TEHAMA NA ATHARI ZAKE KATIKA MAISHA YA KILA SIKU
- Gshtargets
- Mar 9, 2022
- 27 min read
Updated: Jan 13, 2023
MLANGO WA KWANZA : NADHARIA
Kwa nini watu wengi wanaosoma matumizi ya kompyuta, hawana uelewa halisi kuhusu undabi wa faida za tehama na mambo ambayo hufanyika kwa kutumia kompyuta?
Suali hili nimekuwa ni kijiuliza sana na kuwashirikisha baadhi ya walio pitia taaluma ya tehama.
Sasa katika makala haya tunalenga yafuatayo:
Kutoa ufafanuzi wa kina ili kila mmoja kati ya watakayo soma Makala haya wabainikiwe umuhimu ya maarifa ya matumizi ya Tehama katika maisha ya kila siku,
Kutoa ufafanuzi kuhusu historia ya tehema na michango tofauti ya kitaaluma walio itoa wasomo katika kuifikisha Tehama ilipo leo,
Kutoa maarifa ya kina na machache kiasi kuto kumchosha msomaji lakin faida kubwa sana itapatikana kwa msomaji wa Makala,
Kutoa mukhtasari wakutosheleza kuhusu faani kadha za za kompyuta kupitia:
Historia na kukuwa kwa kompyuta,
Utangulizi wa matimizi ya maarifa ya kompyuta,
Ukarani na sekreteriati,
Mtandao,
Utunzaji wa nyaraka na vielelezo …Nk.
UTANGULIZI
Kama wahenga wanavyo sema " kila zama na kitabu chake " wakiwa na maana kwamba zama hazilingani katu na kila zama huwepo mambo fulani yanayo shamiri katika matumizi kuliko kinyume na zama nyengine.
Haito pingika kuwa tehama ina mchango mkubwa katika kumuendeleza mwanadamu zama hizi kukilo kitu kinginecho. Suala la ujuzi au ukosefu wa ujuzi wa matumizi ya tehama, ikiwa bado haija dhihiri athari yake katika jamii, basi miaka michache ijazo kutakuwa na usumbufu sana kwa mtu asiye na maarifa ya matumizi ya tehama.
(Picha namba 1)

karni ya 20 ilikuwa majengo ya maktaba ndio marejeo makuu katika kujiendeleza kielimu, leo mambo yamebadilika mnoo kiasi ukitembelea majengo hayo uatayakuta hayana watu wanaosomo zitabu zaidi ya watumishi majengoni hapo. Hata watunzi wengi wa vitabu wamebadili namna ya uuzaji wa vitabu vyao. Badala ya uuzazi wa mfumo wa amali sasa hivi wauza vitabu kupitia mtandano, bali vitabu vinge hivi sasa havipo tene katika mfumo ya kitabu cha kuguswa kwa mikono. Yaani uwezekano wa kusoma vitabu sasa hivi umeshika kasi kubwa kusoma kupitia tehama ( simu au kombiuta). Uuzaji bidhaa duniani na kuhifadhi kumbukumbu muhimu za watu imekuwa ni kwa njia ya mtandao.
Kwa mukhtasari ya ufupicho wa athari za maarifa ya matumizi ya tehama, tulio uelezea hapo juu, bila shaka wewe msomaji utabainikiwa umuhimu wa maarifa ya matumizi ya tehama kwa kila mmoja maishani mwake. Kutokana na umuhimu huo tulio uona sisi tumependelea kusomesha tehama kupitia tovuti yetu hii kwa kufunza misingi ya utumiaji wa kompyuta kwa lugha ya kiswahili ili kupunguza changamoto kwa wasio jua lugha ya kiingereza maana hakuna ulazima kompyuta kusomeshwa kwa lugha ya kiingereza katika jamii ya watu wasio zungumza kiingereza. Hata hivyo bado changamoto itakuwepo kidogo maana kumpyuta huwasiliana na mtumiaji kwa lugha isio kuwa ya kiswahili. Katika makala hii tumetumia njia rahisi sana za kusomeshea ili kuwawekea wepesi wazito wa kuelewa darasani. Tunaamini kuwa msomaji wa makala hii atakubaliana nasi kuhusu mbinu tulizo zitumia katika kuyaandaa makala haya.
Tunashauri walio na uwezo au ushawishi watumie uwezo wao au ushawishi wao ili kupatikana mifumo inayo endesha kombiuta kwa lugha ya kiswahili kiasi cha mtumiaji mswahili kuondokea ya changamoto ya mawasiliano na kombiuta kwa lugha ya kiingereza
SEHAMU YA KWANZA: KOMBIUTA - historia, vizazi na mapinduzi ya kompyuta
Kombyuta ni nini?
Mashine inayoweza kupangwa ambayo hufanya uchakataji wa kasi ya juu sana wa nambari, pamoja na maandishi, michoro, alama na sauti uchakataji azioweza kuufanya mwanadamu kwa ufanisi na kiurahisi. Kompyuta zote zina kitengo cha uchakataji cha kati ambacho hutafsiri na kutekeleza maagizo; vifaa vya kuingiza, kama kibodi na panya, ambayo data na amri huingia kwenye kompyuta kwa kutumia vifaa tajwa; kumbukumbu inayowezesha kompyuta kuhifadhi programu na data; na vifaa vya kutoa, kama vile vichapishi na skrini za kuonyesha, vinavyoonyesha matokeo baada ya kompyuta kuchakata data. Hiyo ni moja ya maana zinazo tambulisha kombyuta.
Kompyuta ni mashine ya kielektronia yenye madhumuni ya jumla ambayo huchakata data kulingana na seti ya maagizo yaliyohifadhiwa kwa muda ndani yake. Kompyuta na vifaa vyote vilivyounganishwa nayo ni "hardware." Maagizo yanayoiambia kompyuta nini cha kufanya ni "programu."Programu inayodhibiti kompyuta inaitwa "mfumo wa uendeshaji kwa kiingereza operating system", na programu inayoingiza, kuchakata na kutoa data ya mtumiaji inaitwa "programu," kwa kiingereza Applications au App. Leo, kompyuta hufanya kazi ambazo zamani zilikuwa ngumu zaidi. Kwa mfano, unaweza kuandika herufi katika kichakataji maneno, kuihariri wakati wowote, kukagua tahajia, kuchapisha nakala na kuituma kwa mtu kote ulimwenguni kwa sekunde. Shughuli hizi zote zingechukua mtu siku, kama si miezi, kufanya kabla. Pia, mifano hii ni sehemu ndogo ya kile ambacho kompyuta inaweza kufanya.
Ugunduzi, kukuwa na mwendelezo wa tehama.
Nani mtu wa kwanza kugundua kompyuta?
Hakuna jibu rahisi na halisi kwa swali hili kwa sababu ya uainishaji tofauti wa kompyuta na vizazi vyake. Uhalisia wa kugundulika kwa kompyuta na kukuwa kwake katika hali ya muundo, na mfumo wa utendaji wa kompyuta hadi leo hii Ferbruari 2022, kumechangiwa na watu wengi sana kutoka jamii tofauti na mataifa tofauti duniani kinyuma na wanavyo dhania watu wengi, jambo linalo pelekea kuto kutajwa au japo kuteuliwa jina la mtu maalumu na kuenziwa kuwa yeye ndiye aliye igundua kompyuta. Kwa muktadha ya tulio yaeleza hivi punde tunatoa hapa mukhtasari ... na tunatoa taswira ya walio fanya juhudi toka kugunduliwa hadi leo hii:
KWANZA.
(Picha namba 2)

Abuu abdillah Muhammad bin musa alkhawazismiy aliye zaliwa karni ya nane
( mwaka 781 ) nchini iraq zama hizo na ndio iliko nchi husika katika ramani ya dunia ya leo. Muhammad musa bin musa alikuwa ni msomi mkubwa katika zamazake, alitunga vitabu vingi sana katika faani kadhaa za sayansi. moja ya vitabu vyake ni kitabu alicho kiita ALJABRA WAL MUQABAH katika kitabu hicho alikuwa ni msomi wa kwanza duniani kubainisha ndani yake misingi ya naina tofauti za hesabu na kutenganisha rasmi ALGEBRA kuwa ni somo kando ya masomo mengine ya kihesabu. Katika kitabu chake tajwa hapo juu alikuwa ni msomi wa kipekee aliye gundua ALGORITHM ndinu maalumu inayo weza kutumiwa katika utatuzi wa masuala tofauti yanayo mkabili mwanadamu maishani kwake. Baadha ya miaka 300 kitabu husika kikaanza kufundishwa duniani kote katika vyuo vikuu vyote. katika karni ya 20 iliopita alijitokeza msomi muingereza ALAN TURING kutumia rasmi ALgorithm katika mfumo wa utendaji wa kompyuta, jambo lililo kuza umaarufu wa mashine za kompyuta duniani na kuifanya kompyuta kuingizwa katika maisha ya mwanadamu popote alipo katika kila nyanza. Pamoja na kwamba Muhammad Bin Mussa hakutengeneza mashine yoyote ila leo dunia imekuwa yamtuja kuwa yeye ndiye muanzilishi wa kompyuta maana leo hii kati zote zinazo tekelezwa na kompyuta hutumia mfumo wa ALGORITHM katika utendaji na utekelezaji.
PILI
(Picha namba 3)

Katika umri wa miaka 18 Blaise Pascal mfaransa, alianza kufikiria juu ya mashine ya kuchakata hesabu za kujumlisha na kutoa, ikiwa nj wazo la kumsaidia baba yake, ambaye aliteuliwa kuwa msimamizi huko Haute Normandie, na dhamira ya kurejesha hadhi ya ukusanyaji wa mapato ikiwa ni agizo la ukusanyaji wa mapato ya ushuru kwa weledi wa hali ya juu nchini Ufaransa. Mnamo mwaka 1645, Baise Pascal aliunda mashine ya kwanza ya kufanya hesabu duniani. mashine hiyo yaitwa PASCALINE. La pascaline huzingatiwa kuwa ndio "mashine babu" ya kompyuta tunayo itumia zama zetu za sasa. Yaani lau kompyuta zinge kuwa na nidhamu ya kizazi, basi mashine Pascaline ndio ingekuwa ndio ilio zaa kompyuta zote za duniani.
TATU
(Picha namba 4)

Ilikuwa kati ya 1847 na 1849 ambapo Charles Babbage alianza kutumia maendeleo ya kiteknolojia ya injini yake ya uchanganuzi kuunda mipango ya injini ya tofauti nambari 2 ambayo, kwa maelezo sawa, ilihitaji sehemu mara tatu chache kuliko ya awali. Hivyo kompyuta ya kwanza ilikuwa ni ya kiufundi, haifanani na ambayo watu wengi wanaweza kufikiria kuwa kompyuta leo. Kwa hivyo, ukurasa huu unatoa uorodheshaji wa kila kompyuta kwanza, kuanzia Injini ya Tofauti na kuelekea kwenye kompyuta tunazotumia leo. Pia alikuwa wa kwanza kuelezea kanuni ya kompyuta mnamo 1834, wakati wa uzinduzi wa mashine ya kuhesabu ili kusudia kuhesabu na kuchapisha kanuni za hesabu. Hakuwahi kukamilisha injini yake ya uchanganuzi, lakini alitumia maisha yake yote kuiunda kwa maelezo madogo kabisa na kuunda mfano. Mmoja wa wanawe alijenga kitengo cha kati (kinu) na printa mnamo 1888 na alitoa onyesho lililofanikiwa la kompyuta ya mezani katika Chuo cha Royal cha Astronomy mnamo 19081.
Mnamo 1991, kutokana na mipango hii, tuliweza kuunda upya sehemu ya mashine hii ambayo inafanya kazi kikamilifu kwa kutumia mbinu ambazo zilipatikana katika karne ya 19, ambayo inaonyesha kwamba inaweza kujengwa wakati wa maisha ya Charles Babbage.
NNE
(Picha namba 5)

ENIAC (kifupi cha msemo wa Kiingereza Electronic Numerical Integrator And Computer) ilikuwa mwaka wa 1945 kompyuta ya kwanza kamili ya kielektroniki ambayo inaweza kuwa Turing-complete. Inaweza kupangwa tena kutatua, kimsingi, shida zote za hesabu.
Ilitanguliwa mwaka wa 1941 na Z3 ya Ujerumani, mashine inayoweza kupangwa lakini bado ya umeme (matumizi ya relays), na mfululizo wa British Colossus wa kompyuta. Kompyuta iliitwa ENIAC. Ilitengenezwa na JOHN WILLIM MAUCHLY wakati wa Vita vya Kidunia vya pili (1943-1946) na iliundwa kusaidia kuhesabu hesabu zinazofanywa na ubongo wa binadamu. Kwa kufanya mahesabu haya kwenye kompyuta, wanaweza kufikia matokeo kwa haraka zaidi na kwa makosa machache.
Kompyuta za awali kama vile ENIAC zilitumia mirija ya tube na zilikuwa kubwa (wakati fulani ukubwa wa chumba au nyumba kabisa) na zinapatikana tu katika biashara, vyuo vikuu au serikali. Baadaye, kompyuta zilianza kutumia transistors na sehemu ndogo na za bei nafuu ambazo ziliruhusu mtu wa kawaida kumiliki kompyuta.
TANO
(Picha namba 6)

Mfumo wa uendeshaji wa kwanza (OS) uliundwa mwanzoni mwa miaka ya 1950 na ulijulikana kama GMOS kifupisho cha General Motors Operating System. General Motors walitengeneza mfumo wa uendeshaji wa kompyuta ya IBM.Kompyuta asili za programu zilizohifadhiwa ziliratibiwa moja kwa moja na opcode za msimbo wa mashine. …mfumo wa kwanza wa uendeshaji undwa na Microsoft haukuitwa Windows, uliitwa MS-DOS kifupicha cha Microsoft Disk Operating System, na undwa mnamo mwaka wa 1981 kwa kununua mfumo wa uendeshaji wa dos 86 kutoka kwa bidhaa za kompyuta zilizosakinishwa na kuurekebisha ili kukidhi mahitaji ya IBM. Mnamo miaka ya 1990 BILL GATES na kampuni yake waka irekedisha MS-DOS na kutoa WINDOWS ilio mbadili BILL GATES kuwa bilionia wa kwanza na wakipekee duniani kwa kipindi kikubwa mnoo bila ya kuvunjwa rekodi husika.
VIZAZI VYA TEHAMA NA MAPINDUZI YAKE
Kila kizazi cha kompyuta kimeleta maendeleo makubwa katika kasi na uwezo wa kazi za kompyuta. Jifunze kuhusu kila moja ya vizazi vitano vya kompyuta na maendeleo makubwa ya teknolojia ambayo yamesababisha teknolojia ya kompyuta tunayotumia leo. Historia ya ukuzaji wa kompyuta ni mada ya sayansi ya kompyuta ambayo mara nyingi hutumiwa kurejelea vizazi tofauti vya vifaa vya kompyuta. Kila kizazi cha kompyuta kina sifa ya za kipee za maendeleo ya kiteknolojia ambayo kimsingi hubadilisha jinsi kizazi fulani cha kompyuta kinavyofanya kazi tofauti na kizazi kinginecho. Maendeleo makubwa zaidi kutoka miaka ya 1940 hadi leo yamesababisha mashine ya kompyuta kuwa ndogo zaidi kimizani, bei nafuu, zenye nguvu zaidi na bora, na hivyo kupunguza uhifadhi na kuongeza uwezo wa kubebeka ukilinganisha na miundo ya kompyuta za awal.
kizazi cha kwanza (1940-1956)
(Picha namba 7)

Kompyuta za kizazi cha kwanza zilitegemea lugha ya mashine, lugha ya programu ya kiwango cha chini zaidi inayoeleweka na kompyuta, kufanya shughuli, na zilikuwa zatatua tatizo moja kwa wakati mmoja yaani utendaji wa jambo moja tu . Ilikuwa yawachukua waendeshaji siku njima au hata wiki kuanzisha jambo jipya, zilikuwa zatumia umeme mwingi sana jambo lililo pelekea juwe na joto kali na la kupingukia. Ilikuwa katika kizazi hiki kwamba usanifu wa Von Neumann ulianzishwa, ambao unaonyesha usanifu wa kubuni wa kompyuta ya digital na elektroniki. Baadaye, kompyuta za UNIVAC na ENIAC, zilizovumbuliwa na J. Presper Eckert, zikawa mifano ya teknolojia ya kompyuta ya kizazi cha kwanza. UNIVAC ilikuwa kompyuta ya kwanza ya kibiashara iliyotolewa kwa mteja wa biashara, pia Ofisi ya Sensa ya Marekani mwaka wa 1951.
Kizazi cha pili TRANSISTORS (1956–1963)
(Picha namba 8)

Ulimwengu ulishuhudia transistors kuchukua nafasi ya mirija ya utupu katika kizazi cha pili cha kompyuta. Transistor iligunduliwa katika Bell Labs mnamo 1947 lakini haikuwa na matumizi mengi kwenye kompyuta hadi mwishoni mwa miaka ya 1950. Kizazi hiki cha kompyuta pia kilijumuisha maendeleo ya vifaa kama kumbukumbu ya msingi ya sumaku, mkanda wa sumaku, na diski ya sumaku. Transistor ilikuwa bora zaidi kuliko bomba la utupu, ikiruhusu kompyuta kuwa ndogo, haraka kufanya kazi, bei nafuu, isiyo tumia umeme mwingi, na ya kuaminika zaidi kuliko zilizo tangulia, za kizazi cha kwanza. Ingawa transistor bado ilitoa joto nyingi ambalo lilisababisha kompyuta kuharibika mara kwa mara. Kompyuta ya kizazi cha pili bado ilitegemea kadi zilizopigwa kwa ingizo na uchapishaji wa matokeo. Kompyuta za kizazi cha pili zilihamishwa kutoka lugha ya mfumo wa binary hadi lugha za ishara, au kusanyiko, jambo ambalo liliwaruhusu watayarishaji programu kubainisha maagizo katika maneno. Lugha za kiwango cha juu za programu pia zilikuwa zikitengenezwa kwa wakati huu, kama vile matoleo ya awali ya COBOL na FORTRAN. Hizi pia zilikuwa kompyuta za kwanza ambazo zilihifadhi maagizo yao katika kumbukumbu zao. Kompyuta za kwanza za kizazi hiki zilitengenezwa kwa tasnia ya nishati ya atomiki.
kizazi cha tatu (1964–1971)
(Picha namba 9)

Uendelezaji wa mzunguko uliounganishwa ulikuwa alama ya kizazi cha tatu cha kompyuta. Transistors zilidogoshwa na kuwekwa kwenye chips silicon, inayoitwa semiconductors, ambayo kwa kiasi kikubwa kuongeza kasi na ufanisi wa kompyuta. Kompyuta, kwa mara ya kwanza, zilipatikana kwa hadhira kubwa kwa sababu zilikuwa ndogo na za bei nafuu kuliko zilizo tangulia.
Kizazi cha nne MIkroprosesa (1971–SASA)
(Picha namba 10)

Microprocessor ilianzisha kizazi cha nne cha kompyuta, kwani maelfu ya saketi zilizojumuishwa zilijengwa kwenye chip moja ya silicon. Teknolojia ya kizazi cha kwanza iliyojaza chumba au nymba nzima sasa ilitosheleza kwenye kiganja cha mkono. Chip ya Intel 4004, iliyotengenezwa mwaka wa 1971, iliunganisha vipengele vyote vya kompyuta, kutoka kitengo cha uchakataji cha kati na kumbukumbu hadi udhibiti wa pato, kwenye chip moja. Mnamo 1981, IBM ilianzisha kompyuta yake ya kwanza ya kibinafsi kwa mtumiaji wa nyumbani, na mnamo 1984 Apple ilianzisha Macintosh. Vichakataji vidogo pia viliondoka kwenye eneo la kompyuta za mezani na kuingia katika maeneo mengi ya maisha huku bidhaa nyingi zaidi za kila siku zilianza kutumia chip ya microprocessor. Kadiri kompyuta hizi ndogo zilivyokuwa na nguvu zaidi, zinaweza kuunganishwa pamoja na kuunda mitandao, ambayo hatimaye ilisababisha maendeleo ya mtandao. Kila kompyuta ya kizazi cha nne pia yalidhihiri kwake maendeleo ya kompyuta ya GUIs, kipanya, na teknolojia ya mkono. Microprocessor ya kwanza ya Intel, 4004, undwa na Ted Hoff na Stanley Mazor.
Kizazi cha tano AKILI BANDIA (YA SASA NA ZAIDI)
(Picha namba 11)

Teknolojia ya kompyuta ya kizazi cha tano, kulingana na akili ya bandia, bado inaendelezwa, ingawa kuna baadhi ya programu, kama vile utambuzi wa sauti, ambazo zinatumika leo. Matumizi ya uchakataji sambamba na superconductors husaidia kufanya akili ya bandia kuwa ukweli. Hiki pia hadi sasa ni kizazi kikuu cha kupakia kiasi kikubwa cha hifadhi kwenye kifaa cha kubana na kubebeka. Uhesabuji wa kiasi na molekuli na nanoteknolojia itabadilisha sana uso wa kompyuta katika miaka ijayo. Madhumuni ya kompyuta ya kizazi cha tano ni kuunda vifaa ambavyo vitajibu kwa uingizaji wa lugha asilia na vinaweza kujifunza na kujipanga. kizazi hiki cha tano ndio kizazi cha kompyuta ndogo sana kuliko zote na kompyuta ya mapajani hadi kiasi cha mtumiaji kuweka katika mfuko wa suruali yake alio ivaa. Hapo tumeashiria simu janja za viganjani.
SEHEMU YA PILI: KOMPYUTA - vifaa na utendaji wake
Kompyuta imegawanyika sehemu nyingi, na vigawanyiko hivyo huwa tofauti kwa kuzingatia makusudio ya mtu na mtu. hapa sisi tunafupisha na kusema kompyuiuta ina vigawanyiko viwili vikuu tukizingatia mpapaso ( kugusa ). Vigawanyiko vyenyewe ni kama vifuatavyo:
a) HARD WARE
b) SOFT WARE
PART ONE HARD WARE
Hard ware kila device. Device ni kifaa chochote cha kielektronia ninacho jitegemea kwa matumizi.
Mfano: speaker
morinitor (kioo)
mouse ... Nk.
Yaani yoyote kwenye kombiuta ni hard ware ingawa sio kila hardware ni device.
Hardware ni nini ?
Hard ware ni kifaa chochote cha kombiuta ambacho tunaweza kukigusa na kukipapasa kwa mikono yetu.
Device kuu za computer ni kama zifuatazo:
mouse
keyboad
monitor
central processing unity (CPU)
(Picha namba 12)

DEVICES NA KAZI ZAKE KATIKA KOMPYUTA
maana ya device
device ni kifaa chochote cha kompyuta kinacho jitegemea katika matumizi.
mfano: mouse, keyboard, monitor, CPU, printer, kamera, maikrofone ... Nk.
1. MOUSE: Kazi yake yatusaidia mawasiliano na CPU (High light na select) Mouse ina sehemu kuu 2:
i).Left kazi yake ni kuselect na kuhigh light
ii).Right kazi yake kutupa menu ili tuchague kitu gani tunataka processor atufanyie.
Kuna aina 3 za mouse kama zifuatazo:
- Build mouse
- External mouse
- wireless mouse
2. KEYBOARD: Kazi yake inatusaidia kuwasiliana na CPU kwa kumuambia tunachokitaka atufanyie na akatuelewa yeye CPU.
Keyboard ina button zilizo megawanyika makundi mawili kama yafuatayo:
1)function keys ni button anazotumia fundi tu zilizo baki ni keys za kawaida tusome baadhi :
- Ctrl (control key) : husaidia wakati wa kutaka kuweka vivuli kwenye files zaidi ya moja.
- Tab: kazi yake hamisha cancer toka chumba kwenda chumba kingine
- Enter: kazi yake ni kumkubalia CPU alichokifanya kuwa yupo Sahihi au kukubali ujumbe unaotumwa na kombiuta.
- Capslock: Kazi yake ni kubadika herufi ziwe kubwa au ndogo
- Shift: Ni kutuhamisha kutoka mfumo hadi mfumo mwingine au kuandika alama za juu ya herufi katika keyboard.
- space bar: kazi yake ni kuweka mwanya au nafasi baina ya neno na neno.
3. MONITOR: COMPUTER za zamani za viwandani zilikua hazitumii monitor.Kazi ya monitor ni kutuonyesha vilivyomo ndani ya computer na vinavyofanyika kwa wakati husika au kutuonesha jambo kutulo liamuu kumbiuta kulitekeleza.
4. CPU BOX: Ni device iliyobeba ndani mwake devices nyenginezo (RAM, Hard disc, processor ... Nk.
ANGALIZO: Device tulizosoma hapo juu ndio device kuu za computer, devices nyengine ambazo hatukuzisoma hapa ni ACCESORIES DEVICES yaani sio za mzingi kiasi hicho katika utendaji. Ziwepo au zisiwepo kombiuta itafanya kazi bila wasiwasi kabisa.
Mfano: speaker
camera
printer
scanner
microphone ... Nk.
BAADHI YA MISAMIATI INAYO TUMIWA KATIKA MAARIFA YA MATUMIZI YA KOMBIUTA
DEFAULT: Maana yake uasilia wa jambo katika device
BACKSPACE: ni kufuta herufi au neno lilioko kabla ya cansor
MOUSE POINTER: ni kiashiria cha device mouse kinacho onekana desktop au sehemu ya kufanyia kazi katika application
CANSOR: ni hiyo mouse pointer badilika kuwa mfano wa kimstari ninacho cheza katika working space.
FILE: maana yake kumbukumbu zetu tulizo ziweka katika kombiuta. File hutengenezwa kwa kutumia application maalumu inayo husu aina ya file husika.
SELECT: maana yake wela kivuli sehemu maalumu unayo taka kuiwekea marekebisho katika file, maana nyengine ni weke kivuli kwenye file unalo taka kulihamisha au kulifuta au kulinakili.
HIGHLIGHT: ina maana moja na select iliopo hapo juu. Hutumiwa kwa kushindilia upande wa kulia wa mouse , kwa wakati huo huo tukiwa tuna drag. Rangi ya bluu itaingia sehemu husika
EDIT: badili au rekrbisha, hutumika backspace key au delete key, bila shaka ulazima wa ku-highlith upo hasa tunapo tumia delete key.
BACK: rudi utokako
FORWARD: songa mbele,
WORKING SPACE: sehemu inayo onekana punde tu kuifungua application/programu yoyote ili tuanze kuweka tunayo yahitaji au kuweka kumbukumbu zetu.
RESTORE: ni kurejesha file lililofutwa
SAVE: hifadhi kumbukumbu zangu nilizo zitengeneza au nilizo ziwekea mabadiliko
DELETE : futa.
MINIMIZE: ina maana lifanye dirisha kuwa ndogo
MAXIMIZE: ina maana maana lifanye dirisha kuwa kubwa
CLOSE : ina maana lifunge dirisha
DIALOG BOX: maana ni box fulani hutokeza wakati kombyuta yawasiliana na mtumiaji kwa kumhiyarisha kuchangua moja au baadhi ya mambo kadhaa.
COPY: maana yake nakili
CUT: maana yake kata ili uhamishe kwenda sehemu nyengine.
PASTE : maana yake bandika ulicho kinakili au ulicho kihamisha
ACTIVE : ni hali ya menu kuingia kivuli tunapo ziwekea mouse pointer
INACTIVE: ni hali ya menu kuto kuingia kivuli tunapo ziwekea mouse pointer
DESKTOP: ni kombyuta ya mezani asiyo tembea nayo mtumiaji bali huiacha mezani. maana nyengine ya desktop ni moja ya folders za asili zinzzo kufa katika operating system kazi yake ni kushikilia programms icons zilizomo katika kombyuta.
NADHARIA YA LOCATION
Location ni nini ?
kwenye elimu ya computer sehemu yoyote tutakoweka file zetu ndipo panapoitwa location. Location hupatikana katika hard disk, na hard disk inawezo kuwa imegawanyika sehemu zaidi ya moja au ikawa na sehemu moja tu, hizo sehemu ndizo zinayobeba location kwa wakati husika.
hard disk inapo gawanywa hizo sehemu huitwa partion, na partion nazo zinaweza kuwekewa mafaili ndani yake na mafolder tofauti.
Picha hii yatuonesha location ikiwa ina mafolder ya rangi ya jano pamoja na mafaili moja wapo limewekewa kivuli cha rangi blu.
Picha hapo chini yaonesha "file location" au working window iliyo funguka nusu bila kujaza csreen nzima.
(Picha namba 13)

NADHARIA YA FOLDER
Folder ni nini ?
Katika kompyuta, folda ni mfuko au eneo pepe la kuhifadhiaau kuwekea programu, hati, data au folda zingine ndogo. Folda husaidia kuhifadhi na kupanga faili na data kwenye kompyuta. Sehemu yoyote tunayo hifadhia vitu ndani ys kompyuta, isio kuwa partion basi ni folder .Folder, files na partion za hard disci nazo hupewa majina kama ila tu majina ya partion yana kuwa kwa herufi kubwa na operating system ndio inayo fanya kazi ya kuainisha majina ya partion
mfano:
C, D, E
Hivyo hard disk ni location iliyo babeba partion na partion ni location iliyo bebe mafolder na folder ni location ilio beba mafaili, ingawa mafaili yanaweza kuwa katika partion bila kuwemo katika partion..
ANGALIZO
kawaida kompyuta ina hard disk moja tu halafu hiyo hard disk ndio inaweza kuwekewa partion tofauti pia sio vibaya hard disk ikawa na partion moja .
Tunapo unda file lolote ni lazima kabla ya kila jambo tuwe limesha amua ni katika location gani tutapo hifadhi faili husika
Faili lolote tunapo liunda ni lazima tuamue location gani tutako liweka.
Faili lolote tusilo lichagulia location hulazimika kukaa katika location tuliko save faili jengine hapo awali kwa mara ya mwisho au litajiweka Mydocuments
HATUA ZA KUTIZAMA PARTION
1) start menu
2) chagua icon iitwayo this pc (my computer)
3) right click kutumia mouse, chagua open
hatua ya tatu ina njia mbili.
Njia ya pili ni start menu chagua icon this computer left click mara mbili itafunguka na utaona partions.
(Picha namba 14)

inapo funguka yawezekana ikafunguka dirisha kamili au dirisha nusu kama inavyo onekana katika picha hapo juu (Picha namba 13). itapo funguka na ikajaza screen yote ina maana dirisha kamili limefunguka na ikifunguka nusu haikujaza screen nzima ina maana nusu dirisha ndio lililo funguka . Hali ikiwa hivyo ni wajibu wetu kulifungua dirisha kamili .
minimizing ni kufungua dirisha nusu
maximizing ni kufungua dirisha kamili
closing ni kufunga dirisha
PART TWO SOFT WARE
SOFT WARE ni mifumo usiyo wezekana kuguswa inayo msaidia mwanadamu kuitumia hardware ya kombiuta. Yaani Soft ware ni kitu chochote kwenye kombiuta tunaweza kukiona na lakini hatuwezi kukigusa kwa mikono.
Soft ware yoyote kuiona kwetu ni kupitia monitor, yaani tukikiona kitu kupitia macho yetu bila kupitia monitor ni hard ware,hapa tutasoma baadhi ya soft ware tu.
Kuna aina mbili kuu za software kama zifuatazo:
1. OPERATING SYSTEM
2. APPLICATIONS
1. OPERATING SYSTEM
Oparating system ndio soft ware mama inayotangulizwa kabla ya soft ware zote katika kombiuta. Operating system ndio inayowasiliana na hard ware kupitia processor ya kombiuta. Kombiuta inato kiwandani bila kuwa na soft ware yoyote mnunuzi ndiye anaeamua aweke oparating system ipi, na soft ware ipi maana kuna makabila mengi ya oparating system lakini zote zinafanya kazi moja ingawa zinazidiana utendaji.
Hata hivyo zipo oparating system maalum kwa jambo maalum.
2. APPLICATIONS
Applications ni nini?
Application ni software ndogo zinazo bebwa na oparating system. Applications hazilingani, kila applications ina kazi yake maalum kwa mambo maalum.
Mifano ya application: notepad
window media player ...
OPERATING SYSTEM NA KABILA ZAKE
Operating system pia nazo zimegawanyika makundi mawili makuu kama yafuatayo:
a. Client operating system au stand alone operating system, hii ni operating system inayo wekwa katika kombiuta iliyo tengwa kwa ajili ya kuongozwa wala sio kuongoza. ijulikane kuwa kuna kombiuta zinazo ongoza kombiuta nyengine katika mtandao. Yaani client inakuwa ni tegemezi itakapo unganishwa na computer nyinginezo katika mtandao.
Aina za client operating system:
XP
VISTA
WINDOW 7
WINDOW 8
WINDOW 10
MAC O.S (apple )
ANDROID (simu)
b. network operating system (N.T, hii oparating system ikiingizwa kwenye kombiuta, kombiuta husika huwa na uwezo wa kuziongoza kombiuta nyenginezo mtandaoni. Yaani kombiuta hii ndio huzingatiwa kuwa ndio kombiuta kiongozi wa kombiuta nyengine mtandaoni.
Tumesoma hardware (devices) pamoja na software. Mbali na hivi vitu viwili tulivyovisoma zimo nywaya (cables) hatujaziashiria nywaya hizo.
Cables zimegawanyika makundi mawili kwa mujibu wa kazi zake, kama ifuatavyo:
1. ELECTRICAL CABLES hizi kazi yake ni kupeleka umeme kwenye divices ili devices zifanye kazi.
2. DATA CABLES Kazi yake ni kuhamisha kumbukumbu kutoka device moja kwenda nyingine.
kanuni muhimu ya kujua:
data cable yeyote lazima iwe na electricale cable jirani kwa maana kila data cable lazima inayo electrical cable.
PART THREE OPARATING SYSTEM.
UTANGULIZI
Oparating system ina vitu muhimu, kuna haja tuvijue ingawa sio lazima kuvijua vyote.
BAADHI VIONJO MUHIMU VYA KUJUA KATIKA OPERATING SYSTEM
Start boutton: ni sehemu ya kuwasha na kuzimia kombyuta yaan button ya on/off ya hardware. pia kuta start buton nyengine mbili:
operating system kazi yake ni kuzimia au kulaza au kubadili USER ,
kutupatia start menu. ndio aikoni inayo tusaidia kuingia katika operation system na kutizama application zilizomo ndani ya kompyuta. Tunapo bofya start button hutokeza start menu. start button ipo kushotoni kona chini kabisa ya screen/kioo. tumia mouse kuifungua. (Tizama picha ya bluu hapo chini)
Shut down: hii hutumika kwa alijili ya kulaza, kuzima kompyuta au kuhama toka akaunti ya mtumiaji kwenda akaunti nyengine. (Tizama picha ya bluu hapo chini)
Start menu ni button inayo :
tuonesha application zote zilizomo ndani ya kombyuta pia yatusaidia kutafuta file lolote tusiolijua sehemu lilipo
kazi yake inabeba icon za application zilizokuwepo ndani ya computer tunapo click start menu inatokeza menu bar. START MENU: Hii mara nyingi inakua kushotoni mwa monitor katika, huanenaka pindi imebofwa start button. ukipeleka mouse pointer na ukabofya start button unaweza ukaiona wazi START MENU. Kazi ya start menu ni kutuonyesha application zilizomo ndani ya kombiuta kupitia menu. Kila application imewakilishwa na icon yake maaalum ingawa sio kila icon ni application, maana kuna icon za folder na hali yakuwa folder sio application.(Tizama picha ya bluu hapo chini)
task bar: ina kazi mbili kazi mbili:
inatuonesha application zilizo funguka kwa wakati husika maana mtumiaji anaweza kufungua application zaidi ya moja.kazi,
kubeba application tunazo zihitaji mara kwa mara kwa sharti tumwambiee azibebe. Hii task bar hutumika kuazionesha applications zilizofunguliwa kwa wakati husika hata kama hazionekani maana zinaweka kufunguliwa zaidi ya applications moja kwa wakati mmoja na zikalazwa chini (minimized) zisionekana. kazi nyengine ni kuchikilia aikoni za applications tunazo zitumia mara kwa mara, ila kuzishikilia ni lazima tuamrisha kompyuta kufanya hivyo.(Tizama picha ya bluu hapo chini)
desktop; kazi yake ni kubeba program short cut icons na kuhifadhi mafaili pamoja na mafolda.
WORKING WINDOW AU " FILES' LOCATION " : hii hupatikana ikiwa tumesha ingia katika moja ya location yaliko mafaili na/au mafolda. Working window au files location huwa na alama tatu kuliani kona juu. Alama zenyewe huitwa:
minimize: lengo lake ni kulaza " file location " au working window
restore / maximize: lengo lake ni kurejesha mfumo wa ufunguaji wa " file location " au working window
close (Tizama picha nyeupe hapo chini)
PICHA YA FILES' LOCATION AU WORKING WINDOW
(Picha namba 15)

PICHA YA VIONJO VYA WINDOW
(Picha namba 16)

Application ni nini?
Application ni programu tunazozihitaji tunapotaka kufanya kazi mbali mbali, yaani kila aina ya jambo tunalo lihitaji kufanyiwa na kombiuta lina programu yake maalumu ina kila programu ina icon yake maalumu. Programu au application ikiondoshwa ndani ya computer icon yake inapotea pia.
Icon zinakaa kwenye desktop yaani yaletunayo yaona kwenye kioo tunapofungua kombiuta ndio huitwa. Icon pia zimegawanyika katika makundi mawili makuu, kama yafuatayo:
ICON za application (programs)
ICON za folder hizi mara nyingi huwa na rangi ya njano zenye muundo wa kitabu kilichofunguliwa hizi sio applications
ANGALIZO:
WORKING SPACE : hii hupatikana ikiwa tumesha fungua application/program. Working space huwa na alama tatu kuliani kona juu. Alama zenyewe huitwa:
minimize: lengo lake ni kulaza " file location " au working window
restore / maximize: lengo lake ni kurejesha mfumo wa ufunguaji wa " file location " au working window
close (Tizama picha hapo chini)
(Picha namba 17)

NADHARIA YA FILE (FAILI)
Filie ni nini?
Faili ni kitu kwenye kompyuta ambacho huhifadhi data, taarifa, mipangilio au amri zinazotumiwa kutengeneza programu fulani za kompyuta. Kwenye kompyuta kuna aina tatu za faili:
faili za programu,
faili za data na ,
faili za mfumo.
Katika GUI (GRAPHICS USER INTERFACE), kama vile Microsoft Windows, faili huonyeshwa kama aikoni . Pia kila programu huwa na aina maalumu za faini inazo zifungua yaani sio kila faili hufunguliwa kwa programu moja
Kwa mfano, aikoni zote za PDF huonekana kwa muundo ya sura moja katika kompyuta na zote ni sawa na hufunguliwa katika Adobe Acrobat au kisomaji kinachohusishwa na faili za PDF. Ikiwa programu inahusishwa na programu.
BAADHI YA PROGRAMU ZINAZO UNDA FILES ( MAFAILI )
kuna aina nyingi sana ya programu zinazo unda faili, bali huenda tukafa hata bila ya kuziona au kuzisikia aina nyenginezo za faili. Hivyo kwa muda huu tunaashiria chache na icon zake kama ifuatavyo:
1. Aikoni ya Notpad program
(Picha namba 18)

Application ya notpat huunda mafaili ya kabila la text tu yaani huunda mafail ya maandishi kama barua na uandishi wa vitabu ... Nk,
2. Aikoni ya Paint program
(Picha namba 19)

Application ya paint huunda mafaili ya kabila la picha tu yaani huunda mafail ya picha kama michorp na mistari na maua ... Nk,
UUNDAJI WA FILE
Tafadhali kumbuka kuwa computer haikubaali kubeba mafile zaidi ya moja yakawa na jina moja kwenye location moja. Hatua ni kama zifuatazo:
1) tafuta application husuka kupitia start menu ifungue.
2) weka vielelezo vyako (data au kumbukumbu) ukimaliza nenda hatua ya kuhifadhi hilo file.
3) kwenye menu ya application tafuta neno file click
4) weka jina la file (file name)
5) halafu click save as (save)
6) ukitaka kulitafuta file husika nenda my document
ADVANCED FILE SAVING
Tulipo soma application ya NOTPAD tulijifundisha kuhifadhi (save) vielelezo (data) vyetu. Hatua na njia tulizo zitumia ni njia za kijianafunzi tu. Sasa imefika wakati wakujifundisha njia ya ubobezi katika kuhifadhi data zetu katika "file". Njia zenyewe ni kama zifuatazo hapo chini:
1) baada ya kufungua application weka vielelezo.
2) ukimaliza kuweka vielelezo
3) nenda save as.
4) dialog box litakuja tafuta icon ya this pc.
5) double click icon ya this pc kwa left ya mouse chagua partion ulio ikusudia kuhifadhi data (file) zako.
6) double click partion husika itafunguka
7) utaona ndani mafolder chagua utakako weka file lako (au hii hatuaya 7 usiifanye rukia no 8)
8)click save
COPY_ CUT_PASTE
utangulizi;
kuna wakati mtu anahitaji kuwa na file lake moja katika location tofauti location (partition) E&D atakacho kifanya ni ku COPY PASTE, au mtu anaweza kuamua kuhamisha file lake kutoka location E kwenda D (CUT PASTE)
1. HATUA ZA KUCOPY
-Fungua location liliko file husika
-liright click file husika litaingia kivuli na menu itaonekana
-kwenye menu click copy
-halafu kafungue location unakopeleka file lako
-ndani ya location righ click menu itakuja click paste
2. HATUA ZA KUCUT
-fungua location liliko file
-right click file husika litaingia kivuli na menu itaonekana
-kwenye menu click cut
-halafu kafungue location unakopeleka file lako
-ndani ya location right menu itakakuja click paste
-tuliyo yaandika hapo juu yanahusu file zima (copy cut) likiwa halikufunguliwa yaani likiwa limefungwa, wala sio copy cut ya sehemu fulani ya file lililo funguliwa.
-Kuna wakati unataka kucopy au kucut sehemu maalumu ya file wala sio file zima hatua zina badilika kama ifuatavyo:
1) fungua file husika
2) ainisha sehemu husika kwa kuwekea kivuli (high light) kwa kutumia left click na kudrug pamoja, kivuli kitaingia (high light) sehemu husika
3) right click ndani ya dirisha la application menu itakuja chagua copy
4) kafungue file jengine unakotaka kupeleka hayo mambo
5) right click ndani ya file jipya (husika menu itakuja chagua paste
6) nenda file chagua save wala sio save as hapo utakuwaumemaliza kazi
ANGALIZO
*tofauti ya save na save as ni kama ifuatayo:
-hutumika "save as" ikiwa file ndIo latengenezwa halina location bado
-hutumika "save" ikiwa file laongezwa vitu au la punguzwa vitu yaan file ni kongwe lina location yake kitambo ila limefanyiwa EDITING (EDIT).
-Unapo anzisha file ukitumia save litakubali kusaveka, na dialog box itakuja sababu hilo file halina location ila tu njia hii sio nzuri kwa file jipya maana litakuja kukusumbua huko baada ya muda ukalazimika kutengeneza tena upya (usiulize kwanini utaelewa huko tukiendelea kusoma pia sababu itapewa ikifika wakati husika).
BACK SPACE------DELETE
back space: ni kufuta herufi au neno lilioko kabla ya cansor.
tunapo back space lazima tusave kabla ya kufunga file
kudelete lazima tuainishe herufi au neno tunalotaka kudelete
HATUA ZA KUDELETE NI KAMA ZIFUATAZO:
a) ainisha neno au herufi kwa kuhigh light(kivuli),
b) binya button ya delete herufi au neno husika litafutika,
c) lazima kusave kabla ya kufunga file,
d) hatua za kudelete hapo juu zinahusu herufi au maneno (kipande cha file) ama kudelete file fungua location liliko file husika weka kivuli kwa click file husika litaingia kivuli menu itatokeza chagua delete au lileft click file husika litaingia kivuli bonyeza button ya delete.
ANGALIZO
Tunapo delete file huwa tuna lengo la kuliondosha ndani ya kombiuta ili lisiwemo kabisa...lakini yeye kombiuta haliondoshi kabisa kwa kuhofia pengine tumelifuta kimakosa kutokana na hali hiyo kombiuta analiondoa kwenye location na kulipeleka sehemu nyengine (recycle bin) ili kama tumelifuta kimakosa tupate kulirejesha
NADHARIA YA RESTORE
Katima maisha ya kawaida hutokea tukahitaji kuyafikia mambo fulani, kwa bahati baada ya kuyafikia mambo hayo hutokea pia tusiyahita na tukawa na shauku ya kujiweka mbali na mambo husika.
Katika matumizi ya kombyuta huwa tuna hitaji kuwa na files zitakazo tusaidia katika kuyaendea mambo fulani au kufikia malengo fulani. Pia hutokea kuwa baada ya kuyafikia malengo husika ikawa tusihitaji tena kuendelea kuyahifadhi ma-file tulio yatumia katika kuyaendea malengo yetu.
Bali hutokea hata ma-file husika kugeuka kuwa ni mzingo unao tuchukulia nafasi katika storege zetu. Inapo fikia hali ya kuyaona ma-file kuwa ni mzigo usio na faida kwa wakati husika ndipo hutupelekea kufuta ma-file husika kwa lengo la kupata sehemu kubwa ya kuweka ma-file mapya tuliyo kuwa na haja nayo kwa wakati husika.
Vivyo hivyo wakati wa kufuta ma-file tusio ya hitaji hutokea tukafuta kimakosa hata ma-file tulio kuwa tuna ya hitaji. Hapo sasa ndipo tunahitaji kufanya restore.
HATUA ZA KULIREJESHA FILE TULILO FUTWA KIMAKOSA NI ZIFUATAZO:
1) nenda desktop tafuta icon iliyo andikwa recycle bin.
2) double click kwa left mouse recycle bin itafunguka.
3) tafuta hilo file husika au folder husika right click menu itatokeza chagua restore hilo file litarudi katika location liliko kuwepo awali...ikiwa hulihitaji file husika ulikusudia kuliondosha humo humo ndani ya recycle bin zifanye hatua za kudelete file ukifanya hivyo hilo file huwezi ukalipata tena ndani ya computer
NADHARIA YA FOLDER
utangulizi:
tuliposoma partion tuligusia folder kumbe tumeshapata maarifa kuhusina nafolder leo tutaongelea aina za folder zinazo kutwa ndani ya computer aina za folder:
1) folder za asili zisizo kosekana ndani ya computer zina kuja na computer kutoka kiwandani kama zifuatazo:
-recycle bin: ni folder linalo tunza mafaili yanayofutwa ili tuyarejeshe ikiwa tulifuta kimakosa
-my document ni folder linalo kuja ndani ya computer ili tuhifadhie vitu vyetu ndani kwa lengo la kuwa zuia watu wengine kuona vitu vyetu, kwa sharti hiyo my document yetu tuiwekee ulinzi (nadharia ya user)
-library ni folder linakuja ndani ya computer lina mafile madogo madogo ndani (my picture ,down load ,video, music...)
-folder la kawaida ni folder lolote analotengeneza mtumiaji
-directtory ni folder lililo beba faili lililo funguka katika computer kwa wakti husika
-desktop ni moja ya mafolder asili, kazi yake ni zifuatazo:
· kumpokea mtumiaji anapo fungua computer, yaani anacho kiona hapo anapo fungua kompyuta hicho ndio desktop
· kushikilia icon (short cut) za programu zilizomo katika kompyuta
· kuweka vitu mafaili na mafolda mengine.
HATUA ZA KUTENGENEZA FOLDER
1) fungua partion au location unapo taka kuliweka folda unalo kusudia kulitengeneza.
2) right click popote ndani ya location husika, menu itakuja.
3) chagua new, halafu folder.
4) andika jina la folda.
-------mwanzoni mwa somo la folder tuliambizana kwama folder huwa linamuundo wa kitabu cha rangi ya njano ila tutambue kwamba kuna mafolder mengine yasiyo na rangi njano wala muundo wa kitabu. Kitu chochote ndani ya computer kisichokuwa partion iwapo kina sifa ya kuweka mafaili kitaitwa folder hata kama hakina muundo wa kitabu walla rangi ya njano.
Mfano :
recycle bin,
library
pictures,videos...
ANGALIZO:
--folder lolote la asili komyuta hawezi kukuruhusu ulifute katu.
--huko juu tumesoma makundi ya icon kuna haja ya kuashiria aina za icon
AINA ZA ICON NI KAMA ZIFUATAZO:
1) icon halisi
2) short cut: ni kivuli cha icon halisi. short cut hupatikana sana katika locotion ya desktop kuliko location nyenginezo ili kuturahisishia kupata application tuitakayo bila kupitia start menu tutaijua icon ya short cut kwa alama ya mshalE.
ANGALIZO:
icon ni alama inayo tusaidia kulifanya jambo kwenye computer
1)qattu usifute icon isiyo na mshale (icon halisi) maana utapotelewa vitu vyako .
NJIA ZA KUTENGENEZA SHORT CUT
1)fungua partion liliko file husika au icon husika.
2) right click icon husika au file husika itakuja menu
3) chagua send icon to deskk top
4) tayar hiyo short cut itakuwepo desk top
NJIA YA KUSHIKILIA PROGRAM KWENYE TASK BAR
1) right click icon ya program ya application husika menu itakuja
2) chagua pin to task bar
3) utaikuta hiyo application imegandana kwenye task bar.
DATA AND EXTENSIONS
tulipo soma kuhusu application tulikuwa tuna kuandaa upate upate kueelewa data nini, na kuna aina ngapi za data pia upate kuelewa tofauti zilizo kuwepo baada ya data zaina moja, yaani application moja inaweza kutengeneza data za aina tofauti. Inapo tendeneza application aina tofauti ya data, data hizo hutofautikana kwenye EXTANSION. (kama tunavyo jua chakula andazi kina aina tofauti ya aandazi. Vivyo hivyo data za aina mojo zinaweza kuwa na tofauti baina yake)
Data ni nini?
Data ni kitu chochote kinacho weza kuchakatwa na kompyuta, ambazo zinaweza kuhifadhiwa na kupitishwa kwa njia ya ishara za umeme na vikamfaidisha mtumiaji wa kompyuta
AINA ZA DATA NA EXTENSION ZAKE:
1) audio (sauti),
mfano wa extension zake: MP3, AMR
2) picture,
mfano wa extension zake: PNG, JPG, …
3) video (picture na sauti):
MP4, 3GP, …
4) application (program,vielelezo vya utengenezaji kwa wanao tenengezaji software)
mfano wa extension zake: Application haziendi kwa extension bali kwa viersion.
kila data katika data tulizo zisoma hapo juu ina application yake maalum inayo zinda, nazo ni kama zifuatazo:
1)data za maandishi application zake zinaitwa text editor
2)data za picha appliication zake zinaitwa photo editor au imeg editor
3)data za sauti zinatengenezwa na application iitwayo audio editor
4)data za video zinatengenezwa na application iitwayo vidio editor
5)application zinatengenezwa na application iitwayo kompale (compiler)
hizo application tulizo zisoma hapo zimetofautiana pia ubora hata kama ni application mbili tofauti zinazotengeneza ainna moja ya data mfano tunaweza tukawa na aina tano za tofauti za text editor au audio editor au image editor....
ni kwa kuwa tu kila application imetengenezwa ikiwa na ubora wake maalum.
PART FOUR: NYANZA ZA ELIMU YA KOMPYUTA.
UTANGULIZI:
komputa ni chombo kilicho leta mageuzi makubwa sana katika maisha ya walimwengu katika kila nyanza. Bali chombo hiki kimekuwa ni chombo kombozi cha watu kiuchumi, kitaaluma na kijamii. kombyuta imewafanya walio kosa fursa ya kielimu katika umri wao wa utototoni, kujikumboa kitaaluma na kufika daraja kubwa sana kielimu hali ya kuwa wamecelewa sana kusoma. Bali wengine walizuiwa kuendelea na masomo baada ya hapo walijiendeleza leo hii wameibuka kuwa matrilionea duniani kupitia kompyuta.
Tulio yasoma katika part 1, 2, 3 ni mambo ya msingi sana kwa kila anaye amiliana ya kombyuta , kuyajua maana vyuo vyote duniani hulazimika kumsomeshwa kila mwanafunzi aliye na nia ya kusomea kombyuta. Punde tu baada ya kusoma yalio tangulia tumependelea kukupitisha kidogo upate japo vionjo vya baadhi ya fani za kompyuta ziliopo vyuoni na katika vituo vya mafunzo ya kompyuta duniani ili upate kuwa na maamuzi sahihi kuhusu fani gani katika nyanza za kompyuta utakayo jiunga nayo baadae.
PART FOUR. A) COMPUTER NETWORK CONCEPT
Kompyuta Network ni nini?
Kompyuta netwok ni muunganisho wa vifaa vingi (kompyuta na vyenginevyo), ambavyo vimeunganishwa kwa kutumia njia nyingi kwa madhumuni ya kubadilishana taarifa kwa kutuma/kupokea data. Mitandao ya kompyuta pia hujumuisha vifaa vingi vinavyosaidia katika mawasiliano kati ya vifaa viwili tofauti; hivi vinajulikana kama vifaa vya Mtandao na ni pamoja na vitu kama vile vipanga njia, swichi, vitovu na madaraja.
Fungua mfumo (open system): Mfumo ambao umeunganishwa kwenye mtandao na uko tayari kwa mawasiliano. Mfumo uliofungwa (closed system): Mfumo ambao haujaunganishwa kwenye mtandao na hauwezi kuwasiliana nao.
OSI: OSI inasimama kwa Open Systems Muunganisho. Ni muundo wa marejeleo unaobainisha viwango vya itifaki za mawasiliano na pia utendakazi wa kila safu. PROTOCOL: Itifaki ni seti ya sheria au algoriti ambazo hufafanua jinsi vyombo viwili vinaweza kuwasiliana kwenye mtandao na kuna itifaki tofauti iliyofafanuliwa katika kila safu ya muundo wa OSI. Chache ya itifaki hizo ni:
TCP,
IP,
UDP,
ARP,
DHCP,
FTP na kadhalika.
VITAMBULISHO VYA KIPEKEE VYA MTANDAO (NETWORK UNIQUE IDENTIFIERS) HOST NAME: Kila kifaa kwenye mtandao kinahusishwa na jina la kipekee la kifaa kinachojulikana kama Jina la Mpangishi. Andika "jina la mpangishaji" kwenye kidokezo cha amri (Njia ya Msimamizi) na ubonyeze 'Ingiza', hii inaonyesha jina la mpangishi wa mashine yako.
NETWORK TOPOLOGIES
AINA ZA NETWORK
(Picha namba 20)

(Picha namba 21)

PART FIVE. B) INTERNET CONCEPT
tutaidadavua siku chache zijazo
PART SIX. C) DATABASE CONCEPT
Data ni nini?
Database ni nini?
Mfumo wa usimamizi wa hifadhidata (au DBMS) kimsingi sio chochote zaidi ya mfumo wa kompyuta wa kutunza data . Watumiaji wa mfumo husika hupewa vifaa vya kufanya aina kadhaa za shughuli kwenye mfumo kama huo kwa upotoshaji wa data kwenye hifadhidata au usimamizi wa muundo wa hifadhidata yenyewe.
Mfumo wa usimamizi wa hifadhidata (DBMS) ni kifurushi cha programu iliyoundwa kunitolea, kudhibiti, kupata na kudhibiti data katika hifadhidata. DBMS kwa ujumla huchezea data yenyewe, umbizo la data, majina ya sehemu, muundo wa rekodi, na muundo wa faili. Huwapa watumiaji na watayarishaji programu njia ya kimfumo ya kuunda, kurejesha, kusasisha na kudhibiti data. Kazi za Mfumo wa Usimamizi wa Hifadhidata: Mfumo wa Usimamizi wa Hifadhidata hufanya
kazi zifuatazo:
1. Usimamizi wa Kamusi ya Data, 2. Usimamizi wa Hifadhi ya Data, 3. Ubadilishaji Data na Uwasilishaji, 4. Usimamizi wa Usalama, 5. Udhibiti wa ufikiaji wa watumiaji wengi, 6. Usimamizi wa Hifadhi Nakala, 7. Usimamizi wa Uadilifu wa Data, 8. Lugha za Ufikiaji wa Hifadhidata na Kiolesura cha Maombi, 9. Database Mawasiliano Interface.
(a) Usimamizi wa Kamusi ya Data
Kamusi ya data huhifadhi ufafanuzi wa vipengele vya data na uhusiano wao. Taarifa hii inaitwa metadata. Metadata inajumuisha ufafanuzi wa data, aina za data, uhusiano kati ya data, vikwazo vya uadilifu n.k. Mabadiliko yoyote yanayofanywa katika muundo wa hifadhidata yanaonyeshwa kiotomatiki katika kamusi ya data. Kwa kifupi DBMS hutoa uondoaji wa data na huondoa utegemezi wa kimuundo na data kutoka kwa mfumo.
(b) Usimamizi wa Kuhifadhi Data
DBMS huunda miundo changamano inayohitajika kwa uhifadhi wa data. Watumiaji wameachiliwa kutokana na kufafanua, kupanga na kutekeleza sifa changamano za data za kimwili.
(c) Ubadilishaji Data na Uwasilishaji:
DBMS inasaidia uhuru wa data. Kwa hivyo DBMS hutafsiri ombi la kimantiki katika amri ambazo hupata na kurejesha data iliyoombwa. DBMS huunda data iliyorejeshwa kulingana na vipimo vya umbizo la data kimantiki.
(d) Usimamizi wa Usalama:
DBMS huunda mfumo wa usalama unaotekeleza usalama wa mtumiaji na faragha ya data ndani ya hifadhidata. Sheria za usalama huamua haki za ufikiaji za watumiaji. Ufikiaji wa kusoma/kuandika unatolewa kwa mtumiaji umebainishwa kwa kutumia haki za ufikiaji. (e) Udhibiti wa Ufikiaji wa Watumiaji wengi: DBMS huhakikisha kuwa watumiaji wengi wanaweza kufikia hifadhidata kwa wakati mmoja bila kuathiri uadilifu wa hifadhidata. Kwa hivyo hifadhidata inahakikisha uadilifu wa data na uthabiti wa data.
(f) Usimamizi wa Hifadhi Nakala:
DBMS hutoa chelezo na taratibu za kurejesha data ili kuhakikisha usalama na uadilifu wa data. Mfumo wa DBMS hutoa huduma maalum ambazo huruhusu DIM kufanya utaratibu na taratibu maalum za kuhifadhi na kurejesha. Usimamizi wa Urejeshaji unashughulika na urejeshaji wa hifadhidata baada ya kutofaulu.
(g) Usimamizi wa Uadilifu wa Data:
DBMS inakuza na kutekeleza sheria za uadilifu ili kuondoa matatizo ya uadilifu wa data, hivyo basi kupunguza upunguzaji wa data na kuongeza uwiano wa data.
(h) Lugha za Ufikiaji Hifadhidata na Kiolesura cha Maombi:
DBMS hutoa ufikiaji wa data kupitia lugha ya maswali. Lugha ya kuuliza ni lugha isiyo ya kiutaratibu ambayo ni mtumiaji anahitaji tu kubainisha ni nini kifanyike bila kubainisha jinsi ya kufanywa. Lugha ya maswali ya DBMS ina vipengele viwili: lugha ya ufafanuzi wa data (DDL) na lugha ya upotoshaji wa data (DML). DBMS pia hutoa ufikiaji wa data kwa watengeneza programu kupitia lugha za programu.
(i) Violesura vya Mawasiliano vya Hifadhidata:
Watumiaji tofauti wanaweza kufikia hifadhidata kupitia mazingira ya mtandao. Kwa hivyo DBMS hutoa kazi za mawasiliano kupata hifadhidata kupitia mazingira ya mtandao wa kompyuta.


FAIDA ZA DATABASE
Mfumo wa Usimamizi wa Hifadhidata (DBMS) ni seti ya programu inayoruhusu ufikiaji, urejeshaji na utumiaji wa data hiyo kwa kuzingatia hatua za usalama zinazofaa . Mfumo wa Usimamizi wa hifadhidata (DBMS) ni muhimu sana kwa ujumuishaji bora wa data na usalama wake.
Hifadhidata kwa kawaida imeundwa ili iwe rahisi kuhifadhi na kupata habari. Hifadhidata nzuri ni muhimu kwa kampuni au shirika lolote. Hii ni kwa sababu hifadhidata huhifadhi maelezo yote muhimu kuhusu kampuni kama vile rekodi za mfanyakazi, rekodi za shughuli, maelezo ya mishahara n.k.
COMPONETS OF DBMS
Hard ware
Software
Data
Procedure
Database access language
AINA ZA DATA BASE
Aina nne za mifumo ya usimamizi wa hifadhidata:
mifumo ya hifadhidata ya kihierarkia. mifumo ya hifadhidata ya mtandao. mifumo ya hifadhidata yenye mwelekeo wa kitu.
tutaidadavua siku chache zijazo
PART SEVEN. D) PROGRAMMING CONCEPT
tutaidadavua siku chache zijazo
PART EIGHT. E) GRAPHICS CONCEPT
tutaidadavua siku chache zijazo
PART NINE. F) MAINTENACE CONCEPT
tutaidadavua siku chache zijazo
PART TEN. G) TYPING CONCEPT
tutaidadavua siku chache zijazo
kwa mukhtasari huu katika part four tumejitahidi kukupatia taswira ilio jirani na kukamilika kuhusu fani mama za kompyuta. Kama kuna fani utakayo kwenda kutana nayo na ikawa hujaiona katika hizo tulizo orozesha hapo juu, utambue kuwa fani hiyo imetokana na moja ya hizo tulizokuorodhesha ila wewe ndio kukuwa na upeo wa kugundua.
Karibuni sasa katika fani ya TYPING, ili upate kujiajiri mwenyewe na kwa mtaji mdogo kabisa utakao kukomboa na ukata wa maisha.
MLANGO WA PILI : VITENDO
Sehemu hii ni sehemu ya vitendo baada ya kusoma nadharia ya maarifa ya matumizi ya kompyuta
TAFADHALI MAKALA HII INAENDELEA UKUSANYAJI WAKE
Comments