HIJJAB KATIKA JAMII
- Gshtargets
- Jan 8, 2022
- 5 min read
Updated: Mar 7, 2023

Utangulizi
Uhalisiwa wa hijabu ni kwamba hijabu ni moja ya misingi ya kuwepo kwa jamii ya kiislam. Waislamu ni moja ya jamii za watu duniani. Kama inavyo eleweka kuwa jamii hutofautiana na jamii nyengineo kutokana na nidhamu na malezi ya jamii na nyenziye. Sasa hijabu ni moja ya nidhamu katika jamii ya kuislamu tena ni alama kuu ya kipekee inayomtambulisha muislamu na jamii yake popote walipo.
Katika waraka huu umepangwa muda huu kwa ajili ya makala ya hijabuna kwa miondoka isio zoeleka na walio wengi maana kuna mambo kadhaa yanayo husu hijabu, yasio zoeleka bali yakaribia kutokujulikana kuwa yahusu hijabu.
Katika makala hii tumeepuka mazoea walio nayo watu wengi kuhusu hijabu na kulazimika kuyagusia mambo kadhaa yalio na mahusiano na hijabu tukizingatia lengo zima la kuamrishwa kwa hijabu.
MSIKILIZENI MWALIMU UKHTY SARAH AKITOA NASAHA KWA MASIKITIKO MAKUBWA KUHUSU VYANZO VYA KUVUA HIJABU WANAFUNZI WA KIKE PUNDE TU WANAPO HAMA AU KUMALISA KUSOMA KATIKA SHULE ZA KIISLAM.
Dhana ya hijab katika Uislamu
Maana ya neno hijabu katika matumizi ya lugha ni:
Kizuizi
Stara au pazia
Katika dini neno hijabu limetumika kwa maana ya pili kama ilivyo tangulia hapo juu, yaani hijabu ni stara inayo mustiri mwanamke ili viungo vyake vya mwili visionekane na mwanaume yeyote anaye weza kumuoa. Yaani vazi linalo mstiri mwanake huitwa hijabu kwa kuwa huzuia viungo vyake kuonekana. Kumbe pindipo atavaa mwanamke vazi lisilo zuia viungo vyake kuonekana, mwanamke huyo atakuwa bado hajavaa hijabu.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyopo hapo juu tubainikiwe kuwa hakulazimika mwanamke kuvaa hijabu iwapo atakuwa katika mazingira ya ndani kwao kwa sharti wasiwepo wanaume wanaoweza kumuoa.
Mfano: baba mzazi,ndugu halisi wa kiume, ndugu kwa baba au kwa mama...
Lengo la hijabu katika uislam
Tokea zama na zama kutumwa mitume, zinaa imekuwa ni jambo la pili kukatazwa baada ya shirki.
Kila katazo walilo kuja nalo mitume, liliwekewa mikakati ilikufikia katazo husika kutekelezeka. Sasa kuamriwa uvaaji wa hijabu kwa waumini ni moja ya mikakati inayo pelekea katazo la zinaa kutekelezeka katika jamii.
Lengo kuu la kuamriwa hijabu kwa waumini ni kumzuia mwanamke kuwa kivutio kwa wanaume cha hisia za kujamiana.
Walio amriwa kuvaa hijabu
Hijabu imeamriwa kwa watu wote kike na kiume waumini na wasio waumini ingawa baadhi ya watu wamefanya kana kwamba hawahusiki na hijabu.
Sio tu wanawake ndio wanao lazimika kuvaa hijabu, bali wanaume pia wameamriwa kuvaa hijab. Hata hivyo hijabu ya kika ni tofauti na hijabu ya kiume. Ikumbukwe kuwa lengo la hijabu tayari limebainishwa hapo juu. Sasa tutambue kuwa hijabu ni lazima iwe na vigezo na masharti ili iitwe hijabu.
Masharti na vigezo vya hijabu.
Sio kila vazi ndio huitwa hijabu. Lazima masharti na vigezo kupatikana ili vazi liitwe hijabu, vyenginevyo sio hijabu. Masharti na vigezo ni kama yafuatayo:
Kuwa pana ili lisichore miinuko na mibonyeo ya mwili kwa mwanaume na mwanamke,
Kuwa zito kiasi cha kutokuuchora mwili pindipo upepo unavuma na kuifanya miinuko na mibonyeo ya mwili kudhihiri kwa mwanaume na mwanamke,
Kuto kuonesha mwili wa ndani au nguo za ndani, kwa mwanaume na mwanamke,
Kustiri sehemu zote za uchi, huambiwi utupu ndio kabisa. Hata hivyo uchi kwa mwanaume ni tofauti na mwanamke. Uchi kwa mwanaume ni baina ya juu ya kitovu na chini ya magoti. Ama mwanamke, uchi kwake ni sehemu zote za mwili isipo kuwa uso na viganja vya mikono na miguu. Hali hii inayo elezewa hapa ndio inayo tofautisha hijabu ya mwanaume na mwanamke.
Kushika au kugusana kwa hali yoyote sehemu yoyote ya mtu ya utupu ni uvunjaji na ukosefu wa sharti la hijabu maana kufanya hivyo huibua mihemko kwa mshikwaji na mshikaji labda kama ni walemavu wa mishipa ya hisiya za mihemko,
Kushika au kugusana kwa hali yoyote sehemu yoyote ya mtu za mishipa ya hisia za mihemko ni uvunjaji na ukosefu wa sharti la hijabu maana kufanya hivyo huibua mihemko kwa mshikwaji na mshikaji labda kama ni walemavu wa mishipa ya hisiya za mihemko
Hukmu ya hijabu

Hijab ni faradh kwa wanawake na wanaume katika Uislamu walio fikia umri wa balegh
Ewee mtume waambia waumini wa kike wateremshe macho yao (wanapo tembea njiani) pia wahifadhi tupu zao pia wasidhihirishe mapambo yao ( kwa wasiokuwa maharimu zao). Isipo kuwa mapamba yasio epukika kuonekana (viganja vya mikono na miguu) ...
Suratun Nuur 31 Umuhimu wa hijabu kwa walimwengu
Utakasa wa mioyo ya wanaume na wanawake ili kuepuka mawazo na minong'ono ya mashetani.
Utakaso wa mioyo ya wanaume na wanawake ili kuepuka mawazo na minong'ono ya mashetani.
Kuonyesha usafi wa mwanamke wa Kiislamu, na kutupilia mbali mashtaka na tuhuma dhidi yake.
Kulinda wanawake na macho ya waovu na wadhaifu wa imani.
Kuimarisha uhusiano wa kifamilia, na kuimarisha uhusiano wa ndoa kati ya wanandao, na kati ya wanawake na familia zao.
SEHEMU NYETI ZA MWILI ZENYE KUIBUA SHAHAWA ZA WANADAMU
Wanamke kwa wanaume wanazo baadhi ya sehemu za miili yao ambazo ni kichocheo kikubwa katika kuibua haya ya kujamiiana. Sehemu hizo ni kama zifuatazo:
1. kwa wanawake, kiukweli ni kwamba mwili wote wa mwanamke ni kivutio kwa wanaume ila wachache walio pungukiwa na shahawa kuliko wengine, ndio maana vikaweko vitendo vya kubakwa wanawake katika maeneo tofauti duniani. Hata hivyo zipo sehemu ambazo ni nyeti katika kumvutia mwanaume, kama tunavyo zitaja hapo chini.
makalio
matiti
hipsi
macho
sauti
uke au mchoro wa uke katika nguo alizo zivaa.
2. kwa wanaume, uhalisia ni kwamba wanawake pia huvutiwa na wanaume ingawa vitendo vya kubakwa wanaume ni vichache sana duniani kuliko kubakwa wanawake, sababu kuu ni kuwa sio mwili wote wa mwanaume ni kivutio na kichochezi cha shahawa kwa wanawake. Hapa chini tunataja baadhi ya sehemu
kifua
macho
uume au mchoro wa uume katika nguo alizo zivaa.
Sehemu tajwa hapo juu ni lazima kwa anaye muugopa MOLA wake, ajitahidi sana kuto kudhihirisha sehemu hizo kwa yeyote asiye kuwa mwenza wake wa ndoa maana anaweza kuwa ni kisababishi cha zinaa, japo kwa mtu mwengine asiye kuwa yule aliye ziona sehemu hizo.
Ni vigumu sana ukweli kupotezwa, suala la sehemu hizo kuwa ni kichocheo kikubwa cha zinaa linaweza kukanushwa na baadhi ya watu dhahiri shahiri, kwa wakati huo huo wakiwa waelewa kuwa ukweli ni kinyume na madai yao. Sasa iwapo sehemu hizo kuonekana ni sababu ya kuibua shahawa, kuguswa sehemu hizo kwa mpapaso ni hatari zaidi kuliko kutizamwa.
Hivyo kunahaja ya kutambua kuwa mmoja wetu anaweza kuvaa nguo za stara na staha, lakini akaikosa au akaipoteza hijjabu kwa sababu tu ya mipapaso atayo papaswa.
VIDEO HII NI MOJA YA VIFAA KAZI VYA KUSOMESHEA SOMO LA UKOSEFU WA HIJJAB, KWA MATENDO
Mara zote ikitokeza msongamano wa watu katika vyombo vya usafiri au popote, hupelekea masharti ya hijjab kupotea na hijjab kutokuwepo punde tu masharti yanapo kosekana. Mwanamke huyo katika video kuliani hapo, tujalie angelikuwa kavaa kidini ipaswavyo basi angekuwa amesha poteza masharti ya hijah na kumpelekea kulingana na wengine walio kuwa hawakuvaa hijab kwa sababu ya mipapaso aliyo papaswa. vile vile wapapasaji na wao wange kuwa tayari wamesha vunja mipaka yao ya staha na staha kwa sababu ya mipapaso walio ifanya kama inavyo onekena katika video hapo.
HIJJAB NA VYOMBO VYA USAFIRI
ufalisia wa lengo la hijabu ni kuondoa mizizi ya zinaa katika jamii
Comments