MABADILIKO AU MAGEUZI
- Gshtargets
- Jul 20, 2022
- 4 min read

Maana ya mabadiliko:
Mabadiliko ni haja fulani inayo dhihiri katika fikra za mtu au kundi la watu fulani, haja hiyo huchochewa na hali ya mwinendo fufani unao jitokeza katika eneo au jamii kwa jumla na wahusika wakaona haja ya kubadili hali husika. Hivyo mabadiliko ni hali ya kuachana na baadhii ya mazoea na tabia fulani zisizo hitajika, walizo nazo wanajamii au baadhai ya wanajami, na kuhimiza tabia nyenginezo kwa watu wote katika jamii husika, zinazo lenga dira ya mabadiliko tarajiwa.
Mfano wa mtoto, au kijana, humbidi aendane na mabadiliko ya utawala katika shule, mabadiliko ya waalimu katika darasa ...Nk.
Aina za mabadiliko
Mabadiliko yana aina mbili kuu bila kujalisha nyanza za mabadiliko tarajiwa nazo ni mabadiliko kutoka hali mbaya kwenda hali nzuri na ya afadhali kuliko hali ya awali. Suala la ubaya au uzuri wa mabadiliko huhukumiwa na mfumo wa jamii husika.
Mfano:
mabadiliko ya nyanza za kiuchumi ni jambo la kawaida tu watu kuyabaini maana hujikuta thamani ya pesa zao yawahudumia wingi au uchache katika mahitaji yao ya kila siku au kinyume chake.
mabadiliko ya nyanza za kimaadili pia ni jambo la kawaida tu watu kuyabaini maana hujikuta katika hali ya watoto kutokuwa na heshima kwa watu wakubwa au kinyume chake pia.
Kupitia mifano tulio ielezea hapo juu tunatumai kuwa kila mmoja ataweza kuelewa nyanza nyengineza za mabadiliko tulizo kuwa hatukubahatika kuzitaja hapa. Baada ya kutambulisha mabadiliko ni nini na kuelezea mifano hapo juu sasa tunalazimika kugusia sababu za uhitaji wa mabadiliko.
Sababu za uhitaji wa mabadiliko
Uhitaji wa mabadiliko huwepo punde tu ianapo bainika kuwa kuna mambo yasio hitajika tena katika jamii fulani bila kujalisha mambo hayo ni mazuri au mabaya. Yaani mabadiliko yanaweza kuwa ni kutoka hali nzuri kwenda hali mbaya au kutoka hali mbaya kuelekea hali nzuri kama tulivyo bainisha.
Mfano mzuri wakutupatia taswira halisi ni katika yafuatayo:
Nchini singapor miaka ya nyuma raia walikuwa waishi maisha ya kiuchumi ya uporaji wa mali za wapita njia, hali ilio washawishi baadhi ya raia nchini humo kubuni mikakati ya kuleta mabadiliko katika jamii yao. Leo hii singapor ni moja ya nchi inayo pigiwa mfano duniani kutokana na mabadiliko chanya yalio fanywa. Ama mfano wa mabadiliko kutoka hali nzuri kwenda hali mbaya ni ule ulio dhihiri katika maishi yetu ya kila siku, vijana wengi sana wamepotoka kimaadili. Kiasi leo wadai uhuru wa maamuzi ya ndoa za watu wa jinsia moja. Eti mwanamke aolewe na mwanamke mwenziwe na mwanaume hali kadhalika.
Binadamu wote tunayo nafasi ya kukosea au kufanya vizuri katika kipindi chetu cha maisha. Pale tunapofanya vizuri tunastahiki pongezi na pale tunapojikuta tumekosea pia tunayo fursa ya kutambua na kufanya mabadiliko.
Maisha ni kama safari ambayo wakati mwingine huwezi kujua kule unakoelekea nini kitatokea kwa hiyo ipo nafasi ya kuruhusu mabadiliko kutokea katika maisha ya mtu. Wakati mwingine watu huchelewa kufikia mafanikio na kujikuta wakijilaumu kwa nini wamekosea. Leo tutajikita zaidi kwenye mada ambayo tumeipa kichwa HAJA YA MABADILIKO.
Hatakuwepo duniani binadamu ambaye katika maisha yake yote ataishi bila kukosea. Kwa hiyo kukosea ni jambo la kawaida sana katika maisha ya binadamu hata kama kwa njia moja huoni umuhimu wa kuweka matarajio ya kukosea.
Kuondoa matarajio la kukosea ukiwa kama binadamu katika maisha ni sawa kabisa na kujaribu kushindana na upepo kwani ni kitu ambacho hakiwezekanani kwa vyovyote kuweza kuuzuia upepo usivume.
Huwezi kufanya mabadiliko pasipokuwepo na eneo au kitu cha kubadilisha. Tunafanya mabadiliko pale tunapokuwa na kitu ambacho kwa namna moja hakiwezi kukidhi mahitajio fulani ya kijamii kwa wakati husika. Wakati mwingine neno mabadiliko limeonekana kuwa neno zito sana kiasi cha watu kushindwa kulivumilia au kulichukulia kwa umuhimu unaotakiwa na kujikuta wanaliogopa sana maana mara zote mabadiliko huwakosesha baadhi ya watu hadhi walizo kuwa nazo kijamii hapo awali. Sasa ni vema tulilainishe kidogo neno mabadiliko ili kupunguza ukakasi walio nao wengi, jamani kufanya mabadiliko tunako kukusudia hapa ni katika yale tulio kuwa na uwezo nayo.
Kiuhalisia sherehe nyingi za uhitimu yaani mahafali na mikusanyiko ya watu zimekuwa zaendeshwa tafauti ya matarajio maana ukizifuatilia kwa umakini haziendani na uhalisis wa malengo HALISI YA ELIMU NA TAALUMA YENYE TIJA KATIKA JAMII. Tija ya video mlizoziona, yaeleweka kwa kila mtu. Kiukweli Hakuna jambo baya katika maisha kama mtu kujua mapungufu fulani katika eneo fulani la maisha lakini akaendelea kuishi na mapungufu hayo huku akiwa na uwezo wa kuleta mabadiliko.
Kitu chochote atakachoendelea mtu kufanya kila siku hugeuka kuwa tabia yake mfanyaji. Wakati mwingine inaweza kuonekana ugumu wa kuleta mabadiliko kwa sababu tu tumezoea mambo yasio hitajika kufanywa. Jambo linalo pelekea mabaya kugeuka ndio tabia na tamaduni zilizo eneo katika jamii hatima yake mabaya kuwa ni sehemu ya maisha.
Ukweli ni kwamba hata katika upande wa mambo mazuri unayo yafanya kila siku ambayo yanasababisha wewe mwenyewe kuheshimika katika jamii, ulianza kwa kujifunza pole pole haijalishi kuwa ulikuwa unajua au hukujua kama unajifunza.Ulifanya taratibu na kurudia rudia, mwisho wa siku ikajengeka sasa kuwa tabia na imani kwako.
Baada ya kuwa na shauku ya kufanya mabadiliko tumependelea kufanya mabadiliko katika masuala ya sherehe za mahafali na mikuta tofauti maana sisi tunayo mamlaka katika sherehe hii.
Lengo kuu la kufanya mabadiliko ni kuwafanya wahudhuriaji kuendana na dhamira halisi ya lengo la elimu kinyume na mazoea ya mahafali na mikutano mingi inayo andaliwa siku hizi.
Mikutano na mahafali ni sehemu ya watu kubadilishana mawazo ili wapate kuzitatua changamoto zinazo wakwaza na kuwazuia kufikia malengo walio nayo wala sio sehemu ya pumbao bali sehemu ya kutafakari mafanikio na mambo kadhaa yanayo kwanza maendeleo yao.
GHARAMA NA HISTORIA YA MABADILIKO
Kiukweli sio rahisi kuyafikia mabadiliko bila kugharimika. Unahitajika ujasiri mkubwa wa kutamka neno mabadiliko katika jamii maana hiyo huwa ni ishara ya kuwataka wahusika kuachana na tabia zao walizo zizoea, tija yake ni kwamba unaweza kutuhumiwa kuwa huna heshima kwa watu husika. Jambo linalo weza kukusababishia chuki na kutengwa ikiwa sio kuuliwa kabisa.
Mifano iliyo hai tunayo:
1. Mtume kuliwa njama za kuuliwa
2. Maimamu kina Abuu Hanifa, Ahmad bin Hamba, Malik bin Anas na wengineo
wengi kufa kutokana na mateso walio fanyiwa na waheshimiwa wa zama zao.
Sio tu katika nyanza za kidini ndio haya hidhihiri bali hata katika nyanza za kijamii:
Lumumba, Mandela na wengineo wengi wapigania uhuri wa watu weusi
Comentários