwaka 2023. Bali ataye kuwa hai anaweza kushuhudia mambo kutokana na nyakati zitavyo zidi kusonga mbele. Itizame hali ilivyo utaelewa kwanini hata waislamu walio jirani wakaamua kukaa majumbani kwao.


2. MADRASATUN NUURIL MUTAQIINA

Madrasatun Nuuril Mutaqiina, ni madrasa ilipoko Goba mpakani … hapa tulifika kwa njia zisizo tarajiwa. Baada ya ALLAH kukadiria kuwepo madras ani hapo leo januari 2023 tumasha kamilisha anza mwezi wa sita wa huduma. Tulipo ingia hapa, hapakuwa na jingo lolote lililo andaliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za madrasa, ingawa ilikuweko baraza iliokuwa ikitumika kusomeshewa vijana, walipo asisi mwaka wa 2020. Madrasa hii sio milki yetu wala hatuna nia ya kuimiliki labda kama wahisita wataona hivyo na wakadhamiri kufanya hivyo,


3. MASJIDUL IMAAN

Masjidul imaani hukohuko Goba mpakani, kufika kwetu katika kituo hiki pia ni kwa uwezo wa ALLAH. Waumini wa msikiti huo walipo una utendaji wetu katika madrasatun nuuril mutaqiina, walishawishika kutufuata na kutuomba tuuendeshe kikamilifu msikiti huo. Kwa kipindi kikubwa sana msikiti hii ulikuwa ukiyumba kutokana na ukosefu wa usimamizi madh’buti. Jambo lililo wasukuma waasisi wa msikiti huu kuvunja uongozi wa kundi wa hapo awali na kubaki na uongozi wa watu watatu tu bila ya ziada. Hata hivyo juhudi zao za kutukabidhi dhamana ya uendeshaji kamili wa msikiti huo zilihudhuriwa na waumini wasio pungua kumi katika kikao kilicho fanyika hapo hapo kituoni masjidul imaani. Sisi Gshtargets tumekiweka kituo hiki katika uangalizi na kudurusu dhamira ya wamiliki. Tutapo jiridhisha na dhamira zao tutafunga nao mkataba wakutulinda ili kuepuka yasiyo tarajiwa.


4. PROF KAMAL ABEID QURAAN CENTRE

Uhuishaji wa kiwanza cha wakfu kilicho tolewa wakfu kwa kipindi cha miaka Zaidi ya kumi, katika eneo la ukawa kunakiwacha cha wakfu kilicho tolewa na muumini ili kiwe ni moja ya nyezo za maendeleo kwa waislamu. Lakini kwa kipindi kikuwa sana kiwanza hiko hakikufanyiwa lolote kwa hoja wa kutafutwa ufadhili wa ujenzi wa msikiti na madrasa. Tulipo pata taarifa ya kiwanza hicho tuliwatafuta wahusika na kuongea nao kuhusu uhaba ya ugumu wa ufadhili wa eneo lisilo tumika. Wahusika walituelewa na kutukubalia. Siku mbili baada yah apo tulifyeka na kusafisha eneo zima halafu tukachimba na choo na kuanza kutafuta miti ili tusimamishe jingo la miti linatarajiwa kutumika kuwa madrasa kwa ajili ya kuwaepusha Watoto kutembea masafa marefu kwa ajili ya kufuatia huduma za madrasa katika maeneo ya masafa marefu.



 
 
 

Comments


bottom of page