MAKALA NI NINI ?
- Gshtargets
- Jan 8, 2022
- 3 min read
Updated: Jan 22, 2023

MAARIFA YA UANDISHI WA MAKALA
Utangulizi
Kama isemavyo kwamba ” umleavyo mwanandivyo akuwavo ” , basi sina budi ila kuandika nyaraka hizi chache kwa lengo la kuwazindua walio ghafilika au walio jisahaulisha athari na tija ya msemo nilio uashiria hapo juu.
Walio wengi katika jamii ya wasomi, khasa katika jamii ya kitanzania wamekuwa mbali na kuhimiza au kuwazoesha watoto wao tasnia ya uandishi wa makala pamoja na walio wengi kuelewa umuhimu wa elimu kwa watoto wao.
Uhalisia wa walio wengi kuto kunufaika kitaaluma na elimu ya vyuo vikuu na kudhihiri wimbi kubwa la madai ya ukosefu wa ajira hutokana na vijana wengi kutokuelewa kwamba lengo la elimu sio kuletewa ajira bali kuitengeneza.
Katika uandishi wa makala hii kinacho lengwa ni kile walio kipuuza watu wengi nacho ni tasnia ya uandishi wa makala. Karibuni mfuatilie.
Maana ya makala Makala ni muundo mfupi wa utunzi rahisi wa maandishi unao husu jambo maalumu au kipengele fulani cha jambo husika , makala huandikwa kwa moja ya malengo ya fuatayo:
Utafiti mfupi ya jambo lisilo tambulika uhalisia wake,
Taarifa fupi kuhusu muendelezo mpya wa jambo lililo wahi kutambulika hapo awali,
Ripoti fupi ya jambo baada ya kutekeleza ufuatiliaji.
Sifa za makala
1. Wepesi wakufahamika na msomaji wa kawaida hata kama mhusika hana maarifa sana ya jambo husika.
2. Makala huelezea maoni ya mwaandishi tu, wala si vyenginevyo. Yaani sio ajabu kuandikwa makala nyengine kwa lengo la kupinga makala ya awali. Hata hivyo kitaaluma ni kwamba tofauti ya mawazo sio hoja ya msingi ya kuto kuheshimu hisia au mawazo ya waandishi wa makala za watu wengine,
3. Hushauriwa kutimika lugha isiyo ya dharau katika uandishi wa makala ili kuondoa hali ya kujikweza kwa muandaaji wa makala husika,
4. Hushauriwa kutoa mukhtasari wa mada nyengineyo inayo fanana na mada inayo elezewa katika makala husika, kiasi cha kuwaondolea mkanganyiko wafuatiliaji wa makala husika na kuitofautisha na makala inayo shabihiana nayo
5. Makala huwa na mshikamano wa uuiano kati ya ibara zake tofauti zinzo hudumia wazo la makala moja bila kuashiria makala nyingi zene mawazo tofauti na lazima kuwe na mpangilio wa hoja ili kufikisha wazo kwa mfuatiliaji.
6. Makala hushauriwa kuwa saizi fupi inayo tosheleza kuwasilisha wazo.
Faida za maarifa ya uandishi wa makala
Tasnia ya uandishi wa Makala ina faida nyingi sana kwa wanajamii hususan katika zama hizi za ukuwaji wa elimu. Kati ya faida hizo kuna zinazo ihusu jamii kwa jumla na faida zinazo mhusu mwandishi kwa sifa za kipekee. Baadhi ya faida zenyewe ni kama zifuatazo:
· Zinazo ihusu jamii:
Taarifa, repoti au habari kwa wanajamii,
Moja ya njia za kuleta na kuhimiza mabadiliko ya kijamii
· Zinazo mhusu mwandishi:
Moja ya njia za kudhihirisha hisia binafsi
Kukuza uwezo wa kufikiri,
Njia ya kipakee kwa mwanafunzi kumpa umakini na umahiri katika uandhishi ya tatiti za uhitimu,
Kuongeza ubunifu wa kimawazo,
Kukuza maafira na usambazaji wa maarifa husika kwa wanajamii,
Katika zamaa hivi za utandawazi na wingi wa vyombo vya habari uandishi wa makala ni moja ya njia za uhakika katika kujiongezea kipato bila jasho wala mutumia nguvu.
Vipengele vya uandishi wa makala
Makala huundwa kwa kuzingatia vipengele kadhaa navyo ni kama vifuatavyo:
·Wazo la uandishi wa makala
·Anwani (kichwa cha habari) ya makala
·Ufundi wa lugha itayo tumiwa katika uandishi wa makala
·Utangulizi katika makala
·Yaliyomo (ibara tofauti za makala za makala)
·Hisia za mwandishi wa makala
·Hitimisho la wazo la makala
Rejea za nukuu zilizotumika katika makala
Aina za makala
Kuna aina nyingi sana za makala katika tasnia ya uandishi wa makala jambo lililo changiwa na tofauti za maoni ya wanataaluma katika faani na tasnia ya uandishi na tafiti.
Kwa leo sio busara kuelezea aina hizo japo kwa ishara maana suala hilo lina mkanganyiko mkubwa katika kufuatilia vigezo na mashari ya kuainisha makundi tofauti ya makala.
Hata hivyo sitokuwa bakhili wa kukujuzeni kwamba zama hizi za kukuwa kwa elimu na teknolojia tulizo nazo zimebadili tasnia nzima ya uandishi wa makala na kuteta muono na aina mpya ya makala. Sasa hivi kuna makata kuu tatu kuu ukizingatia uwasilishaji. Nazo ni kama zifuatazo:
1. Makala ya maandishi
2. Makala ya sauti
3. Makala ya picha na sauti.
Hatima ya nyaraka hizi Katika jamii ya wanaojitambua tasnia ya uandishi wa makala inekuwa ni chachu kubwa sana ya kuepuka madai ya ukosefu wa ajira. Bali tukiendelea na madai ya ukosefu wa ajira tunaweza kuwa ni sababu ya kukejeliwa kwa elimu, ambo lisilo sahihi. Kuna haja kubwa tena tukabadili namna ya kudhihirisha hisiya zetu kuhusu suala la ukosefu wa ajira. Tuiache elimu itwe elimu wala isikejeliwe bali wa kukejeliwa ni yule aliye kosa kujinufaika kitaaluma na elimu aliyo soma. Uandishi wa makala ni moja ya matunda elimu na utatuzi halisi wa uhaba wa ajira katika jamii zote duniani hususani zame hizi za utandawazi na kukithiri kwa vyombo vya habari.
BOFYO PICHA HAPO JUU TEMBELEA MAKALA ZA WASHINDI WETU
Comments